Polisi wamuiba majeruhi Ukerewe, wamwadhibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wamuiba majeruhi Ukerewe, wamwadhibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zhule, Jan 22, 2010.

 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo inakuaje hii
  Frederick Katulanda, Ukerewe

  SIKU chache baada majeruhi wa tukio la ujambazi lililoua watu 14 kwenye kisiwa cha Izinga, Ukerewe kutoboa siri kuwa askari polisi wawili walikuwa miongoni mwa wavamizi, maofisa wa Jeshi la Polisi wamemchukua mmoja wa majeruhi hao na kumpa kipigo kisha kumrejesha wodini kwa siri.

  Inadaiwa kuwa majeruhi huyo, Vitus Mahendeka, 43, alichukuliwa kwa siri majira ya saa 5: 23 asubuhi na ofisa mmoja wa juu wa polisi wilayani Ukerewe na alipelekwa kwenye kituo cha polisi ambako alikabidhiwa kwa maofisa wengine ambao walimpa mateso hayo.

  Katika toleo la juzi la Mwananchi, iliripotiwa kuwepo kwa taarifa zinazodai kuwa polisi wawili walihusika katika tukio hilo la ujambazi na kunukuu baadhi ya majeruhi hao walioeleza taarifa hizo kwa siri baada ya kuonywa na maofisa wa jeshi hilo wilayani Ukerewe kuwa wasitoboe siri hiyo.

  Habari zilizopatikana kutoka ndani ya jeshi hilo wilayani hapa na katika hospitali hiyo ya wilaya, zimeeleza kuwa majeruhi huyo alifikishwa kituoni kwa mahojiano kutokana na maofisa wa polisi kutaka kuwajua majeruhi waliokaidi agizo lao la kutoeleza kuhusika kwa askari wao katika tukio hilo la ujambazi.

  "Nimefuatwa na askari mmoja ambaye alinipeleka kituoni. Alinieleza kuwa ninatakiwa kutoa maelezo polisi hivyo nikaongozana naye. Nilipofika huko niliulizwa kuwa mie ndiye niliyeeleza kuwa kuna polisi aliyehusika na wizi huo. Sikuwa najua kitu, niliwajibu lakini walianza kunipiga kwenye majeraha yangu kwa kutumia virungu vyao," alieleza Vitus.

  Alisema kuwa alipigwa kwa zamu na askari zaidi ya watatu huku kila mmoja akimuuliza maswali yake na wengine wakimshinikiza kukubali kuwa yeye ndiye jambazi kwa vile alikuwa akiwasingizia askari mwenzao kw alengo la kujilinda asikamatwe.

  "Niliwajibu mimi sijui na kwanza nilikuwa nikiishi mjini Nansio na kuwataka kuuliza ndugu zangu na kufuatilia historia yangu, lakini waliendelea kunitesa mpaka mwajiri wangu alipofika na baadhi ya ndugu zangu ambao walinifuatilia baada ya kuambiwa kuwa nilikuja na askari kituoni," alifafanua.

  Alisema baada ya kukamilisha mateso yao walimruhusu kureja wodini lakini wakamuonya kutotaaja wala kueleza jambo hilo kwa watu ili asipate adhabu nyingine.

  Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo na kuomba masuala yanayohusiana na polisi katika uchunguzi wa tukio la uvamizi huo yaache mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.

  Afisa mmoja wa hospitali alisema kuwa jeshi hilo halizuiwi kufanya kazi lakini linapaswa kufuata taratibu.

  "Hatuwezi kuwazuia kufanya kazi yao, lakini kumchukua mgonjwa ambaye tunaendelea kumtibu ni lazima wawasiliane na uongozi wa hospitali, huo ndio utaratibu wa kazi,"alieleza.

  Hata hivyo, alisema baada ya kusikia taarifa za kuchukuliwa kw amajeruhi huyo, walimfuata na kujiridhisha na kubaini kuwa alikuwa mikononi mwa polisi.

  Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limetangaza kuunda kikosi kazi maalum kwa ajili ya kupambana na majambazi na maharamia ndani ya Ziwa Victoria, ambako kumekuwa kukiripotiwa vitendo vya ujambazi na ukatili dhidi ya wananchi na wavuvi.

  DCI Manumba alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokana na ongezeko la vitendo vya ujambazi na hasa tukio la Januari 17 mwaka huu ambalo lilitokea katika kisiwa cha Izinga na kusababisha vifo vya watu 14 na wengine 18 kujeruhiwa.

  Alisema kuwa lengo la kuundwa kikosi kazi hicho ni kusambaratisha mtandao wa ujambazi katika ukanda huo wa Ziwa Victoria ambao umeoonekana kuota mizizi kiasi cha kupoteza maisha ya wananchi kila siku.

  Alisema kikosi kazi hicho kinaundwa na maofisa mbalimbali toka idara za usalama wa taifa, makachero toka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai pamoja na vikosi vya ulinzi vya polisi toka katika mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara ambayo inazunguka Ziwa Victoria.
  Pia alisema kuwa watu 10 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio hilo la kutisha na kwamba tayari wameshafanikiwa kunasa silaha mbili na risasi 68.
   
Loading...