Polisi, wananchi wajeruhiwa kwenye mgogoro wa ardhi Dodoma

Taarifa yako haijakaa vizuri mkuu! hebu fafanua vizuri hao watu waliouawa na polisi wa ccm waliuawa katika mazingira gani?
Je, walikuwa kwenye maandamano?
Au walikuwa majambazi?
Au walikuwa wanapita tu njiani wakaamua kuwapiga risasi

ili uelewe alichokisema, tafadhali pitia link hii

[h=1]Topic: Vurugu kubwa zaibuka dodoma[/h]
 
walikosea toka mwanzo ilikuwa kabla ya bomoa bomoa Wavae kofia za kijani na T-shirt za njano na wapeperushe bendera za kijani. Wabomoaji wangerudi nyuma. lakini ujombe ni " UKIPENDA BOGA PENDA NA UA LAKE" Maana yake " Ukipenda CCM penda na mambo yake"
 
Mh Rais, kinachofanywa na serikali yako ni uhuni mkubwa. Tena ukatili usiosemeka, kupoteza maisha ya watu kwa ajili ya matakwa ya mtu mmoja ni jambo lisilovumilika hata kidogo. Hivi sasa wananchi wanauwawa kwa kupigwa risasi huko dodoma huku serikali yako imekaa
kimya. Huo ni uonevu.
Mkuu Kibwenga dah mpaka huku upo hata hivyo pole sana unaonekana una hasira kweli kweli..............sikudhani kama una jazba kiasi hicho we rudi kule tu ukapunguze stress
 
naomba cdm ochukue madaraka na baada ya miaka 10 au 20wananchi wapate somo kama ilivyotokea zambia
 
Wabomolewe tuu,mkoa wa dodoma unaikumbatia sana ccm na hiyo ndiyo faida yao
 
wanataka wabomoe nyumb za wagogo ajenge shule ya chekechea na sec, source radio 5
Kama ni hivyo hiyo ni kashfa kubwa kwa serikali yaani inabomoa ili ujenge sekondari! Kuna shule inaitwa Irambo ipo mbali sana tokea Mbeya mjini lakini inapata wanafunzi wengi tena wengine toka Dsm sasa iwaje huyo jamaa ang'ang'anie kujenga hapo kama fremu ya duka kwamba nikikosa kujenga hapa basi biashara yangu haitakuwa nzuri kama nikijenga pale. Halafu huyo mtu anayetaka kujenga alimilikishwa lini?
 
thanx mkuu.

Wakati wa uchaguzi walielezwa kupitia kampeni ya nyumba kwa nyumba kuwa wakichagua CDM, CCM itaondoka na pesa zake na kwakuwa wapinzani hawana hela mtakufa (wagogo) na njaa. Sasa nyumba zote chini na huyo jamaa alienunua eneo hilo kaja Dodoma miaka ya tisini nakukuta eneo likiwa likaliwa na wakazi.

Chakushangaza mamlaka ya ustawishaji makao makuu inadaiwa ilishawapa wananchi hao namba za maeneo hayo wanayokalia hii inamaanisha wanatambulika kisheria lakini si kitajiri.

Hili linafanana na lile tukio la mwenyekiti wa mkoa wa ccm mwanza bwana mabina kununua eneo kisesa ambalo wananchi wanaishi hapo.

Hii ndio ccm bwana na si shangai
 
Nafikiri kuna baadhi yetu hatujui maana ya nyumba, yaani mtu akubomolee nyumba yako?

nakubaliana na wewe. Halafu sielewi hao wanabomoa kwa amri ya nani? Sidhani kama CDA ina mamlaka ya kufanya maamuzi hayo kwa shauri lililo mbele ya Mahakama, unless kuna jambo halieleweki hapa.
 
Ni kweli Kuwabadilisha watu inaitaji muda na kuendelea kuwaeleza ya kile tunachokiamini,watapinga kwa muda fulani, lakini watakapo anza kupata uelewa wa kile tunachokisimamia na ukweli wake wataanza kubadilika.

Hongera MWITA 25 NAPATA MATUMAINI KTK MICHANGO YAKO SASA KWAMBA NURU IMEKUWAKIA KAKA.
Poleni ndugu zangu wa dodoma kwa madhila iliyopata, Mungu awatie nguvu ktk wakati huu mgumu.
 
Natoa pole kwa victims wote wa tukio hilo.
Tatizo lipo kwa serikali yetu wakati watu wanajenga waliwaona wakakaa kimya bila kupima viwanja na kuwajulisha wananchi maeneo halali kujengwa.
Hili bomu lipo sehemu nyingi hapa nchini kwahyo litakuwa linalipuka kila kukicha.

Mfano ni pale Morogoro maeneo ya Chamwino watu wamejenga/wanajenga hovyohovyo tu sitashangaa na wao wakiambiwa wabomoe au wakibomolewa.

Hii yote imesababishwa na serikali kwa miaka 50 sasa hawajawahi kuwa na mpango wa kupima ardhi yote ya nchi yetu sana sana wameishiwa kupima 10% ya ardhi hili tatizo yaani kwa wastani kila mwaka wanapima 0.2% yaani itatulazimu kutumia miaka 450 kupima ardhi yote.

Is this wise? The answer is BIG NO
 
Back
Top Bottom