Polisi wanne mbaroni kwa mauaji ya raia Songea:IGP MWEMA APELEKA KIKOSI CHA UCHUNGUZI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wanne mbaroni kwa mauaji ya raia Songea:IGP MWEMA APELEKA KIKOSI CHA UCHUNGUZI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Feb 24, 2012.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Polisi Mkoani Ruvuma, wanawashikilia na kuwahoji askari wake wanne kwa tuhuma za mauaji ya raia kwa kutumia risasi za moto katika vurugu zilizotokea juzi mjini Songea.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda alisema jana kuwa askari hao walikamatwa na wanaendelea kuhojiwa ili kujua kama kulikuwa na uzembe katika utekelezaji wa majukumu yao."Kwa kuwa tukio hilo limehusisha vifo, hatuwezi kuacha hivihivi tu ni lazima tujiridhishe kuwa askari hao hawakufyatua risasi kwa uzembe,"alisema Kamhanda.

  Kamanda huyo alisema askari hao watahojiwa baada ya kuundwa kwa tume maalumu ya kuchunguza tukio hilo, na tume hiyo ikibaini kuwa kulikuwa na uzembe, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwamo kufikishwa mahakamani.
  Hata hivyo kamanda Kamhanda hakutaka kutaja majina, wala vyeo vya askari hao kwa maelezo kwamba ni ni mapema mno, pia sababu za kiusalama.Katika hatua nyingine Kamhanda alisema tayari watu 54 wamefikishwa mahakamani kutokana na vurugu za juzi.

  IGP Mwema achunguza
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema ametuma kikosi cha maofisa waandamizi kutoka makao makuu ya jeshi hilo, kikiongozwa na Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo, Kamishna Paul Chagonja kwenda mjini Songea kufanya uchunguzi wa ghasia hizo.

  Chagonja akizungumza na Mwananchi jana alisema maandamano hayo hayakuwa ya amani bali ya kihuni kwani yalilenga kuvamia ofisi za serikali ikiwemo Ikulu ndogo na Ofisi ya Mkuu wa mkoa. Chagonja alikuwa akijibu swali lililotaka aeleze endapo haoni kama polisi imetumia nguvu kubwa kutawanya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani.

  "Maandamano ya amani watu wanavamia Ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi ya mkuu wa mkoa?"
  "Sijafika huko ndo naelekea lakini, yale si maandamano ya amani. Yaani wahuni wanataka kuivuruga nchi waachiwe? Kuweni wazalendo, msiwe kama labda ninyi ni waandishi wa BBC kutoka Uingereza, hii ni nchi yenu."

  Alifafanua kwamba, maandamano ya amani yanafahamika kwani watu hulazimika kuomba kibali na kuweka wazi ajenda ya maandamano "Lakini siyo maandamano yale, watu hayakuwa na kibali chochote, wahuni wamejiingiza wanataka kuvuruga nchi tu."

  Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema,"Usifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue hovyo risasi za moto kwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia..., lakini watu wanavamia Ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa, magari ya polisi hapo kuna amani kweli?"

  Alitoa angalizo kwamba ni lazima hata vyombo vya habari, viache ushabiki badala yake viangalie maslahi ya taifa kwani nchi ikivurugika wao pia hawatasalimika na kusisitiza, "Kuweni wazalendo bwana, msifikirie kulishutumu jeshi la polisi tu."

  Wakati IGP akituma kikosi hicho, wanaharakati, wanasiasa na wasomi wamekosoa matumizi makubwa ya nguvu za polisi dhidi ya raia na waandamanaji waliokuwa wakifikisha ujumbe wao kwa mkuu wa mkoa kupinga mauaji ya watu tisa yaliyofanywa kwa imani za ushirikina.

  Juzi wananchi waliokuwa wakiandama kupinga mauaji hayo, walipambana na polisi ambapo watu wanne waliuawa na wengine 41 kujeruhiwa.

  Hali za majeruhi Majeruhi wanane kati ya 11 waliolazwa katika Hospitali ya mkoa wa Ruvuma, jana waliruhusiwa. Majeruhi wengine 30 walipatiwa matibabu juzi na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwao.

  Mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Benedicto Ngaiza alisema tayari wagonjwa wanane kati ya kumi na moja waliolazwa katika hospitali hiyo wameruhusiwa na kwamba ni wagonjwa watutu ndio waliobaki.
  Mmoja wa wagonjwa hao, Shangwe Mtaula (16) mkazi wa Mabatini hadi jana alikuwa hajitambui kutokana na kipigo cha polisi kilichosababisha kuumia vibaya katika paji lake la uso.

  Muuguzi wa wodi alimolazwa mgonjwa huyo, Hildetha Mhonyo alisema binti huyo alifikishwa hospitalini hapo juzi saa tano asubuhi akiwa hajitambui na hivyo alilazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi.

  Muuguzi huyo alisema, bado hali ya Shangwe si nzuri ingawa jana alianza kuzungumza kwa taabu na kwamba anaonekana kuwa na maumivu makali kwenye paji lake la uso, huku macho yake yaonekana kuvimba.Mgonjwa mwingine ni Esta Mbali (29) mkazi wa Mshangano, ambaye amelazwa wodi namba tano baada ya kupigwa risasi katika bega lake la kushoto na kuumizwa vibaya.

  Mgonjwa huyo anasema, hali yake inaendelea vizuri kwa sasa baada ya kupata matibabu. Alisema, katu hatasahau tukio hilo kwani alikuwa akitoka hospiatali kumsalimia binamu yake ambaye alikuwa amejifungua na wakati akiwa njiani alikutana na kundi kubwa la watu wakiandamana na baadaye polisi walianza kuwatawanya kwa mabomu ya machozi, ambapo alifanikiwa kukimbia na kujificha kwenye nguzo ya umeme, lakini ghafla alisikia kitu cha moto kikimuumiza begani mwake . Alisema alipatwa na kiwewe na kuanza kukimbia ovyo, hali iliyosababisha mwili mzima kulowa kwa damu ambayo wakati huo hakuweza kufahamu chanzo chake.

  Esther aliendelea kusimulia kuwa baada ya kutokwa damu nyingi, aliishiwa nguvu na kuanguka, hadi aliposaidiwa na wasamaria wema ambao walimpakia kwenye gari na kumkimbiza hospitalini.
  Mwingine ni Sinje Mchompa (29) mkazi wa Bombambili, ambaye alijeruhiwa katika tukio hilo na kuumizwa vibaya na kipande cha bomu mdomoni eneo la SODECO, wakati alipokuwa akielekea Mabatini.

  Sinje alisema alipokuwa katika eneo hilo ndipo vurugu zilianza na kwamba alishtukia akipigwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni kipande cha bomu mdomoni na kutoboka mdomo hali iliyosababisha meno kuuma sana.

  Mgonjwa huyo ameomba msaada wa kupatiwa matibabu zaidi ili hali yake iweze kurejea kama awali.
  Kwa upande wake Matroni wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma Helta Soko, ametoa ushauri kwa wananchi kuacha tabia ya kufanya vurugu katika maeneo ya hospitalini kwani hali hiyo inasababisha usumbufu kwa wagonjwa waliolazwa.

  Kauli ya Helta inatokana na baadhi ya wananchi kupiga kelele wakati walipokuwa wakiwarushia mawe wauguzi na askari waliokuwa wakipeleka mwili wa mmoja wa waliokufa katika tukio hilo katika chumba cha maiti.  Habari tulizozipata wakati tukienda mitamboni zinasema, kwa mara nyingine, jana saa 12 jioni, polisi mjini Songea walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwaokoa watu wawili waliokuwa wakipigwa na wananchi wakiwatuhumu kwamba ni majambazi wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya wananchi.

  Watu hao ambao walijeruhiwa vibaya walikamatwa na wananchi katika eneo la Mkuzo nje kidogo ya Manispaa ya Songea baada ya kujitambulisha kwa wenyeji kwamba wao walikuwa wakitatafuta shamba la kununua, huku mmoja wao ambaye ni mwanamke akitoroka na kukimbilia kusikojulikana.

  Kutokana na kuwatilia mashaka, wananchi hao waliwazingira na kuwaweka chini ya ulinzi kisha kuwafikisha nyumbani kwa kiongozi wa Serikali ya mtaa wa Mkuzo, John Moyo na baadaye walianza kuwapiga baada ya kutokea utata katika maelezo yao.

  Kuona hivyo moyo alipiga simu polisi ambao walifika na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi, hivyo kuwaokoa watuhumiwa hao kisha kuwakimbiza katika hosipitali ya mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya matibabu.

  Watuhumiwa hao ambao wametambuliwa kwa majina ya Gervase na Juma, walikuwa wakivuja damu katika sehemu kadhaa za miili yao na polisi walipowafanyia upekuzi waliwakuta wakiwa na hirizi na nyaraka zilizoandikwa kwa lugha ambayo haikuwa rahisi kusomeka.

  Chanzo. Gazeti la Mwananchi
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  wanatuzuga tu hawa
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Biashara ya dhahabu........songea itamaliza wengi kama albino vile!!imani hizo za kishirikina zinaathiri hata maendeleo
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Hakuna haja kupoteza pesa za walipa kodi kupeleka maafisa uchynguzi wakati wameshatoa taarifa rasmi ya uchunguzi hata kabla kufika eneo la tukio...hawafai kwenda maana wameshatoa maamuzi wanaenda kufanya nini sasa kama maamuzi yametoka pindi wakita dar bado???wanakula pesa zetu bure
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  • ni bora busara ziwe zinztumia muda mingine nina maana kuwa hakuna haja ya kuwashikilia mateka ktk sakata kama hili
  • ho [p;si janja tu ya kulinda maisha yao
  • hizi tume ni aina ya kubuni namna ya kufungua milango ya kulia hela za vikao
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Uzalendo si kuikinga serikali inapoua wananchi wake!
   
 7. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Hivi mauaji ya Arusha walishapata majibu toka TUME yao ya uchunguzi?????
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hii ni janja ambayo wamekuwa wakiitumia kwa muda mrefu katika kutuliza hasira za wananchi. Hakuna cha maana kitakachopatikana kutoka kwa polisi wa kisiasa.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu ameshatangaza kuwa maandamano yalikuwa ya kihuni sasa anakwenda kuchunguza nini? Kwa hiyo mauaji yalikuwa justified?
   
 10. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Maandamanoya amani watu wanavamia Ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi yamkuu wa mkoa?"
  "Sijafika huko ndo naelekea lakini, yale si maandamano ya amani. Yaaniwahuni wanataka kuivuruga nchi waachiwe? Kuweni wazalendo, msiwe kama labdaninyi ni waandishi wa BBC kutoka Uingereza, hii ni nchi yenu."

  Baada ya kusema haya , hakupaswa kwenda tena huko Songea,au labda anakwenda kutalii na kuharalisha posho ya safari, si kwenda kutafuta chanzo cha tatizo, majibu tayari anayo. WanaSongea msikubali tamko la huyo Chagonja tayari amewadharau, chukueni hatua nyingine.
   
 11. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Unatoa hukumu kabla ya kwenda kuchunguza then unaenda kuchunguza nini sasa
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Viongozi na maafisa wote wa serikali hii akili zao ni kama za JK
   
 13. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu Chagonja ameshatoa verdict kwamba waliouawa walikuwa "wahuni", anaenda kufanya nini huko Songea? Ameshatoa kauli ambazo zinahalalisha vitendo vya askari kuwaua wale raia, kuna haja gani ya kupoteza rasilimali zetu? Atulie mjini aendelee kuwatetea.
   
