Polisi wamwagwa uwanja wa SOWETO hakuna mtu yeyote kukatiza!

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Nipo karibu na uwanja wa Soweto ambapo Polisi wameuzunguka huku katikati mwa uwanja kukiwa na magari mawili ya matangazo ya CDM na Hema pamoja na viti.

Polisi ni wengi kuliko kawaida na wapo na Magari ya Maji ya kuwasha.lengo ni kuhakikisha kwamba Wafuasi na Wanachadema hawapati nafasi ya kuwaaga Marehemu wa Mlipuko wa Bomu uliotokea ktk uwanja huohuo wa Soweto.

Leo ndio ilikua siku ya kuwaaga marehemu ktk viwanja hivyo vya soweto. Watu wengi hapa Arusha kutoka kata mbalimbali walijitayarisha kwenda kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Marehemu.

Kuzuiwa huku kwa watu kwenda uwanjani SOWETO ni muendelezo wa Hujuma na Uonevu unaofanywa na jeshi ka polisi kwa maagizo Viongozi wa serikali na CCM dhidi ya CHADEMA.
Hii ni hatari sana kwa Amani ya nchi yetu. Watu wamekufa na wengine kujeruhiwa,lakini bado serikali kwa kutumia jeshi la polisi linaendeleza hasira kwa Wafiwa bila kujali kwamba CDM na wanachama wake wanaweza kutumia nguvu kuingia uwanjani kitu kinachoweza kuhatarisha Amani na kuleta Vurugu na Vifo vingine.
Polisi tunaomba msikubali kutumika na watawala kwa Maslahi yao.
 
Hii nchi inatawaliwa kijeshi sio haijawekwa wazi tu,nashangaa leo hii Nape,Mwigulu wanaweza amrisha askari,usalama wa taifa fanya hivi na wakafanya-ni aibu sana na ni unethical kuanzia duniani hadi Mbinguni

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hiyo ni strategy ya magamba,wanaamini wakiruhusu watu watakuwa wengi mno nahivyo kuleta picha kuwa iwapo uchaguzi ungefanyika cdm wangeshinda.
 
That is exactly the right thing to be done. Huu upuuzi wa watu kurusha wenyewe mabomu na kisha kutumia misiba kama njia ya kujipatia umaarufu tumeshauchoka. Watu washaamua ku deal na nyinyi jino kwa jino. Na kwa vile meno yenu ni dhaifu na machache, ni muda mfupi tu mtakuwa VIBOGOYO. Hamfiki2015 na mkifika mtakuwa dhsifu saaaaaana
 
Serikali ya Kipuuzi, Matamko ya Kipuuzi na kila kitu chao cha kipuuzi......waulize kwanini sasa wanawazuia watu kwenda hapo. Utaambiwa eti Intelijensia yao imeonyesha kuwa kutakua na Machafuko....... upuuzi mtupu, watu wamekusanyika tangu juzi, mbona hatujaskia chochote wala lolote? I hate CCM and its puppets

CC: zumbemkuu Mohamedi Mtoi MANI
 
Last edited by a moderator:
sometimes mtu unapata mawazo mabaya ujue.....ni upuuzi wa hali ya juu sana huu. They can not stop them rather than encouraging them to move forward
Laiti ningekuwa pande hizo, ningejitoa mhanga niingie kwa nguvu nione itakuwaje.
 
Kuna mtu niliwahi kufanya nae kazi alikuwa mtu wa ajabu. Hisia zake zilikuwa zinakuja baada ya saa 24! Mfano mnaongea, mtu anatoa kisa cha kufurahisha na kuchekesha, watu mnacheka mnafurahi. Ila jamaa yetu anabaki kimya. Kesho yake utaona anaanza kucheka na kurukaruka halafu atauliza "fulani kumbe kumbe ndio maana jana mlicheka sana." Yaani wakati watu walicheka jana yeye leo ndio anacheka wakati watu tayari wamesahau na kuanza mambo mengine.

Sasa Polisi badala ya kutoa ulinzi kabla na wakati watukio wanatoa ulinzi wa kiwanja siku tatu baada ya tukio. Kweli haya ni maajabu ya karne.
 
Hao police (Njuka kutoka CCP) wapo hapo uwanjani toka saa kumi na moja alfajiri. Kamwe hawawezi kuzuia mkusanyiko wa kuwaaga waanga wa shambulio la J'mosi. Tena waache watu waage wapendwa wao kwa amani.
 
Sasa tumefikia baya jamani.Uongozi wa Cdm hawa mashetani wanawatafuta kuwa angamiza,waachieni uwanja huo na amieni kwa wafia mmoja mmoja kwa nguvu moja na Umoja wenu.
 
Japo nipo mbali na arusha lakini nimevaa kombati nyeusi kuomboleza msiba huu wa kitaifa,hakika nepi and company mnalojivunia linakwenda kufika mwisho soon!!huyo fastijeti mfanyeni kama ndio mungu wenu kitaeleweka tu!!!!
 
Kwani huu msiba ni wa CHADEMA ama wananchi wote. Inasikitisha sasa kuona kuwa kama msiba ukiratibiwa na CCM inamaana wahusika na msiba huo ni wana CCM tu. Siamini kama Tanzania tumeshafika hapa, kwanini nguvu kubwa hii wasitumie kuwalinda ili madhara yanayotokea yakome?
 
Nipo karibu na uwanja wa Soweto ambapo Polisi wameuzunguka huku katikati mwa uwanja kukiwa na magari mawili ya matangazo ya CDM na Hema pamoja na viti.

Polisi ni wengi kuliko kawaida na wapo na Magari ya Maji ya kuwasha.lengo ni kuhakikisha kwamba Wafuasi na Wanachadema hawapati nafasi ya kuwaaga Marehemu wa Mlipuko wa Bomu uliotokea ktk uwanja huohuo wa Soweto.

Leo ndio ilikua siku ya kuwaaga marehemu ktk viwanja hivyo vya soweto. Watu wengi hapa Arusha kutoka kata mbalimbali walijitayarisha kwenda kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Marehemu.

Kuzuiwa huku kwa watu kwenda uwanjani SOWETO ni muendelezo wa Hujuma na Uonevu unaofanywa na jeshi ka polisi kwa maagizo Viongozi wa serikali na CCM dhidi ya CHADEMA.
Hii ni hatari sana kwa Amani ya nchi yetu. Watu wamekufa na wengine kujeruhiwa,lakini bado serikali kwa kutumia jeshi la polisi linaendeleza hasira kwa Wafiwa bila kujali kwamba CDM na wanachama wake wanaweza kutumia nguvu kuingia uwanjani kitu kinachoweza kuhatarisha Amani na kuleta Vurugu na Vifo vingine.
Polisi tunaomba msikubali kutumika na watawala kwa Maslahi yao.

Hata wengejaza polisi,mie naamini hakuna siku ambayo nuru ilishindwa na giza watajalibu kila hila wakidhani wanaikomoa cdm lakini ukweli utabaki pale pale,huwezi kuzuia watu kuaga miili ya watu waliokuwa kwenye mkusanyiko wa kampeni za cdm,infact tukio kama hilo nilitegemea intelijensia ya polisi ingebaini kama inavyoweza kubaini wakati cdm inapotaka kufanya mikutano,ipo wapi Movie ya aliyuemteka Ulimbola,Kibanda,Mwangosi,na mengine mengi wanaweza kufanikiwa kwa muda mfupi kuzima sauti za wanyonge kupitia jeshi la polisi lakini hila hiyo itafika mwisho.
 
Mwanga ndio anaweza kufanya hivyo.

Huu ukandamizaji wa Polisi ndiyo unaopelekea damu iendelee kumwagika, kwanini uzuie watu kushiriki kuwaaga wanachama wao? walio uawa ni wanachadema na wanachadema wanataka kuwaaga Polisi haitaki.
 
Back
Top Bottom