Polisi wapigwa kama wezi, wanusurika kuchomwa moto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wapigwa kama wezi, wanusurika kuchomwa moto!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, Jul 14, 2009.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Taarifa za hivi punde kutoka Bukoba ni kuwa polisi wawili waliokuwa na tabia ya kuzizia wananchi na kuwatoa rushwa wamevamiwa na wananchi kisha kupigwa mithiri ya vibaka kabla ya kuokolewa na wenzao katika harakati za mwisho mwisho za kuwaunguza kwa moto.

  Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Bukabuye wilayani Missenyi ambapo polisi hao kutoka kituo kikuuu cha polisi mjini Bukoba walikodi teksi kwa lengo la kwenda kuvizia wanaovusha kahawa ya magendo kwenda Uganda ili kuwatoa rushwa na kuwa hii ni tabia yao ya kila siku.

  Kutokana na vitendo vyao wananchi walijikusanya wakazuia gari hilo kisha kuanza kuwapatia kipigo, kuvunjavunja gari kabla ya kukolewa na polisi wa kituo cha Kanyigo huko Missenyi.

  Hivi sasa polisi mmoja amekimbia hajulikani alipo, ingawa wawili wapo hoi katika hospitali ya mkoa KAGERA.

  Polisi wanafanya jitihada za kufanya gwaride ili wananchi wawatambue wengine ambao hawajajulikana.

  Ni hayo .
   
 2. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Society is sick and tired. Wamechoka sasa. watambue hilo.
   
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,796
  Likes Received: 2,461
  Trophy Points: 280
  hII NZURI KUSIKIA NA BADO KWA HAWA POLICE WA BARABARANI NAO WANAHITAJI KIPIGO KAMA HICHI.KWANI WANAPENDA KUPANDIKIZA MAKOSA KWENYE MAGARI YA WATU KISA WAPATE HELA KWA KWWELI INABIDI IFIKE SEHEMU TUWE TUNAADHIBU KILA KUKICHA.
  ASANTE KWA TAARIFA ILIYOVUNJINVUJIKA.
   
 4. b

  bnhai JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Sorry siungi mkono kujichukulia sheria mkononi. Wananchi wafuate taratibu
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  bnhai,

  Taratibu wamezifuata tangia 1961 bila mafanikio, kwa hiyo sasa "enafu is enafu"! Kama walirushia mawe msafara wa mukulu sembuse polisi wawili tena wala rushwa, ebo!
   
 6. U

  Ulusungu Member

  #6
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba tafsiri ya kujichukulia sheria mkononi,Sababu mtenda kosa anafanya kinyume na sheria, akitendewa kinyume na sheria inaibuka hoja ya kujichukulia sheria mkononi. Kwangu kichina naomba msaada nieleweshwe...
   
