Polisi wameisaliti nchi, jeshi livunjwe haraka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wameisaliti nchi, jeshi livunjwe haraka.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimilidzo, Jan 9, 2011.

 1. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kitendo cha Askari polisi wa Arusha Tanganyika kuwafyatulia risasi na kuwaua waTanganyika wenzao pale Arusha kwa amri ya Mzanzibari Shamsi Vuai Nahodha ni usaliti wa hali ya juu. Inasikitisha kuona kuwa Said Mwema anapokea amri kutoka kwa raia wa nchi nyingine ya kuwaua waTanganyika wenzie kwa risasi naye anakubali kutekeleza amri hiyo. Wenyewe kule nchini kwao Zanzibar walishauana sana na wengine wakakimbilia kupunga upepo kwenye beach ya kule Mombasa Kenya lakini hawakutaka hata kuulizia namba za simu au email adress ya Louis Moreno Ocampo na wakaishia kuwasaliti wale marehemu 60 waliouwawa kwa kuoana CUF na CCM. Sasa huyu mzanzibari baada ya kutumia usaliti na udhaifu wa askari wetu huku Tanganyika anataka kutuingiza katika usaliti mwingine tukae mezane na kusahau roho za watu wetu watatu waliouwawa katika Civil conflict ya Watanganyika kwa Watanganyika halafu yeye achukue cheap popularity kuwa aliwahi kuwasuluhisha waTanganyika, kama alivyofanya Mkwere JK alivyovamia mazungumzo ya Kenya baada ya Mkapa kufanya kazi kubwa na kwa ubinafsi kajifanya yeye ndio alipatanisha. Wakati tukielekea kutimiza Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika huku tukiwakumbuka mashujaa wetu kama Mzee Nyirenda waliouweka Mwenge juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro, hatutakiwi kuwa na jeshi ambalo limewasaliti waTanganyika kwa kupokea amri ya mtu wa nje. Watanganyika wote tunatakiwa tusimame Imara na kulivunja jeshi hili na kuunda jeshi jipya la polisi wazalendo na watakaokuwa tayari kulinda haki za waTanganyika wenzao na kuitetea nchi yao katika hali yoyote. Pia askari polisi wachache mlio wanachama wa JF tumieni fursa ya hili jamvi kuwaomba msamaha waTanganyika wenzenu ktk hili jamvi wakati tunaangalia mchakato wa kuunda jeshi jipya. Mmeshindwa kupambana na majambazi na mmekuwa mkishirikiana nao, lakini mmekataa kushirikiana na CDM katika maandamano ya amani. Kwenu ni bora kushirikiana na majambazi kuliko wakombozi wa Taifa lenu. Usaliti huu wa Polisi wa Tanganyika hauvumiliki, wale wote waliofyatua risasi kwa waTnaganyika wasio na hatia wajisalimishe wenyewe ili waungane na Mwema, Mkwere, Nahodha (of a sinking ship) na Mkuchika katika karandinga kuelekea The Hague.
   
Loading...