Polisi wamkamata Lwakatare, apelekwa kwa mahojiano Makao Makuu

polisi jinga sana,kwahyo matukio yote na watu wote wanawaacha RZ1,Rama,Membe n.k wanaona waanze kwa CDM? filthy police!
 
Kumbe mbinu yao eti ya kutimua makanishna,mara wale wa 150m ilianzishwa ili waishie kwa hili eti wameamka,Vip Rama?
 
Nasema hivyo kwa sababu ni muda sasa tangu mwigulu autangazie ulimwengu kuwa ana cd inayoonyesha viongozi wa chadema wakipanga mauwaji ya baadhi ya watanzania.Wengi waliandika huku jf wakiwataka viongozi wa chadema wamshitaki huyu mtu ili ukweli udhihirike lakini chadema hawakufanya hivyo pia wengi wameandika humu jf ikiwa ni pamoja na mimi kuwa police walifanyie hili jambo uchunguzi isijekuwa ni kweli chadema wana mpango huo au isijekuwa mwigulu ana mpango wake anaotaka kuuhusisha na viongozi wa chadema hadi leo hakuna aliehojiwa wala uchunguzi uliofanywa wala kiongozi wa chadema aliefikisha swala hili mahakamani. Wote mmezembea hadi lile lililokusudiwa likawa tayari yaani mwigulu amemaliza kuiandaa video yake aliyokuwa anatengeneza ili kuwadhalilisha viongozi wa chadema sasa kwa haya yanayoonyeswa kwenye utub humu jf sijui mtawaelezaje wale wananchi ambao hawajui teknolojia ya kuwa mtu anaweza kuchukua picha ya mtu na kuiwekea maneno na ikaonekana ni huyo mtu anatamka hayo maneno sijui itakuwaje.:bounce:
 
chama cha mabwepande?hata mtoto mdogo anweza ku connect hii!mbona baba Ritz anaachia watu waidhalilishe utawala wake?
 
Kuna movie inaitwa A man called God kama umepata nafasi ya kuitazama Kuna michezo humo unarekodiwa katika mazungumzo ya kawaida bila kujijua wanamaliza wanaiedit na kuiwekea sauti nyingine kama umeongea wewe. ila kwa ubovu wa jeshi letu hawawezi gundua ila kwa wataalamu wa Graphics wanaelewa. mi sidanganyiki kwa video iliyoeditiwa china.
 
Watanzania mimi kila siku nawasihi siasa zetu ziwe za kuheshimu utu wa mtu. Tusichochee wala kuanzisha vurugu kwa namna yeyote ile. Kama mageuzi yatakuja tu wakati ukifika kadri watu watakavyoelimika na kuzijua haki zao.
 
Wana JF,

Wilfred Lwakatare ameitwa Makao Makuu ya Polisi sasa hivi kwa mahojiano na jeshi hilo kufuatia video clip iliyowekwa mitandaoni jana.

Kwa taarifa ni kuwa atawakilishwa na wakili Nyaronyo Kicheere na baadaye kama watafungua kesi watakuwa na Mabere Marando.

Je, hii sio double standard ndani ya taifa?

Mbona Mwigulu hajakamatwa baada ya kusema ana mkanda wa njama za kufanya mauaji?

atakamatwaje mwigulu wakati mhusika amepatikana? au hata masuala ya kiusalama unataka yaingizwe siasa
 
nimeiona hiyo video clip...mbona hakuna ushahidi na imerekodiwa kwa simu ya mkononi pia huyo lwakatare ni wa plastic surgery hata sau yake sio hiyo ...ana imitate ila ni uchunguzi wa kisayansi utakao waumbua hao police...swala la sound-matching litawamwagaje....na wanasema wanayo clip 4 inakuja....warudi upya studio wakatengeneze picha mpya hii wataalamu tushaistukia.
 
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda, I can see nguvu ya MUNGU inataka akujidhiirisha ... sitaki kumtetea Lwakatare but CCM na serikali inatakiwa ijiangalie kwa makini zaidi coz, kila propaganda na conspiracy zote wanazoziandaa na kuzitekeleza dhini ya ''wenye-nchi' inaishia kuumbuka yenyewe! Wahenga walisema 'Sikio la kufa, ........', ni vema kwa kipindi hiki cha mwisho wakaanza kutubu na kujisafisha coz wengi hatutakubali waondoke kilaini ... ni vema kama wataongeza nguvu kwenye kutekeleza ahadi nyingi walizotoa kwa wananchi waliowapa kura!

Thanks GOD kura yangu ilienda upinzani, so haya mateso na machungu ya muda ni halali kwangu coz muda wa ukombozi utafika na MUNGU atatulipia kisasi chetu.........
 
Huko mahakamani kama watamfikisha ndipo watakapoumbuka. Hii sinema wanayotaka kuicheza wasifikiri kwamba watu wamelala.
Walijitutumua kutengeneza filamu ya kichina kwa Jerry Muro wakaishia kuumbuka, sasa naona wanataka tena kuumbuka.

Ww ile ya jeri muro ni story ndefu pale serikali aikukurupuka jua hivyo ila hii ya hii clip ya video ndo atujajua chochote
 
Sina shida na kuhijiwa Lwakatare. Siku hizi katika ulimwengu wa IT unaweza kutengeneza picha yoyote na kuiwekea maneno hadi ionekane kuwa ni halisi. Kinachonishangaza ni watu kama Rama Ighondu waliotajwa na Ulimboka kuwa hawajaitwa Polisi na kuna kichaa Mkenya anasota rumande. Michael Kamuhanda alitetoa amri ya "Shoot" wala hakuhojiwa, askari aliyetii amri hiyo halali ndiye anasota. Hii haikubliki.
its true - watu wengi hawajui IT inaweza kufanya mambo yapi; tunatumia just 3% ya matumizi ya IT katika nchi hii. so kutengeneza video clip na kuiwekea maneno ni technologia ya zamani ambayo vijana watundu katika nchi zilizoendelea hutumia , leo kwetu tanzania ni kitu kipya mno na watu wote tunahaha eti Lwakatare anaweza kufanya hivyo kwa manufaa ya nani na kwa nini?
 
nenda youtube andika neno Bukoba boy au hapa JF fungua thred inayosema CHADEMA hapa Lwakatare alikuwa ana maanisha nini????
kwa kipindi cha miaka miwili mitatu sasa kumekuwa na matukio ya kinyama na ya uvunjaji haki za binadamu dhidi ya watanzania wachache wenye moyo wa uzalendo wa kuleta haki na usawa kwa jamii ya kitanzania iliyonyanyasika kwa kipindi kirefu.

Hivi majuzi Absalom kibanda mwenyekiti wa jukwaa la wahariri ameteswa na kufanyiwa unyama wa hali ya juu huku jamii ikibaki na maswali yasiyokuwa na majibu.

Aliteswa mpiganaji DR ULIMBOKA wakati yupo kwenye harakati za kuitetea sekta ya afya hapa nchini.

kijana ISSAH alimwagiwa tindikali huko igunga huku kukitokea mauaji ya kusikitisha ya mwandishi DAUDI MWANGOSI mkoani iringa na mwananchi asiye na hatia huko morogoro.

Watu wenye uchungu na nchi yao wamechoka wameona sasa basi..

Tukio la KIBANDA ni mwendelezo wa matukio yanayofuata.. Hivi karibuni mtasikia tukio lingine kubwa dhidi ya mwandishi mwandamizi wa mwananchi communications Ltd......sikiliza video.

Huyu anayeongea ni mchora dili mkuu kwa maelekezo ya mwenyekiti na katibu wake mkuu.

Hii ni part 4, part zingine zimekwisha tekelezwa Ila ZITAWEKWA HAPA WAKATI MAHSUSI UKIFIKA......
 
Ilitakiwa police waifanyie kazi hawajafanya na hawatafanya. CHADEMA sijawaona kwenye hiyo video, kwa radio mbao imewagharimu CCM 80 million tengeneza huo upuuzi.

Kwa nini polisi wanatakiwa waifanyie kazi ni kwa sababu kwa kuiangalia tu kuna "frame" vipande vya picha vinajirudia vinahitaji kuthibitisha. Kwa ubora wa picha ilivyo maneno lazima yangekuwa yanasikika vizuri zaidi. Kwa hiyo pamoja na kuiweka youtube kwa nini wasingeipeleka kwenye vyombo vya dola?

Mimi kwa matukio haya naona wenye mchezo huu mchafu wanajitafutia maafa
 
Na yule aliyehamasisha mapadri na maaskofu wauwawe naye kafikishwa police????
 
JamiiForums
VIDEO: Mikakati ya CHADEMA kufanya Mauaji kwa Wanahabari

- Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Willfred Lwakatare akitoa maelekezo kwa vijana wake kwenda kutekeleza tukio la kumteka mwandishi wa habari
- CHADEMA wanatakiwa kutufafanulia watanzania, hii ni mikakati yao au wanachafuliwa?
- Serikali na vyombo vya Usalama watuambie watanzania, kwanini watu hawa bado hawajachukuliwa hatua?
...See More
VIDEO: Mikakati ya CHADEMA kufanya Mauaji kwa Wanahabari - Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Willfred Lwakatare akitoa maelekezo kwa vijana wake kwenda kutekeleza tukio la kumteka mwandishi wa habari - CHADEMA wanatakiwa kutufafanulia watanzania, hii ni mikakati yao au wanachafuliwa? - Serikali na vyombo vya Usalama watuambie watanzania, kwanini watu hawa bado hawajachukuliwa hatua? - Kama video hii ni fake, mhusika (Lwakatare) anafahamu nani aliandaa video hii, awape ushirikiano polisi kumtia nguvuni mwandaaji kwa uchochezi! Tazama Video hii hapa --> CHADEMA, hapa Lwakatare alikuwa anamaanisha nini?
 
Mkuu kwa hiyo wewe ulikuwa unategemea kwamba Lwakatare asikamatwe kwa hiyo clip inayotisha namna hiyo? Wacha wamhoji ukweli ujulikane tu
Waswahili mna akili iliyochanganyika na Mchuzi.
Lwakatare ameitwa Central kwa mahojiano, nyie mnasema amekamatwa.
 
nenda youtube andika neno bukoba boy au hapa jf fungua thred inayosema chadema hapa lwakatare alikuwa ana maanisha nini????
kwa kipindi cha miaka miwili mitatu sasa kumekuwa na matukio ya kinyama na ya uvunjaji haki za binadamu dhidi ya watanzania wachache wenye moyo wa uzalendo wa kuleta haki na usawa kwa jamii ya kitanzania iliyonyanyasika kwa kipindi kirefu.

Hivi majuzi Absalom kibanda mwenyekiti wa jukwaa la wahariri ameteswa na kufanyiwa unyama wa hali ya juu huku jamii ikibaki na maswali yasiyokuwa na majibu.

Aliteswa mpiganaji DR ULIMBOKA wakati yupo kwenye harakati za kuitetea sekta ya afya hapa nchini.

kijana ISSAH alimwagiwa tindikali huko igunga huku kukitokea mauaji ya kusikitisha ya mwandishi DAUDI MWANGOSI mkoani iringa na mwananchi asiye na hatia huko morogoro.

Watu wenye uchungu na nchi yao wamechoka wameona sasa basi..

Tukio la KIBANDA ni mwendelezo wa matukio yanayofuata.. Hivi karibuni mtasikia tukio lingine kubwa dhidi ya mwandishi mwandamizi wa mwananchi communications Ltd......sikiliza video.

Huyu anayeongea ni mchora dili mkuu kwa maelekezo ya mwenyekiti na katibu wake mkuu.

Hii ni part 4, part zingine zimekwisha tekelezwa Ila ZITAWEKWA HAPA WAKATI MAHSUSI UKIFIKA......

Mzee naona umelivalia njuga mbona usiwaambie wenye dola waende youtube au wakabidhi kabisa hizo video ili wazifanyie kazi.

Kwa uelewa wangu wewe na wenzio mna misadventure na mna kila aina ya umasalia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom