Polisi watuhumiwa kuwa majambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi watuhumiwa kuwa majambazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Polisi watuhumiwa kuwa majambazi


  [​IMG] Arusha: Mmoja atoroka na bunduki, alihusika katika ujambazi
  [​IMG] Rukwa: Mmoja akamatwa kwa kukwapua pesa kwenye ATM
  [​IMG] Mara: Mmoja akamatwa kwa kutorosha mhalifu mahabusu
  [​IMG] Mwanza: Kisiwa Ukerewe wadaiwa kusaidia majambazi  [​IMG]
  Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la Polisi nchini limekumbwa na kashfa kubwa, kufuatia polisi wake kadhaa kutuhumiwa kuhusika katika mfululizo wa matukio ya uhalifu nchini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kuhusishwa kwa polisi hao katika uhalifu kunalitia doa kubwa jeshi hilo hivyo kuonekana mbele ya umma kuwa limebadili lengo lake la kuwalinda raia na mali zao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika tukio la kwanza, askari wa polisi mkoani Arusha, Mvanga Balele (30), ametoroka na bunduki aina ya SMG, redio ya upepo mali ya jeshi hilo baada ya kudaiwa kuhusika katika tukio la unyanganyi wa kutumia silaha katika eneo la Njiro.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hali kadhalika jeshi hilo linamshikilia askari mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Frank pamoja na pikipiki ya askari aliyetoroka yenye namba T133BAB ambayo ndio ilitumika katika tukio hilo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Tukio hilo ambalo limethibitishwa na jeshi la polisi mkoani hapa lilitokea juzi katika eneo la Njiro baada ya watu watatu akiwemo askari huyo kuvamia katika duka la vifaa vya ujenzi la Kitonga, lakini kabla ya kutekeleza uhalifu huo walizingirwa na polisi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika tukio hilo mtuhumiwa mwingine wa ujambazi, Hilary Kibauli (24), aliuawa na polisi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo baada ya majambazi hayo kuzidiwa nguvu na askari sita wa doria walianguka katika mtaro na mmoja alifanikiwa kutoroka na Kibauli alipohojiwa aliwataja wenzake wakiwemno hao wawili.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilio Matei, alisema kuwa askari huyo alitoroka pamoja na familia yake muda mfupi baada ya tukio hilo na kwamba hajuliakani alipo mpaka sasa.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Askari huyo alitoroka na tulituma vijana kufanya upekuzi na walifanikiwa kukuta vifaa vya kujibadlisha sura nyumbani kwake na tunaendelea kumsaka kwani tukio hili limefedhehesha jeshi, ni aibu kubwa,” alisema Matei.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha Kamanda Matei alisema kuwa Kibauli ambaye alifariki dunia juzi jioni ndiye aliwataja askari hao kujihusisha na mtandao wa ujambazi wa kutumia silaha mkoani hapa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Matei alifafanua kuwa askari huyo alitakuwa katika lindo eneo la Njiro siku ya tukio, lakini uchunguzi ulionyesha kuwa hakufika eneo la ulinzi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alifafanua kuwa siku ya tukio, jeshi hilo lilipata taarifa za siri kuwa kuna majambazi ambayo yalipanga kufanya uhalifu na walianza kuwafuatiliwa na kufanikiwa kuwazingira kabla ya kuteleleza uhalifu wao.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya kuzingirwa na mapambano kuwa makali mmoja alipigwa risasi, lakini yule aliyekuwa na SMG alifanikiwa kutoroka na baadaye kuteka gari la wanafunzi na kuwashusha na kuliendesha na baadaye kulitelekeza katika eneo la Kimandolu,” alisema Matei.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alidai kuwa katika mapambanao hayo askari walifanikiwa kumpiga Kibauli risasi kiunoni na kunguka chini ambapo alipiga kelele akiomba asiuawe kwani ana mambo mengi makubwa ya kujulisha polisi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda Basilio alisema kuwa jambazi huyo alianza kuwataja askari wanaojihusisha na ujambazi, lakini baadaye alifariki baada ya kuvuja damu nyingi. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kufuatia tukio hilo, kamanda huyo aliwataka watu wanaowafahamu askari wanaojihusisha na ujambazi kutoa taarifa za siri ili kutokomeza vitendo hivyo katika jeshi. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aibu hii ikiuukumba mkoa wa Arusha, mkoani Mwanza nako polisi imepakwa matope baada ya wananchi kudai kwamba katika tukio la mauaji ya raia 14 wilayani Ukerewe yaliyofanywa na majambazi wiki iliyopita, miongoni mwao kulikuwa na askari polisi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wananchi waliishiwa uvumilivu na kumtaka Mkurugezi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) wa Polisi, Robert Manumba, aondoke na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe kwa madai kwamba amekuwa ni sehemu ya kulinda uhalifu wa polisi dhidi ya raia.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika tukio la tatu, Polisi mkoani Rukwa inamshikilia askari mwenye namba F 5767 Michael Mangi wa kituo cha polisi Namanyere kilichopo katika wilaya ya Nkasi kwa tuhuma za kuiba zaidi ya Sh. milioni moja za mteja kupitia mashine za kuchukulia fedha 'ATM' ya benki ya NMB tawi la Namanyere.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage, alisema mtuhiwa huyo aliiba kiasi cha Sh. 1,063,000.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda Mantage alimtaja mteja huyo aliyegundua kuibiwa fedha zake ni Kasesaunga Joseph (50), mkazi wa kitongoji cha Ipanda kilichopo katika Wilaya ya Nkasi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema mwananchi huyo aligundua kupungua kwa fedha zake Januari 16, mwaka huu, baada ya kufika katika benki hiyo kwa lengo la kuchukua fedha kununulia bati za kuendeleza ujenzi wa nyumba yake.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya tukio hilo mwananchi huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa benki hiyo na maafisa wa benki walibaini kuwa feha hizo zilichukuliwa kwa vipindi tofauti na kuhamishiwa katika akaunti mbili tofauti.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mantage alisema baada ya ugunduzi huo, uongozi wa benki ulitoa taarifa katika kituo cha polisi Namanyere ambapo wamiliki wa akaunti hizo mbili zilizohamishiwa fedha walikamatwa na kwamba katika mahojiano kila mmoja alikiri kuhamishiwa fedha katika akaunti yake na askari huyo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema watu hao walilieleza polisi kuwa walikuwa wakidanganywa na askari huyo kuwa yeye ana akaunti NMB na kwamba aliwaomba akaunti zao ili ndugu zake wamtumie fedha kupitia akaunti zao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwataja watu waliohamishiwa fedha za wizi na askari huyo kuwa ni Martin Magesa (25) ambaye alihamishiwa kiasi cha Sh. 500,000 na Geoffrey Sinkala (26), aliyehamishiwa Sh. 350,000 na kwamba walizichukua fedha hizo na kumkabidhi askari huyo.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda Mantage alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa fedha nyingine alikuwa akichukua kama muda wa maogenzi na kuhamishia katika simu yake ya mkononi.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo uchunguzi huo umebaini kuwa askari huyo alipata namba za siri ya kadi ya ATM za mwananchi huyo siku chache zilizopita baada ya mwananhi huyo kufika katika benki hiyo na kumkuta askari huyo akiwa lindo na kumuomba amfundishe namna ya kutumia kadi ya ATM.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamamda Mantage alisema kuwa askari huyo amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo na anaendelea na mashitaka ya kijeshi na akipatikana na hatia ataadhibiwa kijeshi na kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika tukio la nne, Jeshi la Polisi mkoani Mara limemfikisha katika mahakama ya kijeshi askari wake, Koplo John kujibu tuhuma za kula njama na kumtorosha mmoja wa watuhumiwa watano wa ujambazi na mauaji ya watu watatu yaliyotokea wilayani Bunda wiki iliyopita.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz , alisema Koplo John alifikishwa katika mahakama hiyo jana na kusomewa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa huyo, Mwanzi Nyamsenda (30), mkazi wa Bunda wakati akiwa katika mahabusu ya kituo hicho baada ya kukamatwa na wenzake wanne kwa tuhuma hizo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Boaz alisema ikithibitika kuwa amemtorosha mtuhumiwa huyo, atafukuzwa katika Jeshi la Polisi na kufikishwa katika mahakama ya kiraia.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Boaz alisema Koplo John ni miongoni mwa askari sita waliokuwa zamu siku ambayo mtuhumiwa huyo inadaiwa alitoroshwa kutoka mahabusu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwataja askari wengine kuwa Koplo Michael, WP Luciana, PC Arico, PC Kozi na Sajenti Sospeter.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema Koplo John alifikisha katika mahakama hiyo baada ya kudaiwa kuthibitika kuwa ndiye aliyemtorosha mtuhumiwa huyo.[/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Juzi Kamanda Boaz alisema kutoroka kwa mtuhumiwa huyo kunazua maswali mengi kwa sababu mlango wa mahabusu haukuvunjwa.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Tutatoa taarifa wakati wowote maana mlango haukuvunjwa, lazima tuone mazingira ya kutoroka kwa mtuhumiwa yalikuwaje, ” alisema Boaz.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Januari 16, mwaka huu majira ya saa 8:00 usiku, kundi la watu wanaoshukiwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki yalivamia maduka matatu katika mji mdogo wa Kibara na kuwaua walinzi wawili na kujeruhi mwingine kwa kuwapiga na vitu kizito vichwani na mtu mwingine Kijiji cha Mugara.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, jana hakuweza kutoa ufafanuzi kuhusiana na matukio hayo ya polisi kuhusika katika matukio kadhaa ya ujambazi, baada ya kuieleza Nipashe kuwa alikuwa na mfululizo wa vikao.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Imeandikwa na Wilbroad Tungaraza, Bunda, Juddy Ngonyani, Rukwa na Charles Ole Ngereza, Arusha.[/FONT]
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hii ni skendo tungoje wengine zaidi
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  We need to overhaul our police force.,habari za namna hii ni nyingi sana kiasi kwamba mtu anaweza kuichukulia poa tu lakini this is very serious, ni aibu sana kwa matendo ya namna hii kutokea kwa jeshi la Polisi ambalo tumelipa dhamana ya kutulinda raia na mali zetu..,kuna baadhi ya askari wachache wanaolipaka matope jeshi letu hili.,inabidi wajichunguze vizuri na kuwabaini wote wenye nia ya kutumia nafasi zao kama polisi kufanyia uhalifu then wawe makini sana kwenye recruitment, ni lazima wa-scrutinize background ya mtu kabla hawajamchukua maana wengine unakuta tayari walikuwa na uhusiano na makundi ya kihalifu kabla hata hawajaajiriwa.
   
