Polisi wamsaka 'Daudi Balali' anayemiliki ukurasa wa Twitter

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,189
103,708
Jeshi la Polisi nchini linaendelea kufanya upekuzi wa kumnasa mtu anayetumia akaunti ya Daud Balali kwenye mtandao wa Twitter. Jeshi linasema kuwa akaunt hiyo fake imekuwa ikifanya uchochezi na upotoshaji dhidi ya serikali ya Tanzania...

Jeshi la Polisi nchini linafanya uchunguzi kumbaini mmiliki wa ukurasa wa twitter unaoendeshwa na anayejiita Daudi Balali, aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba, aliyasema hayo wakati akizungumza na Nipashe ofisini kwake jana.

Bulimba alisema kuwa taarifa za uwapo wa ukurasa huo wa twitter, wamekwishazipata na wanafanya uchunguzi wa kina kumkamata mhusika kisha kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

"Tunazo taarifa juu ya ukurasa huo wenye wafuasi wengi kwa sasa na unaotumika kuwashambulia viongozi wa serikali na wa siasa hasa wale wanaogombea nafasi kubwa za utawala nchini, hivyo Jeshi la Polisi lipo kwenye uchunguzi ili kumbaini mtu huyo haraka iwezekanavyo," alisisitiza Senso.

Ukurasa huo ulioanza kutumika kabla ya Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni kuanza kutumika, una wafuasi zaidi ya 6,000 kwa sasa na umekuwa ukitumika kuwachafua wagombea urais nchini hasa wa upinzani.

Aidha, umekuwa ukitabiri matokeo ya uchaguzi, kitendo ambacho kimekuwa kikiwachanganya wananchi.
Bulimba alisisitiza kuwa jeshi hilo liko makini na linafuatilia hivyo mtu huyo atasakwa na kukamatwa akiwa mahali popote.

Aliwataka pia wananchi kuripoti katika vituo vya polisi pindi wanapopata vitisho vya aina yoyote, kudhalilishwa ama kufanyiwa kitu chochote kibaya kupitia mitandao ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

"Jeshi la polisi linafanya kazi usiku na mchana, hivyo mtu yeyote asijidanganye kwamba atavunja sheria na asikamatwe, maana tuna njia nyingi za kuwabaini watu hao kwa kushirikiana vyema na TCRA pamoja na wananchi, hivyo chanzo chochote kinachohusu uhalifu wa mtandaoni, kitashughulikiwa," aliongeza.

Aliwaonya pia watu waliokuwa wakitumia kurasa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya watu wengine ili kudhalilisha watu na kupotosha umma kwa kutoa taarifa za uongo juu ya masuala mbalimbali kuachana mara moja na tabia hiyo maana wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwa mfano kwa wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Chanzo: Nipashe.com
 
yaani serikali yetu kweli nivituko hivi jeshi la polisi suala la kumsaka huyo balali wa kwenye fb laweza kumaliza hata miezi sita wakati ilitakiwa hata siku 3 haiishi awe ashatiwa ndani tena mnamchomoa kama kuku wa kuku wa kisasa .
 
yaani serikali yetu kweli nivituko hivi jeshi la polisi suala la kumsaka huyo balali wa kwenye fb laweza kumaliza hata miezi sita wakati ilitakiwa hata siku 3 haiishi awe ashatiwa ndani tena mnamchomoa kama kuku wa kuku wa kisasa .
Acha kujidanganya sio kzi rahis kiihivyo kama unavyodhani may be huyu mtu ni mbulula kumbuka hata IS na alshaabab wana ac Twitter na Fb tatizo ni makapuni haya hayatoi taarifa za wateja wao hata iweje
 
Jeshi la polisi nchini linaendelea kufanya upekuzi wa kumnasa mtu anayetumia facebook account ya Daud Balali.Jeshi linasema kuwa akaunt hiyo fake imekuwa ikifanya uchochezi na upotoshaji dhidi ya serikali ya Tanzania...

Chanzo: Nipashe pg5

Kupatikana kwake ni sawa na kutafuna chuma, uyu mtu hawatamkamata kiwepesi kiivyo mapaka jeshi linatangaza inaonyesha wameshindwa coz kutangaza tu pia ni njia ya kumtisha muhalifu asiendelee kutumia iyo acc
 
Mbona fb hamna jina kama hilo? ila yupo tweter anaandika maneno makali sana! ingekuwa yupo huko ulaya mda sana wangekuwa wamesha mtia mikoni mwao
 
Yule wa twitter ndo balaa

Tangu wamkamate yule wa fb aliyekuwa akifurahia mauaji ya police kuwakamata hawa wengine si rahisi hata kidogo maana tayari wanajua kuwa wanatafutwa,halafu huyu Daudi Balali wa fb isije kuwa Balali mwenyewe orijino maana sisi tunajua kuwa Daudi Balali hajafa,ila ni usanii tu wa serikali ya magamba,hata mjinga kiasi gani hawezi kuamini,kwa kweli ccm mmetufanya sisi majuha kwa muda mrefu sana,mtu mwenye hadhi ya gavana anafariki ughaibuni halafu anazikwa huko huko,does this sense? Gavana wa benk kuu ya taifa azikwe nje ya nchi kwa sababu zipi hasa? Hakukuwa na pesa za kusafirisha maiti yake kuleta nyumbani? Kwanini ccm mnatufanya sisi majuha kiasi hicho? CCM muogopeni Mungu mna matendo ya ajabu sana,we need our Daudi Balali back,otherwise ipo siku mtajibu kila ovu mlilofanya,msidhani Mungu haoni upuuzi wenu wa ajabu.
 
Jeshi la Polisi nchini linaendelea kufanya upekuzi wa kumnasa mtu anayetumia akaunti ya Daud Balali kwenye mtandao wa Twitter. Jeshi linasema kuwa akaunt hiyo fake imekuwa ikifanya uchochezi na upotoshaji dhidi ya serikali ya Tanzania...

uongo wenu pelekeni fb kama mngekuwa makini mngeshamkamata
 
Back
Top Bottom