Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 121,947
- 95,237
Jana kwenye taarifa ya habari polis wamekanusha kuwepo kwa tuhuma za kuhuhumu njia ya reli katika mkia wa Kilimanjaro.
Hili jambo linakuwa tofauti na kile alichodai DC Sabaya kuwa ana uhakika wafanya biashara wa mabasi wamehujumu miundo mbinu ya reli kwa makusudi.
Jamani tunaomba viongozi wetu wawe makini kabla ya kutoa matamshi na tuhuma zao kwa wanachi kwani inaleta sintofahamu kwenye jamii inayo tuzunguka.
====
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema hakuna hujuma wala uharibufu wa miundombinu ya Reli katika eneo la Kijiji cha Rundugai Wilayani Hai kama zilivyoelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya .
January 19 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiwa katika Kijiji cha Rundugai akikagua ukarabati wa Reli alitoa agizo la kukamatwa kwa wafanyabiashara wawili wa mabasi kwa tuhuma za kuunda genge la uharifu ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar,Moshi hadi Arusha.
Sent using Jamii Forums mobile app