Polisi waliomdhalilisha mchungaji wakufuzwa

enockino

JF-Expert Member
Oct 14, 2014
260
250
Askari polisi wanne mkoani Kilimanjaro waliotuhumiwa kutengeneza tukio la ushoga kwa mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT) wamefukuzwa kazi.

Polisi hao walidaiwa kumkamata mchungaji huyo na mwanaume mwingine katika nyumba ya kulala wageni wilayani Hai, kumshurutisha avue nguo, kumpiga picha na kudai awalipe shilingi milioni 10 .

Hata hivyo mchungaji huyo ambaye jina lake limehifadhiwa aliwalipa shilingi 5.4 milioni polisi hao kumuachia baada ya kumshikilia kwa masaa sita.

Source: Mwananchi
 

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,216
2,000
Hao askari wameanza kuvuna walichokipanda. Na wasipopata ufahamu wa kwenda kumuomba mchungaji msamaha, na kutubu mbele za Mungu; lazima watateseka na kutaabika maisha yao yote!
 

LebronWade

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,615
2,000
Hao askari wameanza kuvuna walichokipanda. Na wasipopata ufahamu wa kwenda kumuomba mchungaji msamaha, na kutubu mbele za Mungu; lazima watateseka na kutaabika maisha yao yote!
Hujajua,na wala hatujafahamu mkweli hasa ni nani...unatoa hukumu wewe kama nani?

Ukweli halisi kabisa beyond doubt huna.

Yanini kutoa final judgement?
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Ningependa ile adhabu ya NYERERE irudi.... Kwanza walipe faini kwa mhanga wa hilo tukio kisha wahukumiwe kwenda jela...."Wapigwe VIBOKO kumi na viwili wanapoingia na Kumi na mbili siku wanatoka wakawaoneshe wake zao"....Hiyo ni rushwa na uhaini, hiyo adhabu haiwatoshi kabisa...
 

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,216
2,000
Hujajua,na wala hatujafahamu mkweli hasa ni nani...unatoa hukumu wewe kama nani?

Ukweli halisi kabisa beyond doubt huna.

Yanini kutoa final judgement?
Kama wewe ni mmoja wao, nenda haraka kajisalimishe kwa nchungaji husika kwa kumwomba msamaha, kisha upige goti mbele za Mungu utubu

Maana naona unataka kutetea dhambi ya kubambikiza kesi.

Maana ya kufukuzwa kazi ni baada ya mahakama ya kijeshi (maktabu) kuendesha hilo shauri na kuwapata na hatia. Mtavuna mlichopanda!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom