Polisi wanawake toka UK watoa mafunzo kwa polisi wenzao wa Tanzania

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
POLISI WANAWAKE TOKA UK WATOA MAFUNZO KWA POLISI WENZAO WA TANZANIA

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

DAR ES SALAAM JUMANNE AGOSTI 24, 2010. Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza, wameanza kutoa mafunzo kwa maafisa wakuu na wa ngazi ya kati wa Mtandao wa Polisi wanawake ili kuwajengea uwezo na moyo wa kujiamini kama hatua ya kujiandaa kwa nafasi za juu za uongozi kwenye Jeshi hilo.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, Naibu Kamishna wa Polisi(Deputy Commissioner of Police) DCP Rashidi Omari, kutoka ofisi ya Tathmini na Ufuatiliaji ya Jeshi la Polisi, amesema kuwa mafunzo hayo ni maandalizi ya kuwapatia Polisi wanawake nafasi za juu ya maamuzi kwenye Jeshi hilo.

Awali Mwenyekiti wa Mtandao huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi Zuhura Munisi, Mkufunzi kutoka Uingereza Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (Chief Superintendent of Police), Queen Alison na M/S Susie Kitchens, British Deputy High Commissioner, walisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo na kuwafanya wajiamini wanapopata madaraka ya juu.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi Celina Kaluba, ameelezea matumaini yake baada ya kupata elimu hiyo kutoka kwa Polisi wanawake wa Uingereza.

Akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo, kamanda wa Polisi mkoani Singida kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Celina Kaluba, amesema kuwa kwanza imekua kama historia kwa wanawake wa ngazi hiyo kupatiwa mafunzo ya muda mrefu kwa pamoja.

Zaiidi ya Polisi 20 wanawake kutoka mikoa yote hapa nchi, wanahudhuria mafunzo hayo yanayofanyika kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam (Tanzania Police Academy).

Mwisho
 
Back
Top Bottom