 14. PakiJinja

  PakiJinja JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Pumbaf......sasa huyo IGP anaenda kuchunguza kitu gani wakati yeye mwenyewe tayari anatoa shutuma kwa wananchi, anawapachika makosa na kuwatetea Polisi wake.
  Kwa nini Polisi iunde tue ya uchunguzi wakati yenyewe tayari ni chombo cha kiuchunguzi? Wasituletee ujinga na kutufanya sisi mahayawani, katika suala imeonekana dhahiri kuwa upande mmoja kuna serikali na vyombo vyake , upande wa pili kuna wananchi, hivyo Polisi inapoteza mamlaki na utashi wa kuunda hiyo tume ya uchunguzi, labda kama wanachunguza ili wayajue mapunggufu yao wa ajili ya kujifanyia marekebisho ya kiutendaji.
  Ningependekeza Jaji mkuu aunde tume hiyo, lakini naye ni tatizo kwa kuwa ni mteule wa rais, pia chombo anachokiongoza ndicho kinatarajiwa kusikiliza hizo, hivyo pia sisi sahih.
  Hivyo hili suala la kuunda tume lingefanywa na bunge, na si Polisi wajichunguze tuhuma zao.
   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkurugenzi wa Operesheni ya Mafunzo KAMISHA Paul Chagonja............ambaye ni next to IGP...........na huyu ndiye mkuu wa mafunzo ya Jeshi la Polisi.....anazungumza ***** namna hii............halafu tunategemea askari wetu wasiue kama wanalishwa SUMU ya ajabu kutoka kwa wakufunzi wao............

  Yaani Uzalendo wa nchi yangu ni kwa Polisi kuua wananchi wanaoandamana?............hivi jamani ni nani ALIYETULAAANI NAMNA HII....mpaka tunaona ni sawa wananchi kupigwa na kuuliwa...........****** tutauendekeza paka lini.............
   
 16. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  S.h.e.n.z.y zako CHAGONJA
   
 17. m

  moma2k JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 953
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 180
  Huyo Chagonja hafai na hana sifa ya kwenda kuchunguza tukio la polisi kua rai Songea, kwa sababu kwa kauli na matendo yake ameonyesha wazi kushabikia na kuunga mkono mauaji hayo yaliyofanywa na Polisi. Je anaenda Songea kutalii(labda hajiwahi fika Songea)? Maana he is already biased ab initio! Itakuwa vigumu sana watu wenye akili timamu waliosoma na kusikia kauli zake akiwa safarini kwenda Songea kuuamini uchunguzi wake. Inahitajika tume huru ya kuchunguza ujinga na unyama huo wa polisi.Polisi hawawezi kujichunguza wenyewe, wakati juzi walishatoa tamko la kubariki mauaji hayo.

  Shida ya polisi TZ:
  i)Bado linaendeshwa kwa mfumo wa kikoloni.
  ii)Mapolisi wengi elumu ya chini sana.
  iii)Polisi hawana mbinu za kisasa za ku deal na waandamanaji(raia).
  iv)Wanategemea mabavu na kuua raia kama suluhisho za kuzima maandamano.
  v)Hawaijui katiba ya nchi.
   
 18. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa kauli hizi za Chagonja hao askari waliotiwa ndani watolewe tu kwani hata yeye kakiri ange ua.
   
 19. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  bila chombo cha kudhibiti matendo ya jeshi la polisi tz naona MAUAJI YA SOWETO YANAKARIBIA TZ
   
 20. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Kwako IGP Said Mwema, tokea umepewa cheo hicho na partner wako nchi yetu imekumbwa na mikikimikiki mingi kutoka kwa polisi wako.
  Ditopile alimuua dreva wa daladala mkasema ilikuwa bahati mbaya, Zombe akaamrisha maaskari wawachinje wale vijana wa Morogoro ili awapore pesa zao na sasa hivi Zombe na wenzie wako uraiani ila yule shahidi muhimu kafa bado kesi ikiendelea, Nyamongo watu wakauawa eti walikuwa wanataka kuvamia mgodi, Arusha nako Mwema ukawa na taarifa za kiintelijensia kwamba kutakuwa na vurugu kumbe kuna njama jeshi la polisi linataka kuua, na sasa huko Songea polisi wanaua watu ambao hata manati hawana.
  Chagonja anakuja na propaganda za kuhalalisha mauaji haya kwamba eti wale ni wahuni! Sheria gani nyie polisi mliokuwa nayo ya kuhukumu au mnataka na sisi tuanze kuwashughulika mkiwa kwenye anga zetu? Mnatutia kichefu chefu na hasira, tukiamua nyie hamko wengi wala hamna silaha za kutosha kutukabili, na kwa taarifa yako
  uvumilivu wetu unakaribia kufika mwisho.

   
Loading...