 4. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wale askari waaminifu wawafichue hao wasaliti wa jeshi, na wapewe adhabu kali hata kunyongwa ili wengine wajue kuwa askari ni kazi ambayo ukisaliti ni kifo. Hawa jama wanasumbua sana, wanaenda waibia hata wale wenye vijiduka vya majani , kama jana nasikia wamefanya kuiteka chanika na kuwaibia wauza dagaa na majani ya chai , hawa ndo wanaoifanya nchi iwe masikini. Unategemea nini kumwibia muuza daga shilingi elfu kumi? Shame on them. Kazi ipo kwa Mw. Raisi Kikwete, manake ni wamesha ipndua nchi hao wahuni, kwa sababu wanafanya watakavyo, Rais anatakiwa aamke, manake maana ya uamiri jeshi inaanza potea. Hawa jamaa wameshaifanya TZ kama Burundi, walaaniwe wote wenye kuisaliti TZ nchi ya Kimasikini
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kuna wakati nilipendekeza kila mtu anunue bunduki yake ajilinde mwenyewe. Nafikiri hiyo italipa zaidi kuliko hii ya kutegemea ulinzi wa polisi ambao kimsingi wao wenyewe ndo vibaka na majambazi. Fikiria umevamiwa, halafu unampigia jambazi simu aje akuokoe!!! aaah, nimekumbuka, kumbe ndo maana ukipiga simu kwamba kuna majambazi, polisi wanakuja masaa mawili baada ya majambazi kutoka!!!? Ila wanawaumiza wenzao wanaofanya kazi kwa moyo wa uaminifu.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hakuna jeshi kwa mtindo huu
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Jan 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  halafu kuna watu mnawapa kichwa kuwa waue tu majambazi!!
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  na Zombe je???
   
 9. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa kuongezea, hata askari wa kituo cha chang'omne ni majambazi. Wanawazushia watu wanaotaka kuwaibia kuwa ni majambazi.

  Jamaa yangu alikuwa ametumwa kuchukua fedha, askari wa doria walimfuatilia tokea benki mpaka walipokuja kumbana pale mbozi road na kutaka kumpora fedha zake huku wakisema wamemhisi ni jambazi.

  Palikuwa na patashika nguo kuchanika mpaka walipofika kituoni ndipo alipofanikiwa kuokoa fedha zake.

  Niliwaasa, yatupasa kuangalia hawa jamaa wanaposema wamefanikiwa kuua majambazi. Huwa wanauwa raia wema. Unajua tena marehemu hawezi sema. Na akisema hawezi ulizwa.
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi na CCM inawahitaji sana, hasa litakapofika zoezi la kuwatangaza wabunge wa CCM ambao practically wananchi hawakuwachagua ila kwa kuwa CCM wanadola basi wataamu hivyo, ni dhahiri kuwa tuhuma hizi zitawekwa kipolo ili polisi wasiasi kuwapiga wananchi watakaopinga matokeo hayo kwa maandamano. What a country!!
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli,mbona inatisha sana.
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Umemkumbuka eeh! Huyu sijui kama yupo hapa nchini TZ
   
Loading...