Polisi watangaza kuwaua Panya Road sita Dar e Salaam waliokuwa wanatumia Noah

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Jeshi la Polisi limetangaza kuuawa kwa watuhumiwa sita wa vitendo vya unyan’ganyi wa kutumia silaha za jadi ikiwemo mapanga, visu na nondo ambao ni maarufu kwa jina la Panya Road, eneo la Makongo Area Four, Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema watuhumiwa 9 wakitumia gari aina ya Toyota Noah namba T260 BEP walikamatwa lakini walikaidi na kutishia kuwashambulia askari.

Amesema katika kujihami askari waliwajeruhi watuhumiwa sita ambao walifariki baadaye wakiwa hospitali huku wengine watatu wakitoroka.

Ameongeza kuwa uchunguzi wa awali umebaini baadhi ya watuhumiwa waliofariki miongoni mwao ni viongozi wa Panya Road, wengine waliwahi kufikishwa Mahakamani mara kadhaa na wengine walishiriki katika tukio la Kawe lililosababisha kifo cha mtu mmoja.

Amesema kuwa miongoni mwa waliotambulika ni Salum Juma "Babu Salum" mkazi wa Mbagala anayekadiriwa kuwa na miaka 20-27, mwingine ni Khalifa Khalifa mkazi wa Buguruni ambaye aliwahi kushtakiwa kwa makosa ya kutumia silaha za jadi maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Aidha, amesema wamebaini vinara hao kati ya sita waliopoteza maisha walishiriki katika tukio la Kawe Septemba 14, 2022 na kusababisha kifo.


e44522c7-b992-4395-8bd7-6588eea1ba40.jpg

9b90561e-e3a2-414f-8a97-38297caa085f.jpg
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro J. Muliro ametangaza kuuawa kwa wahalifu sita wanaotumia silaha za jadi Mkoani Dar es Salaam katika eneo la Makongo Area 4.

Taarifa zaidi inafuata...

Wanatekeleza kauli ya Makala RC? Pumbavu kweli hawa Jamaa! Basi tufunge Mahakama zote, please siungi mkono Panya road ila sikubaliani na vitendo vya kuwaua
 
Back
Top Bottom