Polisi wamkamata mbunge wa CUF na pia wawapiga risasi watu watatu

Aiseeee, hawa washika bunduki wa JK wameona kuua raia imekuwa fasheni!!! Za mwizi ni arobaini nao siku zao zitatimia tu.
 
Mkuu sana Pompo hali haijafika hapo...Ndio raia nao wanaweza kujibu mapigo lakini kuna swali dogo tu la kujiuliza hapa,kwamba baada ya yote haya nani anafaidi...my take ni kwamba umasikini tulionao wa kipato usitupore na uwezo wetu wa akili...natamani kuona Tanzania yangu ya kale ambayo mshikamano na umoja ndiyo ilikua kauli mbiu!
 
Kwa vile waliouawa ni majambazi, basi serikari ifuate utaratibu wake wa kawaida;
Kuchonga majeneza kwa ajili ya miili ya majambazi hayo, na pia rambirambi ya Tshs 3,000,000/- kwa kila jambazi lililouawa.
Kama tu Nyamongo! bila kusahau kumfungulia huyo mbunge kesi ya uchochezi. Na pia wasisahau kuwaonya viongozi wa vyama vya upinzani kwamba hawaruhusiwi kuhudhuria na kushiriki maziko ya hao majambazi.

Umenichekesha sana, hivi mkulu anayaona haya au yuko nje kwenye ziara? Kumbukeni pia kuna Okampo.
 
duh Binafsi siungi mkono polisi kupiga risasi na kuua hii ni Extrajudicial killings la wabunge kukamatwa nali ni jambo ambalo halina tija bali lin ongeza chuki ya raia kwa polisi na serikali yao maana wabunge hao (wanaokamatwa) mara zote wanakuwa wakishughulikia matatizo ya jamii yanayo sababishwa na utendaji mbovu wa vyombo vya dola au utendaji wa mazoea si wa kifuata sheria. IJP kazi anayo maana watu wake sasa wamekuwa Jeshi lapolisi la CCM sijui naye yumo au ...........
 
acha wapigwe risasi, mikutano na maandamano isiyo na maana.
Omr ikiwa hivi ndio uoni wako nina shaka nawe, mbona UVCCM Arusha hawajaguswa ? hivi wao ni nani na hawa wanaouliwa, kuuawa na kushikwa si binaadamu? Tafakari, Chukua hatua.
 
Jee, kukamatwa kwa huyo mbunge kuna uhusiano wowote na hao waliopigwa risasi?

Jee, una uhakika upi kuwa hao waliopigwa risasi si majambazi?
FaizaFoxy usikurupuke kupost tu soma thread kwanza na inaonyesha hufuatilii vyombo vya habari.
Na kama majambazi wapigwe risasi je ile mijizi ya EPA umeiweka fungu gani sio majmbazi wale? waliorudisha, walio kwisha hukumiwa, wenye kesi na wanaohisiwa tuwauwe?
 
hii ni mipango ya mungu kUwaonesha hawa wake wa Magamba aka CUF kuwa wanachofanya CDM ni sahihi na wanatafuta justice na sio popularity kama magamba wanavyobeza.
Pipozzzzzzzzzzz....Powaaaaaaaa
 
Ule mtindo wa polisi wa kuwakamata wabunge na kuwapiga raia umeendelea huko wilayani Urambo mkoani Tabora. Polisi wanadaiwa kuwapiga risasi raia 3, mmoja kajeruhiwa mgongoni, mwingine mkononi na watatu mguuni.

Pia polisi wamemkamata mbunge wa viti maalamu kupitia chama cha CUF mheshimiwa Magdalena Sakaya. Polisi wamesema wamemkamata mbunge huyo kwa kufanya mkutano bila kibali.

Source. Wapo Radio kipindi cha pata pata leo asubuhi.

Ndugu watanzania wenzangu, hivi hii tabia ya polisi kupiga risasi raia wasio na hatia itaisha lini? Wananchi inatubidi tuikemee kwani ndugu zetu wanaumizwa na kuendelea kufa bila hatia.

Hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Asiyependa Haki.
 
Channel Ten wameonyesha tukio hilo saa moja kwenye taarifa nyumba nzima tumeangua kilio polisi ameua wakamuacha huyo kijana anavuja damu bila mssada kijana mwinhine akawa anajaribu kumuinua akaonekana hawezi mgongoni kote kijana anavuja damu kama chemichemi,halafu polisi alikuwa anapiga risasi mfululizo kama yuko vitani sijawahi kuona polisi kuingia vitani na raia ambao hawakuwa na silaha huku wakikimbia ovyo.

Rais Jakaya kama haoni kwamba Jeshi lake la Polisi limeasi basi angejee maafa mengine, nasikia hata kura polisi walimnyima
haya mambo tuliyasikia na kuona video za polisi wa makaburu nyakati zile za makaburu
 
yaweza kuwa hiyo mikanda ya mauaji, wakuu wanaitumia kujiburudisha na jamaa zao kama alivyokuwa akifanya Idi Amini yule nduli wa Uganda, si tumeshuhudia wakilipia mauaji hayo?
 
Jee, kukamatwa kwa huyo mbunge kuna uhusiano wowote na hao waliopigwa risasi?

Jee, una uhakika upi kuwa hao waliopigwa risasi si majambazi?

Faiza=gain, mi nataka kukuoa, serious; kwani napenda sana majibu ya ujuba kama haya nadhani nitaenjoy sana ndoa yangu huku nikikuzidane siku moja-moja!
 
Kwani CUF si ni CHAMA TAWALA inakuwaje mbunge wao akamatwe. Wao si kila siku wanakipiga vijembe CDM kwa maandamano. Sasa nao wanasema wanataka kuandamana, nilimsikia jana Mtatiro anasema wanataka kuandamana kupinga unyanyasaji wa polisi!!!!! Sasa hawa polisi wanawanyanyasa hata watawala!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:hatari::hatari::hatari::hatari::hatari:
 
By In2EastAfrica - Mon May 30, 2:09 pm

Magdalena-Sakaya.jpg
Magdalena Sakaya


Police in Tabora Region have arrested the Civic United Front (CUF) Special Seat MP Magdalena Sakaya, six other party leaders and five residents of Urambo District for allegedly inciting chaos.

The Tabora Regional Police Commander, Mr Liberatus Barlow, told the ‘Daily News' over the phone on Sunday that the 12 suspects would appear before the court on Monday to answer charges of illegal assembly and chaos incitation.

Mr Barlow explained that the MP had gone to Usinge Ward with other party leaders in the wake of a four-day special operation to stop illegal activities in the Mpanda Line Forest Reserve. While in Usinge, the suspects allegedly incited chaos.

"In the operation, we confiscated 820 cows, 1,780 fish, 178 timbers, 14 logs, five wooden doors and two bicycles out of which 100 cows were taken by their owners after they had paid the fine. The remaining 720 cows remain in police custody," he said.

Mr Barlow added that on Friday, the Shela Village Chairman (CUF) mobilized residents to resist against police action. He also allegedly led them to where the cows were kept in a forceful attempt to take them. He was arrested together with five others before doing that. They were charged on the same day.

"Ms Sakaya and company went to the area without our knowledge, held a rally and when we went to see what was going on, angry residents stoned a police vehicle while one of them, Saidi Juma, jumped on a police's back causing accidental gunfire where he was killed and a policeman injured," he said.

The RPC noted that following the incident, the MP and other six CUF officials were arrested plus five other residents.

Earlier on Sunday, the CUF Deputy Secretary General (Mainland), Mr Julius Mtatiro, admitted that the arrested MP and six other officials were sent by the party to witness the situation and, if possible, assist the victims.

"We got information that our village chairman had been arrested after he questioned the police move; we contacted the police but they showed no cooperation. We, therefore, decided to send a delegation of party leaders to witness what was going on," he claimed.

Mr Mtatiro named other leaders who have been arrested as Doyo Hassan Doyo, Zainabu Nyumba, Yasin Mrotwa and Masoud Omari, all executive committee members.

Others include the contestant for parliamentary seat in the last year's general elections in Urambo West Constituency on CUF ticket, Kirungi Kirungi, and the party's human right officer, Hashim Bakari.
By ABDULWAKIL SAIBOKO, Tanzania Daily News
 
Back
Top Bottom