Polisi Wamuua Mwenzao, Wasingizia Majambazi. Polisi Kudanganya, si Tanzania Tu?

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,265
21,439
Nadhani tumezoea sana hapa Tanzania kupata matukio ya Polisi kusema uwongo. Tukumbuke kwamba Polisi lazima ale kiapo cha uaminifu katika kazi yake, lakini mara nyingi ni kama kiapo hicho kinatolewa kama kasuku kuongea maneno ya binadamu. Kuna wakati unapata matukio watu wanauawa na polisi, na polisi wanasema walikufa katika kujibishana risasi.

Miaka ya nyuma tunakumbuka wafanya biashara wa madini waliuwawa na polisi na kuporwa madini na polisi wakasema waliwaua kama majambazi. Matukio ya polisi kubambikia watu kesi hapa nchini wengi tunayajua. Tunajua wapo baadhi ya polisi wachache waaminifu, lakini, kwa ujumla, ni kawaida polisi wengi kusema uongo bila kujisikia anafanya kosa? KUna matukio mengi madogomadogo hapa nchini polisi wanasema uongo bila hata aibu. Najua anaedanganya kirahisi katika dogo atanganya katika kubwa. Huo ndio ukweli.

Labda ndio, na sio hapa kwetu tu. Huko Marekani, hasa katika kuuwawa na polisi kwa watu weusi, mara nyingi sana Polisi wamesema uongo.

La kushitua ni hapa juzi huko Afrika kusini, polisi, akiwa amevaa uniform, wakiwa katika tukio la ujambazi, aliamua kumpiga polisi mwenzie risasi ya kichwa na kumuua na yeye na polisi wenzake wakadai huyo polisi mwenzao aliuwawa na majambazi katika majibizano ya risasi. Kumbe kulikuwa na video iliyochukua tukio zima na ukweli ukaja kujulikana.

Jambo hili limenifanya njiulize sana. Hivi polisi bila kujali kiapo chao, kusema uongo ni jambo la kawaida hapa Tanzania na kwingineko duniani? Kama ni hivyo basi inabidi nimwogope polisi nisiejua ana nia gani na mimi kuliko hata jambazi ninaejua hana nia nzuri na mimi.

Soma hii habari;
How can police officers, sworn under oath, lie like this? | IOL
 
Polisi wao kwa wao wenyewe hawaaminiani, usije kumuamini polisi hata siku moja, polisi anakuua huku anacheka
 
Back
Top Bottom