Polisi waomba kibali kumkamta Mbunge wa CCM kwa nguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waomba kibali kumkamta Mbunge wa CCM kwa nguvu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jun 29, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Polisi kumkamta Mbunge kwa nguvu
  Na Cosmas Mlekani
  29th June 2011  Jeshi la Polisi mkoani Mwanza huenda likamkamata Mbunge wa Busega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Titus Kamani, ili kumhoji kuhusiana na tuhuma za kutaka kumuua aliyekuwa Mbunge jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni.

  Tayari Jeshi hilo limekwisha kumwandikia barua Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashillilah, kumtaka mbunge huyo kwenda Mwanza kuhojiwa kuhusiana tuhuma hizo zinazomkabili.

  Jeshi hilo limesema kuwa endapo Dk. Kamani ataendelea kukaidi amri ya polisi ya kwenda jijini Mwanza kutoa maelezo, linaweza kutumia nguvu kumkamata kwa mujibu wa sheria.

  Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Mwanza (RCO), Deusdedith Nsimeki, alisema juzi jijini hapa kuwa mtuhumiwa huyo bado hajafika polisi kutoa maelezo yake dhidi ya tuhuma zinazomkabili licha ya polisi kumtaka kufanya hivyo.

  Inadaiwa kuwa Mei 31, mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza liliiandikia barua katika Ofisi ya Bunge kumtaka Dk. Kamani kwenda Mwanza kwa ajili ya mahojiano maalumu na jeshi hilo dhidi ya tuhuma hizo.

  Nsimeki alithibitisha kuwa hadi sasa Dk. Kamani hajafika Mwanza kutoa maelezo kwa Jeshi la Polisi.

  Alisema kuwa ikiwa mbunge huyo ataendelea kukaidi amri hiyo halali, wataomba kibali kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), ili watumie nguvu kumkamata.

  Jeshi hilo liliandika barua Mei 31, mwaka huu, yenye Kumbukumbu No. MZR/CID/SCR/105/2011/4 iliyotumwa kwa Katibu wa Bunge ikimkata kumruhusu Dk. Kamani kwenda Mwanza kutoa maelezo polisi katika Jalada No. MW/IR/2607/2011-MR-CC.28/2011 lililofunguliwa kwa kosa la kula njama na kutaka kumuua Dk. Chegeni.

  Watuhumiwa wanne tayari wamekwisha kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kujibu tuhuma hizo.

  Waliofikishwa mahakamani na sasa wako nje kwa dhamana ni Dismas Zacharia Ndaki, Erasto Kazimili Kombe, Queen Joseph Bogohe na Ellen Joseph Bogohe.

  Kesi yao imepangwa kutajwa Julai 6, mwaka huu.

  Dk. Chegeni aliangushwa katika kura za maoni na Dk. Kamani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

  NIPASHE ilipowasiliana na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, jana jioni, kuhusiana na suala hilo, alisema kuwa wanachofahamu ni kuwa Dk. Kamani alikuwa Mwanza na kuongeza kuwa kama hajafika Polisi ni kitu kingine.

  "Sisi hatupendi masuala kama haya yawasumbue wabunge, lakini la kwake (Dk. Kamani) ni gumu kuliingilia," alisema Joel.

  Alipoulizwa kama ofisi ya Bunge ilipokea barua kutoka Polisi ikitaka Dk. Kamani kwenda kuhojiwa Mwanza, Joel alisema hana uhakika kwa kuwa wakati huo hakuwepo katika ofisi hiyo na kusisitiza kuwa anachokifahamu ni kuwa mbunge huyo hivi karibuni alikuwa Mwanza.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ivi ndo utaratibu wa kukamata wabunge sio!? Mbona ni wa sisiem to wanaombewa kibali bana?
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mbona Mbowe kwa kola lile na aina ya kesi pressure ilikuwa kubwa mno lakini kwa huyu tuhuma kubwa kabisa bado kibali kinatakiwa ?Mhn haya Tanzania yangu
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Waombe na ndege ya kijeshi pia !
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Kibali cha nini......si wafanya KAMA KAWA KAMA DAWA YAO...??? Wale wa upinzani waliokwisha kamatwa waliombewa vibali........???
   
 6. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hizi double standards kwenye hii nchi ikob siku zitaisha tu,akwa wa ccm polisi wanaomba kibali upinzani piga,garagaza,polisi mnajiandalia matatizo makubwa sana
   
 7. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Kuna haki
  pia kuna haki ZAIDI
   
 8. L

  Lua JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kibali kwani wanataka kuwinda?
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  sahani na vijiko vimeanza kugongana halafu mnasema amani iko wapi?
   
Loading...