Polisi wamefanya makosa makubwa ZANZIBAR - Kushtakiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wamefanya makosa makubwa ZANZIBAR - Kushtakiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jul 21, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Polisi wamefanya makosa makubwa sana na huenda wakashitakiwa katika vyombo vya ndani au vya kimataifa ,hakuna sababu ambayo wanaweza kusema ikakubalika, hakukuwa na fujo wala mikusanyiko wanayoidai.
  Mkusanyiko ulikuwepo na hata baadhi ya viongozi walikuwepo hapo ni mkusanyiko wa kuwaombea wale waliokumbwa na kuzama na meli .wakiwemo waliopotea,waliopoteza maisha na waliopona.

  Ni jambo gani lililowafanya polisi kwenda kupiga mabomu na wao ndio waliosababisha fujo kama lile fujo liliopita ,chanzo ni polisi.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwiba, poleni sana!. Kama unadhani polisi watashitakiwa utakuwa unajidanganya!.

  Yale maandamano ambayo mlimiminiwa risasi za moto na watu zaidi ya 40 wakailiwa, nani alishitakiwa?!.

  Mwembechai waliingia na buti mpaka msikitini na kuinajis kibla, nani alishitakiwa?!.

  Maandamano ya Chadema Arusha, waliwafyatulia risasi na kuua watu wawili mmoja Staendi Kuu na mwingine Unga Ltd, wakasingizia walitaka kuvamia kituo kikuu cha polisi!, wamechukuliwa hatua gani?!.

  Jana nyie mmelizwa tuu kwa vibomu vya machozi ndio washitakiwe?!. Washitakiwe kwa lipi ili hali walikuwa wanaulinda muungano!.

  Kama matumaini yako ni Maalim Seif kufanya lolote ndani ya ndoa yenu na CCM kwa jina la SUK, endelea kusubiria, wana ndoa wa ukweli wamekula yamini ya " collective resiponsibilities" ndio maana yuko kimya kama maji mtungini!.
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kosa kubwa uamsho mmefanya ni kuchoma makanisa na vitabu vitakatifu vya Mungu, Mbona hamkushitakiwa kwani ninyi uamsho mnathamani gani ya kuogopwa hata msipigwe marungu na mabomu kutokana na tabia zenu za kuto Mjua Mungu? na kuthamini Imani za wengine? Mtenda maovu adhabu yake kwanza huanza kuipata hapa hapa,
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,803
  Likes Received: 2,576
  Trophy Points: 280
  Tanzania police ni ATL: Above The Law.
   
 5. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Una uhakika ni uwamsho ? Tupatie ushahidi ,au na wewe wafata redio mbao ?>
   
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  UAMSHO ni KUNDI la KIGAIDI linatakiwa lisipewe nafasi ya kupumua kabisa, na hata wanaoshabikia ni wa HALIFU wanaopaswa kudhibitiwa vilivyo, Hawa wenzetu wanaiga hata mabo ya kijinga na ya Hatari sana coz wana ufukara mkubwa mno wa kufikiri tizama Makundi yote ya KIGAIDI DUNIANI yamewakuta na wameyapokea na sasa wanauana wenyewe kwa wenyewe.Hebu ona Nigeria wanachoma makanisa na wakristo, angalia wameiga sasa kenya Majuzi wamepiga mabomu makanisa, znz nako the same, angalia kenya Wameanza Mombasa kutaka iwe Jamuhuri eti wajitenge, znz wanaiga na Bara watafuata na ukiwaona karibu wana waza sawa 2 CHUKI na wengine, popote walipo hata wakiwa wenyewe nivivo hivo.
   
 7. mchongameno

  mchongameno Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza lazima tujiulize hao watu waliopigwa mabomu walikuwa eneo gani? Pili walikuwa wanahatarisha maisha ya wengine au kufanya jambo lolote linalohatarisha usalama wa nchi? Hapo walipokusanyika lengo lao hasa lilikuwa ni lipi? Chanzo cha mkusanyiko wao ni nini? Tutakapopata majibu ya maswali haya tunaweza kujadili kwa undani zaidi uhalali au uharamu wa kukusanyika eneo husika.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unajua kama Kenya kuna kesi inaendelea ? Nani aliwashitaki ? Hivyo Zanzibar kuna kesi ya mauaji ya Mkapa ,huyu tunae labda afe ,Ila akae akijua tu yanayotokea hapo Kenya yatatokea Tanzania .

  Hili halina mjadala na hawa wanaochokoa chokoa kama wanatafuta chaza basi wasitie wasiwasi ,kila kitu kinarekodiwa na wakuu hawa wapolisi wa vituo majina yao yanarikodiwa kwa wakati fujo au mauaji au upigaji unapoanza na eneo lake kwa tarehe na saa ukijumlisha wanaojeruhiwa . Si lazima makosa haya yashitakiwe wakati huu wa utawala wa dhulma ,siku utawala wa haki utakapodhihiri basi majina ya wakuu wa vituo vya polisi yatakapofikishwa mahakamani.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi binafsi sikupendezewa na maamuzi hayo na nilishalaani tangu kitambo!
   
 10. Mwl Mkwaya

  Mwl Mkwaya Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Bob G na Pascal......Heshima kwenu,
  Huwezi kusema Muungano na dini na kuchoma kanisa.Wanaona Sirya na Libya wamepeta kwa kufanya vuguru wkt mpk sasa amani imepotea. Napenda sana watu wakifunguka na kusema ukweli juu ya hawa Uamsho, wanachokifanya upuuzi,meli kuzama mara ya pili naamini ni pigo la Mungu kwa kumchomea nyumba zake za Ibada(makanisa) japo wamekufa mchanganyiko lakini ni adhabu from our Lord Almighty God....


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio hata CHADEMA wameitwa magaidi ,unaona mwezi huu wengi wamepandishwa mahakamani ,endelea kushangilia kwa uamsho kuitwa magaidi.
   
 12. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakat ukifika muamsho tunatakiwa tujiandae ni kuwa na chupa za petrol tu. "arm in arm will fight little trouble" inatakiwa kama wanasema ni ugaidi ss ndio tuuoneshe.
   
 13. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mkuu,

  Arusha walipiga wakaua wakati maandamano yalikuwa ya amani kabisa. WaTZ wakakaa kimya na kuwaachia CDM wauguze maumivu yao. Wakadhalilisha wabunge wanawake, hata wanaharakati wakakaa kimya.

  Hii inanikumbusha makala ya Johnson Mbwambo katika gazeti la Raia Mwema wiki iliyopita alipoeleza alivyosema mchungaji mmoja wakati wa utawala wa ki-imla wa Dikteta Hitler nanukuu " Walikuja kuwafuata Wayahudi, sikusema kitu kwa kuwa mini siyo Myahudi; Wakaja kuwafuata viongozi wa wafanfakazi, sikusema kitu kwa kuwa mini siyo kiongozi wa wayfanyakazi; Wakaja tena kuwafuata Walemavu, sikusema kitu kwa kuwa mini siyo mlemavu; Walipokuja kunifuata, hakukuwa na aliyebaki kunisemea".

  Najua una kichwa cha kufikiria na sio nywele, endelea mwenyewe......................
   
 14. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  haiwezekani polisi kushakiwa nchi hii...muulize mkapa alipowamiminia risasi wale askari walishtakiwa??
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni kweli na ndio ukaona hawa polisi huwa hawajali si Znz hata huku Tanganyika ila one day yes ,utawala dhalim utakapoanguka basi ,wakuu wa vituo wajue ,nao watakuwa chini ya sheria,hapo ndio watajua kama muhogo si mzizi.
   
 16. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  hizi ndoto kila mtu kabla ya uhuru huwa anazo ila baada ya uhuru kila mtu hutaka kula matunda ya uhuru kwa urefu wa kamba yake...historia ya zenji iko wazi sana katika hili enzi za hayati karume na wapigania uhuru wenzie kama kina jenerali OKELO
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Usijifiche mgongoni kwa chadema ili uungwe mkono!!!!!! Wenyewe wanajiita "wanamuamsho"
  mungu hapiganiwi kwa silaha yoyote, mungu ni mmiliki wa hiyo inayoitwa "NGUVU" sio unatanguliza ndevu na kujidai unampigania mungu.
   
 18. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Ukiona unafuatwafuatwa sana na kupigwa na polisi hata km huna kosa ujuwe kuwa wewe ni muhalifu uliekubuhu.hivyo uhalifu wako umewafanya polisi kuamini kuwa mahali popote utakapo unekana uwe na nia nzuri au ovu wao wanajuwa kuwa kitendo unacho kifanya ni cha kihalifu tu.kwa sababu umejijengea msingi huo.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Pasco umesomeka mkuu..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Pasco umesomeka mkuu..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...