Polisi watimua mbio kujinusuru na vijana wa CHADEMA

Nabado itafika kipindi watakimbia vivuli vyao bada la raia ,Arusha si Mtwara
 
Arusha ni ukanfa wa gaza. Kitachofuata siku za mbele huenda ni kuhakikisha kuwa rangi ya kijani haionekani popote.

natumaini kuamapinduzi hayaji kwa wote bali uanzia sehemu moja na kisha kusambaa kwa wote..
Arusha nichazo cha mabadiliko kisha kijana mh lema atasambaza mapinduzi hayo kwa nchi nzima..
tutatarajia hata polisi uacha maisha yao yakuamriwa na kwenda kuleta mapinduzi makubwa katika jamii yao ambayo wengi wao wanatoka,pia ambayo wengi nimasikini...
viva ARUSHA
viva TANZANIA
USAWA UNAKARIBIA KUJA TANZANIA....
 
Bora mmewavurumisha maana hawa jamaa wanakera sana dhidi ya wao kujimilikisha zaidi huko CcM
 
kwa maana hiyo benk haina ulinzi na hapo ni Arusha!

Mkuu ilikuwa mida ya saa 11:45 jioni na nilikuwa pale Modern supermarket au maarufu kama RTC wakati hayo yakitukia na wala siyo stori ya kuambiwa. niliondoka saa 12 na lindo lilikuwa empty may be sasa wamesharudi baada ya hali kutulia
 
Sidhani kama ni uoga Mungi. Si rahisi kuwa na SMG halafu ukawa muoga. Nadhani utakuwa ni mpango mkakati kwa kuepusha shari, na hii taarifa mimi binafsi naipokea vizuri. Kuna busara imeamriwa hapo polisi Arusha. Polisi mmefanya busara sana leo Arusha. Big up! Si kila kukimbia ni cowardice. Kukimbia kwingine ni wisdom.
Kweli mkuu manake ukiamua kutumia SMG kujilinda madhara yangekuwa makubwa. Heri nusu shari kuliko shari kamili. Nadhani wamekimbia kujiokoa na kuokoa maisha ya wengine.
 
Wewe unashangaa ppolisi wawili kukimbia wakati kuna 109 ilikuwa imejaza polisi walikimbia na wana silaha zao...

Mkuu hii hofu ya Leo ya polisi sijui imetoka wapi. Nimegundua vita nzuri ni ya kupigana bila maneno mengi kwani baada ya Lema kuvuliwa ubunge walitegemea vurugu kubwa. Walipoona kimya wakafikiri wananchi wamejipanga kwa mambo mamabaya zaidi na wakafikiri wao ni target namba 1. Nahisi kuna jinsi polisi wamejijengea hofu kwa wrong information na ndo maana leo kila kona polisi walikuwa wanazomewa na wakiona nyomi wanatimua hata kama wako ndani ya magari
 
Wasipoangalia huu uadui ukikua yatatokea makubwa na yakutisha
 
Polisi hao bila shaka hawana elimu ya Uraia.Inakuwaje polisi kumkimbia raia pasipo kosa?Iwapo vijana wa CDM walikuwa wanania ya kutaka kuwavamia Polisi hao tena eneo la Benki hapa binafsi siungi mkono kwa vijana hawa.

Soma thread vizuri ni kwamba benki ilipo ndiko kuliko na njia ambayo vijana wa CDM walikuwa wanapita tena wakikimbia huku wakisukuma gari la kamanda Lema na hakuna hata mmoja aliyekuwa na nia ya kuvamia polisi ila tu walipoona polisi walipiga kelele kwa pamoja "haoooo!!!! huku wakiendelea na safari yao ya kumsindikiza Lema kuelekea old Arusha road kuelekea Kijenge na Impala hadi Njiro.
 
ni vizuri wamefanya hivyo kuepusha shari. Nafikiri polisi walitumia busara maana mob justice siyo nzuri siku zote... there is never a mob thinking..
 
