Polisi, Wanajeshi na maafisa wa serikali kuwa juu ya sheria.

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,388
2,000
Habari zenu wakuu, hii nimeiona mara nyingi sana na imekuwa ni kawaida kwa askari Polisi,mwanajeshi au maofisa wa serikali kuwa juu ya sheria sijajua kama ni sheria zetu ndio zinasema hivo au ni mazoea tu ???

Kwa mfano, ni jambo la kawaida Polisi akiwa kwenye gari yake binafsi kutokutii sheria za barabarani kisa tu amevaa sare za kazini. Na ndio hivyo hivyo kwa wanajeshi au usalama wa taifa na wengineo wenye mamlaka kwenye nchi hii kutokutii sheria za barabarani au mara nyingine hata kwenye vyombo vya maamuzi watatumia nyadhifa zao.

Waweza kumkuta mwanajeshi anaenda kumkamata mtu kitemi kumfikia kituo cha polisi kisha akawaamuru Polisi ole wenu mumtoe bila ya ruhusa yangu mutanijua mimi ni nani jamani hii sheri inasemaje kwenye vitu hivi ????
 
Wissman

JF-Expert Member
Dec 12, 2014
997
1,000
Wanajeshi wamezidi kwa hilo.. Kurukisha watu vichura, kupiga, kukuvua jezi yao mahali popote watakapojiskia wao kisa tuu mtu amevunja sheria kwa kuivaa, na mengine mengi sana. Mi nilishashuhudia trafiki akipewa mkongoto wa nguvu toka kwa mjeshi kisa aliwasimamisha(daladala) na kuwaambia abiria washuke dereva apeleke gari kituoni. Dereva alikuwa hana "gazeti" la kumwachia
 
Sheria inasemaje kuhusu hili jambo,ina maana raia hawezi kulishitaki jeshi (JWTZ) ???
 
darts

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
257
250
Kaka Vitu vingine usitake Watu wakijibie wewe fanya practical then uje utujuze mrejesho Maana Suala lakusema SHERIA inaruhusu kwani kuhusu kuvunjwa kwa Shelia na mambo yanaenda Umeona eneo Moja kaka . TRA UKO KODI HAZIKUSANYWI ,LEO NDIO TUNAONA MAOSPITALINI ,MASHULENI DAH .

Ndugu mrejesho plz
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom