Polisi wakiri kuongoza kuvunja Sheria za Usalama barabarani, Madereva wa Magari ya Serikali na Askari wa jeshi hilo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam imesema wanaongoza kuvunja Sheria za Usalama Barabarani ni madereva wanaoendesha magari ya Serikali wakiwamo askari wa jeshi hilo.

Kaimu Kamanda wa kanda hiyo, Lucas Mkondya alisema jana kwamba madereva hao wamekuwa wakivunja sheria hiyo kwa makusudi kwa kisingizio kuwa magari ya Serikali hayakamatwi.

Hata hivyo alisema madereva hao sasa watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu.

"Jeshi la Polisi halitavumilia mtu yeyote atakaye vunja Sheria ya Usalama Barabarani na wanaoongoza madereva wanaoendesha magari ya Serikali wakiwamo askari polisi ambao hawana kinga yoyote itakayowazuia wasikamatwe.

"Ninawaomba maaskari wa usalama barabarani wanapowaona madereva hao wamevunja sheria wawakamate ili wachukuliwe hatua za kisheria", alisema Mkondya.

Alisema jumla ya magari 13,712 yalikamatwa kwa makosa mbalimbali, pikipiki 749, daladala 5,701 huku makosa yaliyo kamatwa yakiwa 14,461 ambayo yaliingiza Shs 429,600,000 zilizotokana na tozo kuanzia Agosti 11 hadi 17.

Chanzo: Mwananchi
 
sheria ichukue mkondo wake... sio kubagua magari yanayofanya makosa..

pia hawa viongozi wetu wakiwa wanaendesha magari yao ni wababe sana... nilishuhudia mheshimiwa mmoja akimtishia na bastora dereva wa daladala kisa ni kosa la barabarani..
 
"Jeshi la Polisi halitavumilia mtu yeyote atakaye vunja Sheria ya Usalama Barabarani na wanaoongoza madereva wanaoendesha magari ya Serikali wakiwamo askari polisi ambao hawana kinga yoyote itakayowazuia wasikamatwe.


Very political statement
 
Back
Top Bottom