Polisi wanadaiwa kushikilia simu 18 za wanawake wa CHADEMA Pamoja na gari la mmoja wao kwa zaidi ya miezi miwili

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,796
2,000
Taarifa hii ya kusikitisha na kufedhehesha imefichuliwa na Msemaji wa Chama hicho wa Kanda ya Pwani Mh Gervas Lyenda.

Inadaiwa wamama hao walikamatwa Kwenye viunga vya Mahakama ya Kisutu siku ya Kesi ya Mwenyekiti wa Chadema tarehe 5/8/2021 na kulundikwa Police Central kwa siku 5 mfululizo , huku ndugu zao na wanasheria wao wakikatazwa kuwaona , mmoja wa wamama hao aliyekuwa na gari binafsi , gari yake hiyo nayo imewekwa selo hadi leo hii kwa kosa la kuendeshwa hadi Mahakamani.

Hata hivyo juhudi za wamama hao kudai simu zao zimegonga mwamba, kwa vile kuna TETESI KWAMBA SIMU ZAO HAZIPO , POLISI WAMEGAWANA (tunaendelea kutafuta ukweli). 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
6,385
2,000
Taarifa hii ya kusikitisha na kufedhehesha imefichuliwa na Msemaji wa Chama hicho wa Kanda ya Pwani Mh Gervas Lyenda .
Tumia akili kuandika wamezichukua kwa uchunguzi kila aliwahi kukamatwa na polisi anajua hili ,acha kupotosha

USSR
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,720
2,000
Polisi wa Tanzania, ukiwashirikisha kwenye tukio ambalo kuna hela au vitu vya thamani, utajuta. Hakuna tofauti na ukimshirikisha jambazi.

Hata kwenye zoezi la kuwaondoa machinga, wakitumika tu polisi, mali nyingi zitaibiwa na polisi. Ukidai sana unaweza kuuawa au kubambikiwa kesi.

Kumbukeni kilichowatokea wafanyabiashara wa madini wa Morogoro. Walinyang'anywa fedha, wakauawa, na kisha kutangazwa kuwa ni majambazi. Hao ndio polisi wa Tanzania.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,720
2,000
Tumia akili kuandika wamezichukua kwa uchunguzi kila aliwahi kukamatwa na polisi anajua hili ,acha kupotosha

USSR
Mimi na wenzangu tuliwahi kuvamiwa na majambazi hotelini, polisi waliitwa. Siku ya 2 majambazi walikamatwa na vitu vyetu vyote.

Tuliitwa kuvitambua vitu vyote, isipokuwa fedha. Mimi niliitambua simu yangu. Nilifuatilia hiyo simu, mwanzoni niliambiwa ni kielelezo, nitapewa baadaye. Baadaye nikaambiwa haionekani. Ikawa ndiyo mwisho.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,211
2,000
Mimi na wenzangu tuliwahi kuvamiwa na majambazi hotelini, polisi waliitwa. Siku ya 2 majambazi walikamatwa na vitu vyetu vyote. Tuliitwa kuvitambua vitu vyote, isipokuwa fedha. Mimi niliitambua simu yangu. Nilifuatilia hiyo simu, mwanzoni niliambiwa ni kielelezo, nitapewa baadaye. Baadaye nikaambiwa haionekani. Ikawa ndiyo mwisho.
Kuna simu yangu iliporwa na Polis mwaka 2013 iPhone 4 wakati huo ziliuzwa laki sita bahati nzuri sikutoa password, lakini waliuza kama screpa aisee
 

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,178
2,000
Hivi nini kazi ya mifuko mikubwa miguuni mwa suruali yake? Ni kutunza risasi? Hapana. Sasa nini kama si kutunza pesa na simu wanazokwapua
 

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
9,261
2,000
Taarifa hii ya kusikitisha na kufedhehesha imefichuliwa na Msemaji wa Chama hicho wa Kanda ya Pwani Mh Gervas Lyenda...
Haya mambo ndiyo yanaleta aibu kubwa.

Hivi wanaoenda mahakakamani kufuatilia kesi za jamaa zao huwa hawaruhusiwi kwenda na magari binafsi?

Polisi inakosea na hili ndilo linapelekea kuonesha UOVU mkubwa dhidi ya sheria za nchi
 

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
9,261
2,000
Tumia akili kuandika wamezichukua kwa uchunguzi kila aliwahi kukamatwa na polisi anajua hili ,acha kupotosha

USSR
Hiyo gari ilibeba vilipuzi?

Tunajitukanisha sana tukiendelea kutetea huu mwenendo wa jeshi la polisi kufanya unyama kwa kigezo cha kisiasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom