Polisi watimua kwa mabomu,wananchi wakijaribu kuzuia msafara wa Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi watimua kwa mabomu,wananchi wakijaribu kuzuia msafara wa Rais

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gudboy, Oct 16, 2009.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Na Geofrey Nyang’oro

  JESHI la Polisi jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na risasi za moto kutawanya mamia ya wakazi wa Kipawa waliotanda barabarani kwa nia ya kuuzuia msafara wa rais.

  Wananchi hao walikuwa wakitaka kumfikishia Rais Jakaya Kikwete ujumbe wao wa kupinga kulipwa fidia ya kubomolewa nyumba zao kwa kutumia sheria ya mwaka 1967.

  Sheria ya Ardhi ya 1999 inathaminisha ardhi na nyumba tofauti na sheria ya awali ambayo ilikuwa ikithaminisha nyumba pekee kwa kuwa ardhi ilikuwa mali ya serikali.

  Sheria hiyo pia inamshirikisha mkazi kwenye mchakato wa tathmini, inatoa fedha za gharama za usafiri na kodi ya pango kwa kipindi cha miezi 36.

  Serikali ya mkoa juzi ilitangaza kuanza kulipa fidia jana na ilipanga kuwa malipo hayo yafanyike ndani ya eneo la Gereza la Ukonga, hatua ambayo ilionekana kulenga kuepuka vurugu za wakazi hao.

  Lakini badala ya kwenda Ukonga, wakazi wengi wa Kipawa, ambao wametakiwa wahame kupisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, waliamua kutanda kwenye Barabara ya Nyerere kwa lengo la kuzuia msafara huo wa rais ambaye alikuwa akitokea mkoani Mara.

  Wakazi hao walitanda barabarani wakiwa wamevaa vitambaa vyeupe mikononi na mabango yaliyosomeka sisi wakazi wa Kipawa hatudanganyiki na kulipwa fidia kwa sheria ya zamani" na "hakuna kusaini hundi kwa sheria ya zamani, kauli ambazo wamekuwa wakizitumia kila wanapokutana kwenye harakati zao.

  Kutokana na hali hiyo polisi ililazimika kutoa matangazo kwa kutumia kipaza sauti ikiwataka wakazi hao kutawanyika kwa madai kuwa mkusanyiko huo si halali na umekiuka sheria za nchi, lakini umati huo wa watu ulikaidi ukidai kinachoendelea kufanywa na serikali ni ubabe.

  “Sisi tunapinga kulipwa fidia kwa sheria ya zamani; tumeshaiandikia serikali notisi ya siku tisini tukitaka ibatilishe utaratibu wake la sivyo tunakwenda mahakamani, inakuwaje leo serikali ianze kulipa fidia, kwa nini serikali inang'âng'ânia sheria hiyo hata kukiuka notisi tulizokwishazifikisha mahakamani, alihoji Rajabu Hussein mkazi wa Kipawa.

  Wakazi hao walisema kinachofanywa na serikali ni usanii kwani wanaostahili kulipwa ni wao na si watu waliokwenda kupokea fedha hizo na kumtaka rais aingilie kati sakata hilo.

  Wakazi hao walidai watu wanaopokea fidia wamepandikizwa na si wakazi wa Kipawa huku wakisisitiza kuwa wakazi wa Kipawa ndio waliopo kwenye eneo hilo wakipinga sheria hiyo kutumika.

  Wakati hayo yakiendelea, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Evance Balama aliwasili katika eneo hilo na kueleza kuwa watu wa Kipawa ni wabaya na kwamba hawaitakii mema serikali yao.

  “Polisi hakikisheni watu hawa wanatawanyika,”alisema Balama na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea rais aliyewasili jana kutokea mkoani Mara.

  Kauli ya Balama ilionekana kama kichochea kwani kuanzia hapo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakitumia mabomu ya machozi, walianza kuushambulia umati wa watu uliokuwa umekusanyika katika eneo hilo.

  Polisi hao walikwenda mbali zaidi baada ya kuingia kwenye makazi ya watu karibu na barabara hiyo na kuwapiga na baadaye kumkamata mwenyekiti wao, Mulisa na wasaidizi wake.

  Katika tukio hilo, polisi walimjeruhi mtu mmoja na kusababisha watoto watano kupotea.

  Hali ilikuwa tofauti kwenye maeneo ya Gereza la Ukonga ambako idadi ndogo ya watu ilijitokeza kuchukua hundi za malipo ya fidia zao.

  Akizungumza mara baada ya kuchukua hundi hizo, Hamisi Mvugalo, aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa Kipawa, alisema ameamua kuchukua fedha hizo baada ya kuridhika na kiwango alichokabidhiwa.

  Alisema ameteseka kwa muda wa miaka 13 sasa, lakini baada ya kujua analipwa kiasi gani ameona kinatosha na atafanikiwa kujenga nyumba zake zote mbili na pia kupeleka watoto wake sekondari mwakani.

  Fedha ninayoipata inatosha. Mimi nina watoto wawili wanahitaji fedha kwa ajili ya karo, pia hela hiyo nimeona ni nyingi na itatosha hata kujenga nyumba zangu mbilia alisema Mvugalo.

  Serikali iliwazuia wakazi wa Kipawa kuendeleza makazi yao kwa ahadi ya kuwalipa fidia baada ya kufanya tathmini ya mali zao, lakini tangu tathmini hiyo ifanywe mwaka 1997, wakazi hao wamekuwa wakisubiri fidia bila ya mafanikio huku nyumba zao zikibomoka kiasi cha baadhi yao kulazimika kuhamia kwenye majengo ya Shule ya Msingi ya Kipawa kujihifadhi.

  Lakini baada ya serikali kutenga fedha za fidia, ilitangaza kuwa itawalipa kwa kutumia Sheria ya Ardhi ya 1967, badala ya sheria ya mwaka 1999.

  Afisa ardhi mwandamizi mkoa wa Dar es Salaam, Edgar Japhet alisema wamepanga kulipa fidia kwa wakazi wote wa eneo hilo kwa muda wa siku 45.

  Alisema wamekadiria kuwalipa watu 100 kwa siku na kusisitiza kuwa kama idadi itaongezeka, watazidisha nguvu ili kuhakikisha wote wanalipwa.

  Malipo hayo yalikwenda sanjari na notisi ya siku 45 kwa kila aliyepokea hundi kutakiwa awe amebomoa nyumba yake.

  Msafara wa Rais Kikwete ulipita eneo hilo saa 8:05 mchana na kukuta pande zote za eneo la Kipawa zikiwa zimezingirwa na FFU waliokuwa chini ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile.

  Source: Mwanachi
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  The writting is on the wall


  people are running out of options
   
 3. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #3
  Oct 16, 2009
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kulikua na umuhimu wa kutukia nguvu kwani?
   
 4. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Damn it piss me off. Its shame Makongoro Mahanga has betrayed them. Come 2010 what will this scumbag have to offer? Let us wait and see.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  miafrika bwana........unamvunjia mtu nyumba leo halafu unaithamanisha kwa gharama za mwaka 1967????

  Nadhani serikali ya kikwete ina matatizo, nahisi tunahitaji utawala wa kijeshi basi kama utawala wa kilaia umetushinda.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  we better have a military government rather than having the so called democratic one under CCM
   
 7. F

  Franki Member

  #7
  Oct 16, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba maoni yenu wadau katika hili..Sheria inasemaje?Na hasa wanasheria; "Watu wa Kipawa, wanastahili kulipwa kwa sheria ya 1967 au ya hivi karibuni?"
  Isije ikawa sheria iliyopitishwa na bunge letu,na taratibu nyinginezo, zinawataka wakubali malipo kwa sheria ya zamani, na kuanza mbele kwa mbele! Isije ikawa wanaanzisha vurugu zisizo na maana.
  Au, kwa nini wasiende mahakamani, ambapo tunaambiwa ndiko hasa kwenye haki zetu zote!?
   
 8. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Inawezekana wameona ccm haitapata kura hata moja kutoka kipawa, isingekuwa hivyo wasinge watoa hadi uchaguzi upite.

  Kilichotakiwa hapa ni kutumia busara tu, maana walizuiwa kujenga mwaka 1997, na sheria ilipitishwa 1999, sasa hapo wanatakiwa walipwe kwa sheria ipi?

  serikali inatarajia kupitisha sheria ya kuruhusu kutoa mimba, je walio jela kwa kutoa mimba wataachiwa?
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  nuf said!
   
 10. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hesabu za uwiano walizikimbia
   
Loading...