Polisi wasusiwa maiti Ifakara,kituo cha polisi Mngeta(kata ya Mchombe)

mwalukuni mchanyato

JF-Expert Member
May 15, 2013
404
230
Hivi sasa hali si shwari Mngeta katika kituo cha polisi kata ya Mchombe katika Wilaya ya Kilombero.

Ambapo maiti ya kijana ajulikanaye Kesi inasemekana ameuawa usiku wa kuamkia Leo.

Kisa cha kuisusia polisi maiti ni madai ya wananchi kudai kuwa marehemu alitoa taarifa kituo cha polisi Mchombe katika tarafa ya Mngeta kuwa kuna watu wanataka kumuua, ila baadae inasemekana mtu huyo anayejulikana kwa jina la Kesi.

Hadi mda huu saa kumi hii bado mabomu ya machozi yanarindima kutawanya raia ambao wamefunga Barabara zote zinazoingia polisi kwa magogo.

3bfe6bb26c48db9fd096fbf02a804c18.jpg
 
Poleni sana ndugu zangu naamini atakuwa mndamba huyo aliyeuawa (maana ndio kabila kubwa maeneo hayo)
Ndio hivyo jamani wao huzifanyia kazi intelejensia za mambo ya kisiasa zaidi!

Hivi sasa hali si shwari Mngeta katika kituo cha polisi kata ya Mchombe katika Wilaya ya Kilombero.Ambapo maiti ya kijana ajulikanaye Kesi inasemekana ameuawa usiku wa kuamkia Leo.Kisa cha kuisusia polisi maiti ni madai ya wananchi kudai kuwa marehemu alitoa taarifa kituo cha polisi Mchombe katika tarafa ya Mngeta kuwa kuna watu wanataka kumuua,ila baadae inasemekana mtu huyo anayejulikana kwa jina la Kesi.Hadi mda huu saa kumi hii bado mabomu ya machozi yanarindima kutawanya raia ambao wamefunga Barbara zote zinazoingia polisi kwa magogo.
3bfe6bb26c48db9fd096fbf02a804c18.jpg
 
Poleni wafiwa, ila siku nyingine semeni chadema wanajiandaa kuingia mtaani mtapata ulinzi wa kutosha. R.I.P Kesi.
 
Hali bado si shwari sasa milio ya mabomu ya machozi inaendelea.Huyu ni kijana hivyo vijana na ndugu bado polisi wanajaribu kuwatawanya.
 
Inasikitisha sana polisi kupeleka vifaru kwa wanaokutana mkutanoni na kushindwa kumlinda Kesi,r.i.p Kesi damu yako haitakwenda bure!!
 
Hiyo ni kazi ya vyombo vya usalama na sehemu aliporipoti marehemu kama vile kwa Mwenyekiti wa kijiji.Mm na wewe hatuwezi jua.Ila hilo ni tukio Leo limetokea Mchombe Ifakara.
 
Inasemekana alienda kutaarifu kuwa kuna watu wanataka kumuua.Kumbe jamaa wanamchora tu alipoingia katika kituo cha polisi.Baadae akakutwa ameuawa inasemekana karibu na sio mbali sana na kituoni.Kinachoonekana jamaa walikuwa wanamwinda bado.Sasa raia wakawa wanahoji vipi ajiweke katika mikono salama ya jeshi,halafu baadae akutwe amekufa maeneo ya karibu na kituo?Hapo kijana na ndugu ndio swali lao lilipokuwa inasemekana.
 
Askari wangesikia ukawa wanajiandaa kufanya mkutano ulinz ungekuwa wa uhakika yan mtu haibiwi hata pen ss hapo policccm kaz kwenu
 
Polisi ni jeshi la kuilinda CCM. Hawana la maana watakalokusaidia.
 
Back
Top Bottom