Polisi wameweka kambi Ilala Sokoni, wanashusha abiria wasio na barakoa na kuwacharaza bakora

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,798
Niko Ndani ya daladala, natokea Tabata kwenda Mnazi Mmoja.

Gari yetu ilipofika Amana, tukatahadharishwa kila mtu avae barakoa, mbele Kuna FFU wanatembeza kipondo.

Hatukuamini. Tulipofika Ilala Sokoni/ Bomani, tukakuta jamaa wamejipanga, wanaingia kwenye basi, Kama huna barakoa unashushwa, unachapwa na kuchuchumalishwa chini, nadhani wanasubiri gari kubwa zaidi lije kuwasomba.

Naona huu ni mpango wa Kaka Mwenye Ofisi Yake Hapo Bomani
 
watoe bure, unajua watu wengi tutakufa kwa serikali kushindwa kutoa miongozo yenye uhakika kwa watu wake.
sasa watu wanavaa barakoa za vitenge zinazozuia vumbi tu zile maalum hazinunuliwi tena.
 
Back
Top Bottom