Gari la polisi limevunjwa vioo baada ya kupigwa na mawe wakati likipita karibu na viwanja vya NMC
 
Jamani nisaidieni kuelewa, kwani ukiwa polisi utashi unauacha chuoni mara baada ya kumaliza mafunzo. Nina maanisha ule uwezo alioumbwa nao binadamu mwenye akili timamu wa kuelewa jema na baya!

Anyway, huenda wenzetu - masoko wanayonunua bidhaa yana unafuu, mishahara inawatosheleza, watoto wao wanasoma ktk shule ambazo zina madawati ya kutosha, walimu wamelipwa kwa wakati, maabara zina vifaa; na ikawa pia hospital zao ni zile za Apolo kule India; lakini kama si hivyo, basi kuna haja ya kujitathimini.
Yaani, ukombozi wa ndani - wa kujitambua tena kujitambua kweli kweli.
Ni aibu mbele hata ya muumba wao, binadamu mwenye utashi kutumika kama 'toilet paper'
Ni nani anayeipenda mara baada ya kuitumia!
 
ccm mambo yenu mnayoyafanya mnasababisha chuki kati ya polisi na raia,fanyeni mambo yenu kwa busara ya hali ya juu

Mkuu ulichoongea kina mantiki kubwa mno. Viongozi wetu wanapandikiza mbegu mbaya sana kati ya wananchi na polisi kwa ubinafsi wao. Wanatumia jeshi kama chombo cha kutawala kwa mkono wa chuma, kulazimisha yasiyolazimishika, kujiimarisha madarakani, na kuikandamiza demokrasia.

Katika mchakao wote huu ambao hutumia Chain of command (President---> IGP/Waziri husika---> RPCs/RCs /DCs/RCOs ---> Frontliners etc) Ukiangalia level zote huko juu wanakuwa safe kwani wao wanalindwa na kulipwa malupulupu makubwa. Ila ukija kwa frontliners ambao ndiyo hasa waoneaji wa wananchi, ina create mazingira ya chuki na disharmone between frontliners and public. Hii inaweka maisha ya frontliners rehani na maisha public rehani. Polisi ni kaka, dada, mama na baba zetu ambao ni binadamu kama sisi tunaokutana nao sokoni, hospitali, bar, na kila sehemu, ukiacha hao wakubwa ambao wao wamejificha na kutoa amri tu. Kitendo cha polisi hawa kukimbia si cha kufurahiwa ila ni dalili mbaya kuwa sasa nchi inataka kupelekwa kwenye cat and mouse game.

Na ikifikia mahali Polisi wakianza kuwinda raia na raia kuwinda Polisi basi hakuna atakaye salimika hata hao waliopo juu kabisa ya chain of command. Hii inanikumbusha Innocent polisi aliyeuwawa pale manzese baada ya polisi kuonea wananchi. Polisi yule (Mussa Mtunguja) alikuwa akitokea zake kazini kurudi nyumbani na wala hakuwa katika operation, lakini kwa ajili ya hasira za wananchi dhidi ya vitendo vya polisi wakampasua kichwa. Kitendo kile kilikuwa ni ishara ya wazi kwa watawala kuwa polisi wasitumike kukandamiza wananchi kwani kwa kufanya hivyo unakuwa umeweka rehani maisha ya polisi pia. Hata kama serikali ikijigamba itakamata watakaodhuru polisi bado maisha ya polisi aliyedhurumiwa hayatarudi. Kwa nini polisi isifanye kazi yao traditional? (i.e prevention of crime and protection of life and property)

Sir Richard Mayne (1829) wrote about the objective of Police Force as:
"The primary object of an efficient police is the prevention of crime: the next that of detection and punishment of offenders if crime is committed. To these ends all the efforts of police must be directed. The protection of life and property, the preservation of public tranquillity, and the absence of crime, will alone prove whether those efforts have been successful and whether the objects for which the police were appointed have been attained."

Doing anything other than prevention of crime is an abuse of Power and misuse of Police Force.
 
Back
Top Bottom