Polisi wapekua tena nyumba ya Lwakatare

Kwa wale magwiji wa sheria za Tanzania, Naomba nisaidiwe,

Kwa sheria ya Tanzania, how many maximum days suspect anatakiwa kuwa mahabusu kabla ya kuwa charged or released.

mkuu naamini wewe uko kwenye system pia, kwa tanzania hakuna linaloshindikana kuna jaama namfahamu aliwahi kukaa miezi 15 bila kufikishwa mahakamani na baada ya hapo akaachiwa huru....
 
Polisi wambana Lwakatare

Bakari Kiango na Nuzulack Dausen, Mwananchi

Polisi wamezidi kumbana Mkuu wa Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare baada ya kupekua nyumbani kwake kwa siku ya pili mfululizo.

Lwakatare, ambaye ni mbunge wa zamani wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF, alikamatwa juzi mchana kwa kutuhumiwa kwa kufanya uchochezi wa uvunjifu wa amani baada ya kunaswa kwenye picha ya video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii

Upekuzi wa pili
Nyaronyo Kicheere, ambaye ni Mwanasheria wa Lwakatare, aliliambia gazeti hili jana kuwa mteja wake, ambaye anashikiliwa na polisi hao, alipelekwa nyumbani kwake Kimara-King’ong’o jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upekuzi huo.

Ilikuwa mara ya pili kwa Lwakatare kupekuliwa kwani mara ya kwanza ilikuwa juzi jioni baada ya kuhojiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Lwakatare, ambaye alitolewa Kituo cha Kati cha Polisi, alipelekwa jana kwa msafara wa magari mawili ya polisi chini ya ulinzi mkali.

Nyaronyo alisema kuwa msafara huo uliondoka saa 10.00 jioni kwa ajili ya safari hiyo ya Kimara wakitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam kilipo Kituo cha Kati cha Polisi. Alisema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao kizito kati ya maofisa wa Idara ya Upelelezi (DCI) na wale wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

“Hawa watu walikuwa na kikao kirefu siku nzima ya leo (jana) nadhani walikuwa wanaangalia kama kuna uwezekano wa kumshtaki au la mteja wangu.Walipomaliza kikao waliamua turudi tena nyumbani kwa Lwakatare ili kuendelea na upekuzi,” alieleza Kicheere.

Kama ilivyokuwa juzi, upekuzi kwa Lwakatare uliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Obadia Jonas.

Polisi wanasemaje
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa bado wanaendelea kumshikilia Lwakatare huku wakiendelea na uchunguzi wa suala hilo. “Kama kukiwa na taarifa za ziada nitawajulisha msiwe na wasiwasi,” alisema Senso na kukata simu.

Lwakatare alikamatwa juzi saa saba mchana katika makao makuu ya chama hicho na kupelekwa katika Makao Makuu ya Polisi kwa mahojiano.

Juzi siku nzima mitandao ya kijamii ilikuwa imetawala na habari picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky kwa madai kuwa anashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, kutengeneza migogoro.

Pia, Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu , ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.

Chadema wapinga
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema mkanda wa video unaoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii ukimwonyesha Lwakatare akipanga njama za uhalifu hauna uhalisia na kwamba huo ni uzushi ulioratibiwa na kufanikishwa na vyombo vya dola.

Pia Dk Slaa alidai kuna mpango mwingine kabambe unaofanywa na idara za dola kuhakikisha kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anakamatwa kutokana na sumu anazotema bungeni na kwingineko dhidi ya Serikali.

Dk Slaa alisema kuwa taarifa za kuwapo njama za kukichafua chama chake kupitia mkanda huo wa video alizipata kutoka ndani ya Serikali Jumatatu iliyopita hata hivyo, wakati akiendelea kupanga mkakati wa kushughulikia tayari ulikuwa umeshaingizwa katika mitandao
ilishidikanaje kupekuliwa mtu aliyesema kwamba anayo CD ya wauaji kupekuliwa? kwa kuwa hizo za kumkamata Lwakatare zinaonekana njama, ukitoka huko atakuwa na sifa ya Mandela
 
mkuu naamini wewe uko kwenye system pia, kwa tanzania hakuna linaloshindikana kuna jaama namfahamu aliwahi kukaa miezi 15 bila kufikishwa mahakamani na baada ya hapo akaachiwa huru....

Thanks kwa kunidokeza hilo. I'm very sorry for him.

Hata hivyo alipaswa arudi mahakamani kudai haki yake (compensation)
 
Kwa wale magwiji wa sheria za Tanzania, Naomba nisaidiwe,

Kwa sheria ya Tanzania, how many maximum days suspect anatakiwa kuwa mahabusu kabla ya kuwa charged or released.
masaa ya kushikiliwa yakiisha ana achiwa then akitoka hatua mija tu anakamatwa tena... kaka hujui hilo????
 
Sasa hivi hamna tena utawala wa sheria,
ubabe umetawala.Ila ukiona hivyo,mwanzo wa haki unakaribia,kwani wao wamemueka shetani mbele,sisi tumemtanguliza MUNGU.
 
Kwa wale magwiji wa sheria za Tanzania, Naomba nisaidiwe,

Kwa sheria ya Tanzania, how many maximum days suspect anatakiwa kuwa mahabusu kabla ya kuwa charged or released.
Within 24 hours tangu ukamatwe unatakiwa ufikishwe mahakamani ili usomewe shitaka linalokukabili,.
 
Leo yamerud kwa Lwakatare,wadau eanalalama kwa polis,ila ikiwa kwa wavaa kofia na kanzu,pongez kibao kwa polis,,,,sitaacha kuwazodoa wanafki
 
Kwa jinsi polisi walivyo na uweledi wao unavyotia shaka, sitashangaa wakiumbuka kama walivyoumbuka kwa yule mwandishi wa tbc. Wampeleke mahakamani
 
Sasa hivi hamna tena utawala wa sheria,
ubabe umetawala.Ila ukiona hivyo,mwanzo wa haki unakaribia,kwani wao wamemueka shetani mbele,sisi tumemtanguliza MUNGU.

kwakua kakamatwa Lwakatare umegundua hakuna utawala wa sheria,,,,,hehehee,,,polis hao mlokua mnawasifia kwa upuuzi wao miskitin wanang'ata huku na huku
 
kwanza unamkamataje mtu wakati huna evidence ya kutosha? pia kuna nini cha kupekua ambacho hakikuonekana mara ya kwanza?! hii ipo Tanzania tu inaitwa Tz zaidi ya uijuavyo! video yenyewe ambayo inatumika kama kidhibiti hovyoooooooo!!!!
 
Polisi wambana Lwakatare

Bakari Kiango na Nuzulack Dausen, Mwananchi

Polisi wamezidi kumbana Mkuu wa Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare baada ya kupekua nyumbani kwake kwa siku ya pili mfululizo.

Lwakatare, ambaye ni mbunge wa zamani wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF, alikamatwa juzi mchana kwa kutuhumiwa kwa kufanya uchochezi wa uvunjifu wa amani baada ya kunaswa kwenye picha ya video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii

Upekuzi wa pili
Nyaronyo Kicheere, ambaye ni Mwanasheria wa Lwakatare, aliliambia gazeti hili jana kuwa mteja wake, ambaye anashikiliwa na polisi hao, alipelekwa nyumbani kwake Kimara-King’ong’o jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upekuzi huo.

Ilikuwa mara ya pili kwa Lwakatare kupekuliwa kwani mara ya kwanza ilikuwa juzi jioni baada ya kuhojiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Lwakatare, ambaye alitolewa Kituo cha Kati cha Polisi, alipelekwa jana kwa msafara wa magari mawili ya polisi chini ya ulinzi mkali.

Nyaronyo alisema kuwa msafara huo uliondoka saa 10.00 jioni kwa ajili ya safari hiyo ya Kimara wakitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam kilipo Kituo cha Kati cha Polisi. Alisema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao kizito kati ya maofisa wa Idara ya Upelelezi (DCI) na wale wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

“Hawa watu walikuwa na kikao kirefu siku nzima ya leo (jana) nadhani walikuwa wanaangalia kama kuna uwezekano wa kumshtaki au la mteja wangu.Walipomaliza kikao waliamua turudi tena nyumbani kwa Lwakatare ili kuendelea na upekuzi,” alieleza Kicheere.

Kama ilivyokuwa juzi, upekuzi kwa Lwakatare uliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Obadia Jonas.

Polisi wanasemaje
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa bado wanaendelea kumshikilia Lwakatare huku wakiendelea na uchunguzi wa suala hilo. “Kama kukiwa na taarifa za ziada nitawajulisha msiwe na wasiwasi,” alisema Senso na kukata simu.

Lwakatare alikamatwa juzi saa saba mchana katika makao makuu ya chama hicho na kupelekwa katika Makao Makuu ya Polisi kwa mahojiano.

Juzi siku nzima mitandao ya kijamii ilikuwa imetawala na habari picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky kwa madai kuwa anashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, kutengeneza migogoro.

Pia, Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu , ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.

Chadema wapinga
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema mkanda wa video unaoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii ukimwonyesha Lwakatare akipanga njama za uhalifu hauna uhalisia na kwamba huo ni uzushi ulioratibiwa na kufanikishwa na vyombo vya dola.

Pia Dk Slaa alidai kuna mpango mwingine kabambe unaofanywa na idara za dola kuhakikisha kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anakamatwa kutokana na sumu anazotema bungeni na kwingineko dhidi ya Serikali.

Dk Slaa alisema kuwa taarifa za kuwapo njama za kukichafua chama chake kupitia mkanda huo wa video alizipata kutoka ndani ya Serikali Jumatatu iliyopita hata hivyo, wakati akiendelea kupanga mkakati wa kushughulikia tayari ulikuwa umeshaingizwa katika mitandao

Ni imani ya watanzania kuwa sasa ukweli utajulikana, tuwape muda Polisi ili wafanye kazi yao vizuri.
 
polisi wanao mhoji rwakatale na kumpekua nyumbani kwake wanaujua ukweli uko wapi, lakini kwakua wanafanya kazi ya mheshmiwa hawawezi sema daima hata wao wanatetea kazi na uhai wao. Lakini sishangai kwa kuona 99% ya wachangiaji kwenye majamvi mengi wanaiponda hiyo video na kubaini ukweli hii inamanisha hatudanganyiki.
 
Said Mwema ameharibu sana Jeshi la Polisi. Wengi walidhani Mahita alikuwa na madhaifu, lakini uongozi wa Mwema utabakia doa katika historia ya Jeshi la Polisi, na sioni ni kwa vipi tunaweza kuwa na Jeshi lenye uadilifu bila ya kulivunjilia mbali hili la sasa na kusuka kila kitu upya!

Hii ya kukamatwa kwa Lwakatare, watu wasingekuwa na shida kama historia ya utendaji wa polisi wetu ingekuwa nzuri. Lakini tumeona jinsi mambo yamekwenda hovyo, polisi wanauza madawa ya kulevya (na kupeleka ushahidi wa sukari), polisi wanafanya magendo mipakani, polisi wanateka raia na kuwatesa, polisi wanabambikia watu kesi, hivi kweli hapo tuna polisi au genge la Mafia?

Na yanayopokuja mambo ya msingi polisi wanabaki kimya hata pale ambapo ushahidi uko wazi. Iweje hadi leo polisi haisema la maana kuhusu kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka, licha ya victim kutaja watuhumiwa? Kwanini watu waamini kuwa polisi hawahusiki na uuandaji wa hii video given perfomance yao? Zanzibar wameshindwa kazi kabisa imebidi waombe FBI!

Mwema ulianza na matumaini, lakini utaacha genge la Mafia, na sote kama Taifa tutapata shida sana hadi hapo tutakapokuwa na jeshil la polisi. Unaacha Polisi kama adui mkubwa wa jamii. Very sad!
 
Polisi wa Tz bana, sasa walienda kupekua tena nini? Wajue tu sasa ndio muda muafaka watoe details za hayo mahojiano, tuone kama sio dili lao na akina Riziwani
 
Back
Top Bottom