 7. U

  Ulusungu Member

  #7
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado hata wahalifu wakikamatwa kwenye tukio 'INNOCENT TILL PROVEN GUILTY' Justice itakuja tengamaa mpaka pale kuna wale ambao sheria itawaona kama ni 'GUILTY TILL PROVEN INNOCENT' Ingawa nafikiri kwa kiasi fulani trafic offence madereva ni Guilty till proven innocent,kwani haijarishi mazingira ya mtu kugongwa na gari derva anakuwa charged.
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  haya mambo yameachwa kwa kipindi kirefu wananchi kujichukulia sheria hakuna utawala wa sheria hata kidogo
  kuna mtu anatoa takataka ndani ya nyumba yake anapeleka katikati ya barabara inapojengwa
  mwingine anakata bomba anaacha maji yanatiririka
  Mwingine anafungulia maji ya ****** na kuyaelekezza barabarani
  mwingine anayanganya mke/mume wa mtu
  mwingine anajenga katika kiwanja cha shule
  mwingine anatiririsha sumu kwenye mto
  mwingine hanunui pikipiki hata moja huku akila fedha zote kwa bei ya bilioni 36
  mwingine anabaka mtoto wa shule au bi kizee
  mwingine anawagawia matajiri,wazungu wahindi waarabu viwanja vya starehe
  mwingine anaumuua kibaka
  mwingine anambaka mfungwa mwenzake
  mwingine anamuua albino/bi kizee
  mwingine anauza mbuga na wanyama
  mwingine anaanzisha gazeti ,redio tv yake ya kumsifu toka saa moja asubuhi mpaka kesho
  mwingine anamsemea raisi na kugeuza Ikulu nyumba ya mamake
  mwingine anampiga traficki akiongoza magari
  mwingine anayanqanya masanduku ya kura au anabadilisha matokeo
  uliona wapi wananchi wanapopotoa msafara wa Raisi
  hakuna utawala kabisa,hali imeachwa hovyo hovyo hovyo hakuna utawala kabisa mambo mengi maovu ule msemo wa Tanzanians are humble people umeondolewa na utawala wa JK
  Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Africa
  Mtaona busara za polisi wataua au kuumiza kama wanachi 200 hivi waliokuwemo na wasio kuwemo na wataita operesheni safisha na hapo ndipo watakapozidisha hasira za wananchi panahitajika busara saana kushughulikia swala hili,tuliwaambia polisi alfu 40,000 hawawezi kupambabana na watanzania milioni arobaini serikali ikaze buti irejeshe ni dhami kati ya wananchi na watendaji wake vinginevyo watuchunwa ngozi huko tuendako,huwezi kupmbana na mtumwenye njaa hasira zake mbaya sana
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Taratibu zipi Tanzania??? Tanzania haina taratibu wala ethics, vinginevyo usingekuta kuna majority unrest kiasi hiki. Naona kichapo hicho kiendeleee hadi kwa maaffa ardhi, polisi wala rushwa (99.9%), mafisadi wote, migodini ambako watu wameibiwa ardhi yao kwa fidia ya kilio, ambao kemikali zinaua watu na nyingine ni silent killer but taratibu zimechukuliwa weeeeee na jibu hakuna. Kwa nini mkoa wa Marwa wanauna?? kwa nini zitakuwa kibao!!!! Yote ni kwa kuwa taratibu zinakiukwa hasa na wenye mamlaka na wananchi wamechoka. Sasa basi kama kweli wamechoka nataka wafanye a change uchaguzi wa 2010!!!!! Tatizo sijui nani kiongozi wa sasa wa upinzani anafaa kuwa Rais, vinginevyo kiongozi safi wa SSM (if at all exists) ajiunge upinzani apatiwe kura. Nani yuko tayari??? Nyoosha mkono!!!!!!! Walahi mimi baba yaki mpendwa SSM sitaukata!!!!
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Tuambie hizo taratibu za kufuatwa na hao wananchi
   
 11. b

  bnhai JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kuna kauli moja Amnesty International huwa wanaitumia mara kwa mara. Mpenda haki yoyote hawezi kumuadhibu mtu bila kumpa uhuru wa kuhukumiwa na vyombo vilivyoweka na katiba. Na pia mpenda haki yoyote hudhihirisha namna anavyoheshim haki za binadam pale anapokosewa yeye na hatua ambazo huzichukua. Siungi mkono suala la unyanyaswaji wananchi na pia siungi mkono askari kutoa rushwa. Vipo vyombo vya kushughulikia malalamiko. Tufuate taratibu
   
 12. b

  bnhai JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Zipo namna za kuaddress grievances zetu na si kwa kupoteza maisha ya watu. Wapeni elimu ya Uraia, kila mtu aelimishe jamaa zake taratibu tutafika tunapopahitaji. Tusiipoteze amani ambaye tumekuwa tukiilinda kwa muda mrefu. Tuziadabishe mamlaka uhusika kwa taratibu zilizoweka si kupopoana na mawe
   
 13. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haya ni matokeo ya ukiukaji wa maadili ya kazi kwa Jeshi letu la Polisi.Wasipojirekebisha mengi yataendelea kutokea.
   
 14. K

  Kitoto Akisa Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imesemwa kuwa ukiona ovu mbele yako liondoe kwa mikono yako, na kama huwezi basi likemee kwa nguvu zako zote na la ukishindwa basi sikitika moyoni, lakini kusikitika ni dalili ya udhaifu. Hureee wananchi wa Bukoba mmeonesha mfano wa kuondoa uovu kwa mikono yenu na sio kusikitika, maana mmesha kimea sana tu lakini wapi
   
 15. b

  bnhai JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Pia inasemwa kwamba kusamehe ni bora zaidi au pia mnausiwa muwe ni wenye kusubiri
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  The epitomy of chaos.

  1. Serikali haina mifumo mizuri ya masoko inayohakikisha wananchi wanaweza kulipwa vizuri baada ya kuuza mazao yao, a recipe for chaos.

  2.Wananchi wanaona hakuna mifumo mizuri ya kuuza mazao yao, hivyo wananvunja sheria kwa kutumia njia za magendo, a recipe for chaos.

  3. Polisi, ambao ni sehemu ya ukiritimba wa kiserikali unaosababisha wananchi wakose kuweza kuuza mazao yao kwa uhuru, wanaongezea machungu kwa wananchi kwa kutaka kuwatoza rushwa, a recipe for chaos.

  4.Wananchi kwa kukerwa na "uonevu" wa serikali na wafanyakazi wayo, wanaamua kuchukua hatua mikononi mwao na kuwaadibisha askari hawa, chaos.

  Jinsi ninavyoiona hali hivi sasa mambo yanajichanganya polepole, tutafika sehemu ambapo tutashindwa kurudi nyuma na matokeo yake yatakuwa mabaya sana, narudia mabaya sana.
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Huo si utawala wa sheria.

  Siungi mkono
   
 18. N

  Nanu JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ni mara nyingine polisi wakipigwa na wananchi kwa kusizingiziwa ni wezi. Mwezi uliopita, wengine wawili walichapwa Kibamba Dar Es Salaam baada ya kuwazuia wachimba mchanga mtoni. Nao waliawaita wezi watu wakawafamia nusura wangeuawa. Lakini tabia hii si nzuri, kuna watu wengine wazuri wa tabia walishahukumiwa kama wezi na wananchi kwa kuwachoma moto. Driver taxi mmoja aliuawa miezi iliyopita baada ya kumdai abiria wake amlipe nauli, yule abiria aliingia ndani na kutoka nje akipiga kelele mwizi, watu wakamvamia driver wakamuua na kuchoma gari. Inabidi tuangalie hili kwa makini. Wakati mwingine vaa sura kuwa wewe ndiyo mtu amekuitia mwizi halafu watu bila kujiuliza wakaanza kukutwanga, hii inatokea. Lazima tabia hii idhibitiwe and vyombo vinavyo husika.
   
 19. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160

  Utawala upi wa sheria unaunga mkono? sheria za Qatar au Tanzania? Let us be honest bana.

  Hiyo sehemu lilipotokea "tifu" naifahamu sana, ni maeneo ya karibu sana na kijiji nilichozaliwa! Polisi ni wanyanyasaji sana maeneo hayo, wao ndio wanaowakamata watuhumiwa na wao ndio wanatoa hukumu! kule hakuna utawala wa sheria (rudia sentensi niliyopigia mstari mara nne).

  wenyeji wa kule wana msemo wao kuwa "kukola ebya balimbonaa" (tafsiri: kutenda jambo with impunity). Haya maeneo ya stori za unyanyasaji wa Polisi tangia early 80's wakati tuna-cross Uganda border kwenda kununua mafuta ya taa, sabuni, chumvi, sukari, e,t,c (hizi bidhaa hazikupatikana Tanzania miaka hiyo).

  Wakati huo kulikuwa na PC kwenye "border post" mmoja akiitwa Haruna (RIP) alikuwa anaabudiwa sana na alikuwa mnyanyasaji sana (of course na genge lake la mapolisi), walikuwa juu ya sheria hawa of which hii trend imeedelea mpaka leo! Hii ni jamii iliyoukuwa imetoka kwenye vita then na bado ikaendelea kuwa insecure baada ya vita, na imeedelea hivyo miaka 31 baadaye!

  What exactly do you expect? Bin-adamu akinyanyaswa sana lazima ata-revolt, hivyo ndivyo ilivyo! Haya matukio polepole yata-cover nchi nzima na trust me and God, that is when Tanzania will realize the "change we believe in"

  Musibe ge (have a good afternoon).
   
 20. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ebu hacha nidhamu za woga, unaona vitendo vinavyo fanywa na hawa polisi ni vizuri kweli, BIG UP Kagera, huku Dar tuko pamoja nanyi.
   
Loading...