Polisi wamnasa muuguzi kwa wizi wa dawa za Serikali mkoani Kigoma

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia wakazi wawili wa kijiji cha Kaguruka kata ya Rungwe Mpya wilayani Kasulu akiwemo muuguzi wa zahanati ya kijiji hicho wakituhumiwa kuiba dawa za serikali zilizoletwa katika zahanati hiyo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi FERDINAND MTUI amesema watu hao ambao majina yao yamehifadhi , walishtukiwa na wananchi baada ya muuguzi huyo kuiba na kumkabidhi mwananchi mwingine kwa lengo la kuficha.

Hata hivyo wananchi walibaini wizi huo na kuanza kuwashambulia mpaka viongozi wa kijiji walipofika na kuwafungia watuhumiwa ofisi ya kijiji ili kunusuru maisha yao.

Kamanda MTUI amesema watuhumiwa hao walikuwa wameiba dawa za aina mbalimbali za binadamu na vipimo vya malaria ambavyo thamani yake haijafahamika na kwamba watafikishwa mahakamani.
 
Hivi ndo wananchi tunatakiwa kuwa, tuwe na uchungu na vitu vyetu, zile dawa si za serikali ni Zetu sisi, ila tu tusichukue hatua mikononi ni kuwadhibiti kama hivyo kwa kuwafungia n.k..Safi sana Wanakijiji, tukiendelea hivi tutafika mbali, tusaidiane na Serikali katika kukomesha uhalifu.
 
Back
Top Bottom