Polisi waliopewa kazi Maalumu Arumeru walalamikia malipo ya tshs 10,000 kwa siku

kinganola

Senior Member
Aug 16, 2011
117
30
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,polisi waliokuja wilayani Arumeru zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ta mkoa wa Arusha, wamemuandikia barua ya siri Dr Slaa na kumuomba awasemee tatizo lao la malipo kiduchu ya tshs 10,000 kwa siku.

Serikali imetumia gharama kubwa sana kuleta vifaa vya kijeshi na kusahau kuwalipa fedha stahiki watumiaji, kuna Diffender na Cruzer hardtop zaidi ya 40, Magari la majikuwasha 2 na lori moja la mabomu ya machozi.

Kitendo hiki kimewakera sana Polisi. Safari hii hata mkiwaamuru wapige mabomu itawawia vigumu sana maana wamekiri nawenyewe wamechoka na serikali kandamizi ya CCM...
 

Attachments

  • Arume.jpg
    Arume.jpg
    119.3 KB · Views: 105
  • Arumer2.jpg
    Arumer2.jpg
    27.5 KB · Views: 107
Hata wakilipwa milioni moja kwa siku, tunachotaka wasimamie haki tu.
 
Hii nchi ni ya ajabu sana!!!! Hivi kuna vita gani ambayo inasababisha serikali ipeleke askari wengi, mabomu na magari yote hayo? hayasio matumizi mabaya ya pesa za umma? Inatia kichefuchefu kweli.
 
Walishaambiwa na Nyerere kijana wa Musoma..kuwa wao wakiambiwa nyumas geuka wanageuka bila kujua kuna nini na wala hawaulizi lolote...kudadadek
 
Mwigamba alipoandika makala kwenye Tanzania daima akiwataka askari waache kutii amri zisizo halali, serikali ikamfungulia mashtaka na hao askari wakanyamaza kimya. Sasa wamepatwa na shida wanaanza kuomba chinichini wasaidiwe. Hivi ni lini wataamka na kudai haki zao? Sidhani kama kudai haki ni dhambi au kosa la jinai au utovu wa nidhamu. Hilo ndilo alilowaambia Mwigamba kwenye makala ambayo ameshatakiwa juu yake. Polisi waamke, waache ulofa
 
Walishaambiwa na Nyerere kijana wa Musoma..kuwa wao wakiambiwa nyumas geuka wanageuka bila kujua kuna nini na wala hawaulizi lolote...kudadadek
Yani wanageuka tu..........

halafu wakiambiwa nyuma geuka, mbele tembea wao wanatembea kuelekea nyuma........wanasahau mbele ni alipo kiongozi wao.!!!!!
 
Sio kila hoja lazima uchangie, zingine acha wachangie watu wenye pointi kuliko hizi pumba zako

Nimesema hakuna cha ajabu kwa sababu. Polisi weshajua kumbe CDM wana pesa ya kumwaga. Ikiwa housegirl wa katibu mkuu analipwa 280000 unadhani wao watalipwa ngapi?
 
Back
Top Bottom