Mh. Pinda unayajua haya? Kuna hatua zimechukuliwa au hadi iundwe tume nyingine kuchunguza?
Inapofikia polisi tunaowatarajia kutulinda wanaua watoto wetu? Tunasuburi kuona waliohusika wakiwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Inapofikia polisi tunaowatarajia kutulinda wanaua watoto wetu? Tunasuburi kuona waliohusika wakiwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Polisi walaumiwa vifo vya wanafunzi Kantalamba
2008-05-04
Na Sammy Kisika PST, Sumbawanga
Wakati maiti ya tatu ya mwanafunzi wa shule ya sekondari Kantalamba ikiopolewa ndani ya mto Lwiche, wananchi mkoani Rukwa wamelitupia lawama jeshi la polisi kwa kudai linahusika kwa kusababisha vifo vya wanafunzi hao.
Mwili wa mwanafunzi wa tatu umepatikana jana nyakati za asubuhi baada ya kuonekana ukiwa unaelea katika mto huo, ambapo ilitolewa taarifa polisi na waokoaji kufika sehemu ya tukio na kuuopoa mwili huo.
Mwanafunzi huyo aliyeopolewa katika mto huo ametambuliwa kuwa ni Joseph Sadala (18), mwanafunzi wa kidato cha pili na mkazi wa Chala wilayani Nkasi mkoani humo.
Hata hivyo mwili wa Joseph, umekutwa tayari ukiwa umeharibika baada ya kukaa kwa mua wa siku tano ndani ya mto huo, ambapo ulitambuliwa na wanafunzi wenzake.
Mazingira ya kupatikana kwa mwili huo ni kama yale ya mwanafunzi aliyeopolewa juzi ambapo Katekista wa Kanisa Katoliki kigango cha Kanatalamba Bw.Cosmas Nchinga aliuona na kuwaarifu walimu wa shule hiyo waliojihimu katika eneo hilo.
Kufuatia kuongezeka kupatikana kwa miili zaidi ya wanafunzi hao, wanaoripotiwa kufa maji, wananchi wa mkoa huo wamelitupia lawama za moja kwa moja kwa jeshi la polisi kwa kile kinachodiwa kuwa walitumia nguvu kubwa katika kudhibiti vurugu za wanafunzi hao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bw.Sebastian Mbilinyi mkazi wa majengo mjini hapa alidai Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) hakikutakiwa kutumia nguvu kubwa kiasi kile kutokana na hali halisi ya tukio lenyewe lilivyokuwa.
Alisema kuwa vurugu za wanafunzi hao, zilitakiwa kudhibitiwa kwa kutumia busara kwanza, kwa kuwataka wanafunzi hao kuondoka kwenye nyumba ya Mkuu wa shule na kurejea bwenini, lakini badala yake hakuna tangazo lolote lililotolewa isipokuwa FFU walivamia eneo hilo na kuanza kupiga mabomu ya machozi.
``Unajua sisi Watanzania wengine, katika umri huu mkubwa hatujawahi kusikia mlio wa bunduki, sasa inakuwaje kwa hawa vijana ambao wengi wao wametoka mazingira ya vijijini wanaposikia miio ya bunduki mfululizo na ikiwa ni usiku lazima wakimbie hovyo na matokeo yake ndio kama haya ya kutumbukia mtoni`` alisema Mbilinyi.
SOURCE: Nipashe