Nipo karibu na uwanja wa Soweto ambapo Polisi wameuzunguka huku katikati mwa uwanja kukiwa na magari mawili ya matangazo ya CDM na Hema pamoja na viti.
Polisi ni wengi kuliko kawaida na wapo na Magari ya Maji ya kuwasha.lengo ni kuhakikisha kwamba Wafuasi na Wanachadema hawapati nafasi ya kuwaaga Marehemu wa Mlipuko wa Bomu uliotokea ktk uwanja huohuo wa Soweto.
Leo ndio ilikua siku ya kuwaaga marehemu ktk viwanja hivyo vya soweto. Watu wengi hapa Arusha kutoka kata mbalimbali walijitayarisha kwenda kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Marehemu.
Kuzuiwa huku kwa watu kwenda uwanjani SOWETO ni muendelezo wa Hujuma na Uonevu unaofanywa na jeshi ka polisi kwa maagizo Viongozi wa serikali na CCM dhidi ya CHADEMA.
Hii ni hatari sana kwa Amani ya nchi yetu. Watu wamekufa na wengine kujeruhiwa,lakini bado serikali kwa kutumia jeshi la polisi linaendeleza hasira kwa Wafiwa bila kujali kwamba CDM na wanachama wake wanaweza kutumia nguvu kuingia uwanjani kitu kinachoweza kuhatarisha Amani na kuleta Vurugu na Vifo vingine.
Polisi tunaomba msikubali kutumika na watawala kwa Maslahi yao.