Polisi watatesa na kuua raia hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi watatesa na kuua raia hadi lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Mar 12, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Nimesoma kwa masikitiko makubwa kuhusu kijana, mwanaume, Mtanzania, aliyefariki baada ya kukamatwa na kuhojiwa na Polisi, hatimaye kufariki akiwa hospitalini, baada ya mateso aliyoyapata akiwa mikononi mwa Polisi kumzidia, hatimaye mauti kumfikia.

  Habari hii imenikumbusha - na kunitia uchungu - yale yaliyowakuta wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, waliouwawa na askari Polisi, na tume iliyoundwa na Rais Kikwete kuwatia hatiani. Lakini vipengele tata vya sheria viliwaweka huru akina Zombe na wenzake.

  Nauliza, askari polisi watatesa na kuaa raia hadi lini? Huu ni ukiukwaji mkubwa wa Katiba juu ya Haki ya Kuishi ya raia, kwani Katiba imeweka wazi juu ya haki hii.

  Hakuna askari polisi mwenye haki ya kuua raia, wala kutoa adhabu yoyote ile kwa raia, ikiwa ni wakati wa mahojiano au upelelezi wa kesi. Lakini Serikali imekuwa ikiyafumbia macho na masikio matukio haya ya ukiukwaji mkubwa wa haki, katiba na sheria.

  Masikini, Mussa Juma amepoteza maisha yake mikononi mwa polisi, waliokula kiapo cha kuwalinda raia na mali zao. Leo polisi ndio wanaokuwa wa kwanza kabisa kuwaua raia! Je, hii ni haki?

  Kwako Rais wetu, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Nakuomba uwawajibishe Makamanda Wakuu wa Mikoa yote ya Kipolisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ili kulinda heshima ya Jeshi la Polisi, kwani sasa, sisi wananchi hatuna imani nalo.

  Pia, nakuomba uunde Tume ili kuchunguza kwa undani mauaji haya ya binadam huyu asiye na hatia.

  Ukweli ni kwamba, wako askari WABAYA sana ndani ya Jeshi hilo, wanaoshirikiana moja kwa moja na wahalifu, wakiwalea na kuwafuga, kwa kuwa ushirika huo ni haramu wenye malengo ya maslahi binafsi, jambo ambalo ni ufisadi mkubwa kabisa!

  TUNATAKA HAKI ITENDEKE! Rais, TIMIZA WAJIBU WAKO!

  ./Mwana wa Haki
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Nilishasema police wa TZ wanauwa raia kwa rate sawa na majambazi yanavyoua watu mitaani au zaidi,inasikitisha sana lakini dawa yao hawa sio serikali kuwakomesha,katika History inaonyesha inaweza kuchukua mtu mmoja tuu kukomesha ubazazi kama huu,angalia States sheria nyingi za kibaguzi sio serikali ilianza kuziondoa,ni watu wachache waliosema "ENOUGH",angalia kesi ya Brown Vs Board of Education hii ilikomesha ubaguzi kwenye elimu America nzima forever,angalia interracial marriage in virginia jamaa walichoka kunyanyaswa wakafight Court ikachange America nzima,rudi kwenye KKK walivyokomeshwa na watu binafsi wakajikuta wanaishia maana serikali iliwashindwa,watu walichoka kuwa terrorized wakaamua kupambana nao mahakamani maana walikuwa wanawaletea lawsuits kama mvua na kuishia kufilisika...dawa ya police wa Bongo ni kwenda against mmoja mmoja kumfanya fundisho kwa wengine huku wengine wakisukuma bunge kuweka sheria zaidi za kulinda Raia kutoka kwa hawa polisi,lakini hii inahitaji watu smart & money na media yenye akili.
   
 3. P

  Preacher JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye kufahamu sheria - ni sawa polisi wa patroli kumfuata raia usiku wa manane (saa 7) na kugonga gate lake kwa nguvu wakidai afungue waingie? Hata kama ameshitakiwa je mchana wote mbona wasimkamate? na pia watumie maneno ya kumtishia kumdhalilisha?? Je mtu akipatwa na kitendo kama hiki anawashitaki wapi?? anayefahamu anijulishe nimsaidie ndugu yangu aliyekumbwa na mkasa huu.

  Nawasilisha
   
 4. M

  Mchili JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Inafaa ndugu wa marehemu wariport tube ya haki za binadamu suala hili na wawepo wakati wa postmotum. Matukio kama haya ndio chanzo cha vurugu katika jamii manake itafika mahali watu wataresist any atempt of police arest. Ikiwezekana wanaharakati wa haki za binadamu na NGOs watoa mwanasheria wa kujitegemea ashuhudie postmotum na afanye upelelezi binafsi kabla ya mashitaka, wasije wakafungua mashtaka feki kama ya akina Zombe.

  Kwa kweli inasikitisha kupoteza uhai wa kijana kama Musa, nguvu kazi ya taifa hili na tegemezi la familia yake. |Polisi wanajiamini sana hasa baada ya kina Zombe kuachiwa huru.

  Ona walichotaka kumfanyia Muro. Tusipochukua action, any of us can taste the same experience. Leo kwa Mussa, kesho kwangu na wewe. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu aliyekufa kwa mateso makubwa.
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kisheria hairuhusiwi kumkamata mtu kwake ikifika 12 jioni mpaka 12 asubuhi. Kama wanataka kukukamata inabidi waizingire nyumba usiku kucha mpaka asubuhi. Pia hairuhusiwi mtu kukamatwa nyumbani bila kuwepo Kiongozi wa mtaa, na pia hata kama wanataka kukupekua nyumbani kwako kwa muda ulio sahihi, inabidi uwe na mashahidi na pia kabla hawajakupekua unatakiwa kwanza uwapekue wapekuaji wasije kuingizia kitu wakakusingizia.

  Lakini masharti yote hayo jaribu kuwauliza Polisi wetu wakija kumkamata mtu uone utemi wao, kejeli na nguvu watakayotumia. Ni kwamba TZ siku hadi siku raia wanakosa haki zao za kikatiba.
   
 6. W

  Wakwetu Senior Member

  #6
  Mar 12, 2010
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli inasikitisha sana. Mimi sishangai hat kidogo kwani ni kawaida ya polisi. Nimewahi kushuhudia kijana anatoka kwenye ATM kuchukua hela zake then polisi wanaolinda benki hiyo kumfuata na kumnyanganya zilie hela. Uzuri ni kwamba alipiga kelele raia wema wakawashambulia polisi na mawe polisi wakakimbia. OCD wao alipelekewa majina ya wahusika lakini akasema ni uzushi.
  Hivi unadhani hao viongozi wao hawajui? wanajua sana, Wao walitokea huko chini na walikuwa wanafanya hivyo hivyo ila kuna kulindana. Sina imani na jeshi la polisi hata siku moja. inaniuma sana kuona wanafanya vitendo kama hivyo. wao "reasonable force" kwao ni kupiga kwa kadiri unavyoweza.
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,671
  Likes Received: 21,902
  Trophy Points: 280
  Serikali iko kimya kuhusu Polisi kupiga raia au wakati mwingine inatoa majibu ya hovyo hovyo. Jee raia ambao wako wengi dhidi ya Polisi nao wakiamua kupiga Polisi (jambo ambalo linawezekana) Serikali itaendelea kukaa kimya? Nakumbuka Pemba wamewahi kumchinja Polisi kutokana na huu huu ukandamizaji.
  Wakati wa kuchukua hatua kali ni sasa ili kuepusha hayo.
   
 8. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  niko mikononi mwa polisi,
  maisha yangu bado ni mikosi,
  afandeeeeeeee(Mr II a.k.a Sugu)
   
 9. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mbona tunaona one side of the story?
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mwanahaki, nashauri uwasaidie ndugu wa marehemu kufungua kesi ya madai dhidi ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani, mkuu wa jeshi la polisi, mwanasheria wa serikali na polisi wahusika katika mauaji hayo. Hii inawezekana ila watu hawapendi kwenda mahakamani kupata haki zao. Rejea kesi ya kuuwawa kwa kombe mjane alilipwa pesa ya kutosha baada ya kufungua kesi ya madai.
   
 11. K

  Koba JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...way to go,wakianza kufilisika watatia adabu!
   
Loading...