Polisi watawanya wananchi waliokusanyika kushuhudia misukule mkoani iringa

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,571
ZIMEZUKA habari zenye utata ambazo hazijathibitishwa mkoani Iringa kuwa mtoto mmoja anayedaiwa kufa na kuzikwa kuonekana leo akidaiwa kuwekwa Msukule.
Tukio hilo limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa na kupelekea polisi kufika kuwatawanya wananchi waliokusanyika eneo hilo na kuwasaka wale wanadaiwa kueneza uvumi huo.
Hata hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya waliokuwepo eneo hilo ambaye amethibitisha kuona msukule huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia.
Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule huyo.
 

Attachments

  • 1.JPG
    1.JPG
    46.9 KB · Views: 258
  • 2.JPG
    2.JPG
    38.2 KB · Views: 390
  • 3.JPG
    3.JPG
    57.2 KB · Views: 303
Huyu kamuhanda anapenda force,kuwatawanya 4 what.
Hata kama umejaza chuki nyingi kichwani mwako dhidi ya Kamuhanda...jaribu kuwa muungwana kidogo, je angeacha wachome nyumba ya mtu mwingine kwa imani za kishirikina?? Tumia busara japo kidogo...fikiri kwa akili kidogo kama
nyumba husika ingekuwa ya mama yako...au mtuhumiwa wa uchawi akiwa mkweo ungemlaani Kamuhanda kwa kuwatawanya waliotaka kuchoma nyumba yake moto?? Ninyi ndio mnaosababisha JF ishuke thamani yake kwa kuendekeza ushabiki na uzandiki...
 
Watanzania inabidi tubadilike kwa kweli, yani mtu umesikia kitu hata hakijathibitishwa unafanya maamuzi magumu kama hilo la kutaka kuchoma nyumba ya mtu.

Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
 
haya mambo siyo mageni, hapo kinondoni muslim, gari liliwahi kugonga nyumba na dalini alitoka msukule. Huyo msukule iliidaiwa alizikwa miaka ya sitini na alikuwa na nywele ndefu mpaka nyayoni. Huyu msukule nimemuona kw amacho yangu hapo soko mjinga kinondoni na hupenda sana kuchezadraft au kuangalia bao ila hasemi. wewe nenda hapo soko mjinga halafu ulizia huyu mtu, muuzaji wa sokoni yeyote atakuonesha.
 
Ya Lamadi juzi na jana yalikuwa cha mtoto siyo?

Wachawi wapo ila ni Ole wako usipokuwa na Imani yake Kirsto Bwana wetu!
 
Nasikia huko Iringa mitaa ya Frelimo wananchi wenye hasira walivamia nyumba ya mama Mbilinyi kwa imani kama hizi. Kulikoni Iringa?
 
we will remain poorer and poorer!! Lord Have Mercy on us! stupid US!!
 
haya mambo siyo mageni, hapo kinondoni muslim, gari liliwahi kugonga nyumba na dalini alitoka msukule. Huyo msukule iliidaiwa alizikwa miaka ya sitini na alikuwa na nywele ndefu mpaka nyayoni. Huyu msukule nimemuona kw amacho yangu hapo soko mjinga kinondoni na hupenda sana kuchezadraft au kuangalia bao ila hasemi. wewe nenda hapo soko mjinga halafu ulizia huyu mtu, muuzaji wa sokoni yeyote atakuonesha.
Wasomi Amerika, Ulaya na Asia wanahangaika na kuvumbua mambo makubwa makubwa sisi wasomi wa Kiafrika bado tunaamini na kueneza mambo ya misukule, vibwengo na vinyamkera. Aibu aibu aibu.
 
Nitaenda Tanga kwa huyo mtu ili akanifundishe jinsi ya kufanya. Nina mpango wa kuwaweka MISUKULE viongozi wa Serikali ya CCM wote.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Akili za kiafrika. Mtu kusikia kuna msukule kesha amini na anataka kuchoma nyumba ya watu moto. Akili zetu ni nyepesi na za kushabikiashabikia vitu vya kijinga.
 
Hayo ni mambo ambayo yanachangia kukoleza u umasikini tulionao,jaribu kuangalia ayo mambo yanatokea sana uswahilini kwa nini?hatuoni yanatokea sehemu zile watu wanaishi geti kali,kwa hiyo ktk maisha yetu ya uswahilini mtu anaweza akazusha jambo likasambaa bila ukweli wowote.:laugh:
 
Hivi kumbe haya mambo yapo?kweli nashindwa kuielewa hii technologia ya hali ya juusana.africa hoyeeeeeeee
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom