Polisi wapekua tena nyumba ya Lwakatare | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wapekua tena nyumba ya Lwakatare

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima, Mar 15, 2013.

 1. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Polisi wambana Lwakatare

  Bakari Kiango na Nuzulack Dausen, Mwananchi

  Polisi wamezidi kumbana Mkuu wa Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare baada ya kupekua nyumbani kwake kwa siku ya pili mfululizo.

  Lwakatare, ambaye ni mbunge wa zamani wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF, alikamatwa juzi mchana kwa kutuhumiwa kwa kufanya uchochezi wa uvunjifu wa amani baada ya kunaswa kwenye picha ya video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii

  Upekuzi wa pili
  Nyaronyo Kicheere, ambaye ni Mwanasheria wa Lwakatare, aliliambia gazeti hili jana kuwa mteja wake, ambaye anashikiliwa na polisi hao, alipelekwa nyumbani kwake Kimara-King’ong’o jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upekuzi huo.

  Ilikuwa mara ya pili kwa Lwakatare kupekuliwa kwani mara ya kwanza ilikuwa juzi jioni baada ya kuhojiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Lwakatare, ambaye alitolewa Kituo cha Kati cha Polisi, alipelekwa jana kwa msafara wa magari mawili ya polisi chini ya ulinzi mkali.

  Nyaronyo alisema kuwa msafara huo uliondoka saa 10.00 jioni kwa ajili ya safari hiyo ya Kimara wakitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam kilipo Kituo cha Kati cha Polisi. Alisema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao kizito kati ya maofisa wa Idara ya Upelelezi (DCI) na wale wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

  “Hawa watu walikuwa na kikao kirefu siku nzima ya leo (jana) nadhani walikuwa wanaangalia kama kuna uwezekano wa kumshtaki au la mteja wangu.Walipomaliza kikao waliamua turudi tena nyumbani kwa Lwakatare ili kuendelea na upekuzi,” alieleza Kicheere.

  Kama ilivyokuwa juzi, upekuzi kwa Lwakatare uliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Obadia Jonas.

  Polisi wanasemaje
  Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa bado wanaendelea kumshikilia Lwakatare huku wakiendelea na uchunguzi wa suala hilo. “Kama kukiwa na taarifa za ziada nitawajulisha msiwe na wasiwasi,” alisema Senso na kukata simu.

  Lwakatare alikamatwa juzi saa saba mchana katika makao makuu ya chama hicho na kupelekwa katika Makao Makuu ya Polisi kwa mahojiano.

  Juzi siku nzima mitandao ya kijamii ilikuwa imetawala na habari picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky kwa madai kuwa anashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, kutengeneza migogoro.

  Pia, Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu , ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.

  Chadema wapinga
  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema mkanda wa video unaoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii ukimwonyesha Lwakatare akipanga njama za uhalifu hauna uhalisia na kwamba huo ni uzushi ulioratibiwa na kufanikishwa na vyombo vya dola.

  Pia Dk Slaa alidai kuna mpango mwingine kabambe unaofanywa na idara za dola kuhakikisha kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anakamatwa kutokana na sumu anazotema bungeni na kwingineko dhidi ya Serikali.

  Dk Slaa alisema kuwa taarifa za kuwapo njama za kukichafua chama chake kupitia mkanda huo wa video alizipata kutoka ndani ya Serikali Jumatatu iliyopita hata hivyo, wakati akiendelea kupanga mkakati wa kushughulikia tayari ulikuwa umeshaingizwa katika mitandao
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2013
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,556
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  hawakawi ku plant kitu hapo, halafu watapata pa kutokea
   
 3. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu hajalala usingizi na huwa halali kabisa, itafahamika tu
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2013
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,373
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tatizo kubwa la nchi ni jeshi la polisi kuongozwa na wanasiasa badala ya watu wenye professional zao, kitu cha kwanza kabisa ambacho polisi ilitakiwa kukifanya ni kufanya uchunguzi makini wa authenticity ya hiyo clip ili wajue uhalali wake na kwanini ilipelekwa kwenye mtandao badala ya Polisi ili wasiingize ktk mtengo wa siasa kama walivyoukwepa ule mtego wa mwigulu kutangaza kuwa ana mkanda wa chadema kupanga mauaji au cdm imeleta majasusi kutoka afghanistan ile ilikuwa ni siasa tu na polisi wailiona hilo nashangaa hii wauingie mtego wa wanasiasa kichwa kichwa badala ya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili yao wanasikiliza amri ya NCHIMBI nao wanafuata. moja kati ya maoni yangu ndani ya katiba mpya ilikuwa ni kutenganisha kabisa jeshi a polisi na jeshi na wanasiasa.
   
 5. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2013
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 942
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hawa police wetu hawakawii kuingiza vitu vyao nyumbani kwake na kumpambikia ushahidi wakupandikiza kwanini wasipekue vizuri siku ya kwanza wamekosa ushahidi wa kumshitaki wanang'ang'aniza.
   
 6. MJENGA

  MJENGA JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2013
  Joined: Nov 18, 2012
  Messages: 620
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 80
  Hizo zote ni porojo za kujinasua tu. Mara teknolojia mara video shop. Mtahara mno this time mmenaswa na mambo yenu ya hovyo.
   
 7. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #7
  Mar 15, 2013
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  Kwa wale magwiji wa sheria za Tanzania, Naomba nisaidiwe,

  Kwa sheria ya Tanzania, how many maximum days suspect anatakiwa kuwa mahabusu kabla ya kuwa charged or released.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2013
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,303
  Likes Received: 2,200
  Trophy Points: 280
  Nikweli kabisa mambo Yao ya ovyo Kama EPA Richmond Meremeta Gas Mtwara Hali mbaya mahospitalini na wanafunzi wa form four kufail haya yote yamesababishwa na Rwekatare na Chadema
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2013
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,303
  Likes Received: 2,200
  Trophy Points: 280
  Nenda kwa magamba wenzio ambao wapo juu ya sheria ndio wenye majibu
   
 10. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2013
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,102
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ipo siku watz wenye akili timamu wataongea tu... police na idara ya upelelezi ni watu ambao tunaishi nao mitaani ila wao wanajiona mihungu watu.... poa tu maCCM.
   
 11. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,491
  Likes Received: 2,974
  Trophy Points: 280
  Tanzania....tutaendelea kunyanyasika kwa kuwa nchi yetu tuwekabidhi madhalimu
   
 12. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #12
  Mar 15, 2013
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  Sikujua kama kisima chako cha akili kina kina kifupi namna hii. kumbe sihitaji hata kuchota hekima na busara kwa sababu imejaa matope tupu.
   
 13. makavulaivu

  makavulaivu JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2013
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  SiPolisi wa TZ ambao ni influenced na politicians, sidhani kama wataacha kutupia viushahidi vya kumtia hatiani zaidi hapo nyumbani kwake.Malengo sio Lwakatare, Lengo ni kuchafua na kuishusha CDM kupitia hii skendo.
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2013
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,587
  Likes Received: 817
  Trophy Points: 280
  Na mimi nina wasiwasi, wanaweza plant evidence wao. Je wanasachiwa na wakili kabla ya kuingia? I hope nyumba ina ulinzi wa kutosha; maana wanaweza zika kitu hata kwenye compound. CDM isaidie kuongeza ulinzi!
   
 15. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,883
  Likes Received: 2,705
  Trophy Points: 280
  Polisi chonde chonde msisahau na kumpeleka mirembe hospitali kumpima akili yake.
   
 16. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2013
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Polisi huyu mtu akirudi mtaani na Shehe Ponda atokee hatutaki sheria ichukuliwe kwa mtu mmoja tu.Halafu ni mchafu anaingiza vidole puani na kujifuta kwenye t shirt yake aghhh
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2013
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,303
  Likes Received: 2,200
  Trophy Points: 280
  Hivi kile kilichokuwa chuo cha Tanesco hapo morogoro siku hizi kimekuwa Tawi la Mirembe?
   
 18. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2013
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,987
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  24 hours
   
 19. Kertel

  Kertel JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2013
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 2,585
  Likes Received: 687
  Trophy Points: 280
  Ushatukanwa
   
 20. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #20
  Mar 15, 2013
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  Thank you very much.
   
Loading...