Polisi wampotezea mzee wa 900 itapendeza 'dk shika'

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
80,710
93,456
by Malunde 14 hrs ago




dr-shika.jpg
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu yaDar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kesi ya Dk Louis Shika hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba tatu za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo.
Novemba 9, 2017 kampuni ya udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko Mbweni JKT na moja Upanga jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika alifikia bei ya kuzinunua kwa Sh3.2 bilioni.
Mambosasa akizungumza leo Jumatano, amesema kesi yake haina mashiko hivyo hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba hizo zipo na hajatia hasara .
Amesema Dk Shika alikuwa akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezo wake ni mdogo na kusababisha kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba hizo.
‘‘Dk Shika ni wa kumuonea huruma hana kitu tulisema tunamchunguza na tutampeleka mahakamani lakini tumeona kesi yake haina mashiko ndiyo maana hatuendelei nayo,” amesema Mambosasa.
Jeshi la polisi kanda hiyo lilimshikilia na kumwachia kwa dhamana Dk Shika ambaye alikuwa akituhumiwa kwa kuharibu mnada baada ya kushindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo ambapo nyumba za Mbweni JKT alifika bei kwa Sh900 milioni na nyingine Sh1.1 bilioni, huku ya Upanga alifika bei ya Sh1.2 bilioni
Chanzo- Malunde blog
 
Polisi wa Tanzania ni hatariii kweli kweli huyu mambosasa anazid kuleta ujuaj hivi Siku shika akipata hela na akimwomba awe anamfulia chup na pampas kwa milion 6 kwa wiki si litaacha kazi
 
ngoja na mie nikavuruge ule mnada wa magari pale Bandar salama kumbe hamna kesi
 
Back
Top Bottom