Polisi waliopiga Wananchi Ukonga, bado hawajapatikana eti!..

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
Polisi Kanda Maalum ya DSM, bado haijafanikiwa kuwakamata FFU waliohusika kuwapiga raia Ukonga, kwa kuwa waliotajwa hawajapatikana. Wameandika nipashe.

Shughuli nzito kuwanasa Polisi wadaiwa kupiga raia

Jana, Nipashe ilimhoji kwa njia ya simu na Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, ambaye alisema baada ya wananchi kuhojiwa walitaja askari saba kwa jina moja moja na kwamba hakuna aliyejitokeza kuonyesha askari aliyehusika kwenye tukio hilo.

“Bado ufuatiliaji unaendelea maana kuna utata kwa baadhi ya waliotajwa. Mwingine unakuta ametajwa lakini ukifuatilia unagundua kuwa alikuwa lindo benki usiku. Sasa inaonyesha wananchi hawakuwa na uhakika wa kile walichokisema na mmoja aliyekamatwa ametajwa na wananchi kuwa aliwasaidia katika uokoaji wakati wanashambuliwa,” alisema Mambosasa.

“Kumekuwa na shida kidogo ya utambuzi juu ya nani ambaye alifanya tukio hilo. Wangekuwa wanawataja hata kwa kuonyesha picha tungejua kama wale ni askari au mamluki,” aliongeza.

Kamanda Mambosasa pia alisema tukio hilo linapelelezwa na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kuna watu wamepelekwa kwa ajili ya kufuatilia, hivyo wanasubiri kupatiwa matokeo ya upelelezi huo.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kuwabaini waliohusika.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 21 mwaka huu baada ya wananchi wa Ukonga kulalamika kutembezewa vipigo na askari wa FFU ambao walikuwa wamekerwa na kuuawa kwa mwenzao.

Katika tukio hilo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limefungua jalada la uchunguzi ili kuwabaini akari waliohusika kwenye tukio hilo.

Askari hao wanadaiwa kupiga wananchi maeneo mbalimbali Ukonga jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwasaka watuhumiwa wa mauaji ya askari Charles Yanga, aliyekutwa nje ya geti la kambi ya FFU, Mkoa wa Kipolisi Ilala akiwa amekufa.

Kamanda Mambosasa alisema baada ya taarifa ya kifo hicho, askari polisi waliingia mtaani kuwasaka wahalifu na katika operesheni hiyo inadaiwa kuwa waliwajeruhi wananchi.



My take

Hii ndo hali halisi ya Jeshi la Polisi. Na ni mhimili wa Serikali unaofanya haya.

Tukio la Lissu: Takriban miezi miwili sasa hakuna mchoro wala hela ya tuzo!!
 
Polisi Kanda Maalum ya DSM, bado haijafanikiwa kuwakamata FFU waliohusika kuwapiga raia Ukonga, kwa kuwa waliotajwa hawajapatikana. Wameandika nipashe

My take

Hii ndo hali halisi ya Jeshi la Polisi. Na ni mhimili wa Serikali unaofanya haya.

Tukio la Lissu: Takriban miezi miwili sasa hakuna mchoro wala hela ya tuzo!!
Hao nipashe naona wanawashwawashwa wasipoandika mabaya ya polisi basi wataandika ya JW

Nawaambia wakafanye mambo mengine hii waachane nayo maana kuna mambo ya msingi yakuwahabarisha wananchi.

Kila siku ukonga mara dereva jw kakimbia gari ...

Haya hayawasaidii, wakiona maisha magumu waachane nayo wakafanye mengine
 
Hata wale walitaka kumuua kumuua Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu kwa kumpiga risasi zaidi 30 bado hawajapatikana. Kama bado kuna watu wana imani hawa Jeshi la Polisi niwape pole sana.
 
Polisi ilishasema waliopiga Raia ni wahuni wanaosadikiwa kuvaa sare za FFU
 
Kwahiyo mlitengemea wapatikane? wangepatikana endapo tu wangekuwa makada wa chadema
 
Back
Top Bottom