Siku zote tunaambiwa usalama ni jukumu la kila mwananchi na hivi karibuni tumeambiwa jeshi linafanya mabadiliko makubwa baada ya kujitathimini na kuona sura ya jeshi hilo kwa jamii imeharibika kiasi cha kukosa ushirikiano toka kwa jamii. Jana wakati wakiwajibu Bavicha wakasema HAWAITAJI MSAADA WA MTU YOYOTE katika kuhakikisha usalama wa nchi na kama watahitaji msaada kwa VYOMBO VINGINE vyenye mafunzo na ueledi wa kufanya kazi hiyo!
Sasa tuchukue lipi? Au ndo kusema wamechanganywa na mkakati wa Bavicha? Walizuia mikutano leo wanasema wanakuja na majibu mengi! Mara hatukuzuia mikutano ya kikanuni na kikatiba! Mara tupewe ushirikiano na usalama ni jukumu la kila raia, baadae hatutaki msaada wa mtu yoyote! TUCHUKUE LIPI?