Polisi watuhumiwa kumuua mahabusu

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Same. Jeshi la Polisi wilayani Same mkoani Kilimanjaro limeingia katika kashfa nzito baada ya wananchi wa mji huu kuandamana hadi kituo cha polisi kupinga kitendo cha baadhi ya polisi kumpiga mkazi wa wilaya hiyo aliyekuwa mahabusu hadi kufa.

Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa marehemu Maftaha Salimu walisema wameamua kuandamana kudai haki kwani ndugu yao alikamatwa Juni 7, mwaka huu na kupelekwa kituoni hapo na baadaye alipigwa sana hali iliyochangia kifo chake.

Dada wa marehemu, Mwanaid Salim akielezea chanzo cha ndugu yao huyo kupoteza maisha alisema, Juni 6 mwaka huu ndugu yao alituhumiwa kuiba taa ya pikipiki (bodaboda) ambapo alikamatwa na polisi kesho yake Juni 7 na kuwekwa mahabusu.

Alisema mara baada ya wao kupata taarifa kuwa ndugu yao yuko mahabusu walimtuma kaka yao na mama kwenda kumwekea dhamana na kufanikiwa kumtoa lakini alikuwa akilalamika kuwa na maumivu ya kupigwa vibaya na polisi.

“Mama alimchukua na kumpeleka nyumbani akiamini maumivu anayolalamika ni ya muda lakini kadri saa zilivyokuwa zikienda ndivyo alivyokuwa akilalalamika kuumwa na alipewa dawa za kutuliza maumivu.”

Alisema ndugu yao huyo hakuweza kutoka na badala yake alisikilizia maumivu kitandani hadi Juni 11, saa 5 usiku hali yake ya afya ilivyokuwa mbaya na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Same, lakini kabla hajapatiwa huduma alifariki dunia.

Kwa mujibu wa dada huyo wa marehemu, ndugu walikutana na kuamua kwenda polisi kujua sababu za kupigwa kwa ndugu yao na polisi kukubali mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi ili ukweli ujulikane.

Alisema waliongozana na polisi hadi katika hospitali hiyo ya wilaya ambapo mwili huo ulipasuliwa lakini cha kushangaza daktari aliyeupasua aligoma kuwapa majibu na kuwataka wakazike ndugu yao kwani majibu hawatayapata kwa siku hiyo. mwananchi
 
mtuhumiwa hana hatia mpaka mahakama itakpoamua vinginevo sasa kichapo polisi cha nini
 
Back
Top Bottom