Polisi wakihakikisha Usalama wa katibu Mkuu wa CCM Taifa Bashiru Ally akiwa ziarani Mkoani Mtwara

Hebu waangalie hao vijana wanaomsindikiza vizuri, hiyo vaa yao inaashiria nini?? Yawezekana akatokea kichaa akampiga shaba, watasema walikuwa wapi?
Kwani huyo kichaa atakuwa alikuwa anamsubiri Bashiru tu? Kwani huko alikofanya ziara hakuna binadamu wengine wanaoweza kujeruhiwa na huyo kichaa? Mbwembwe zisizo na kichwa wala miguu.
 
Kwani huyo kichaa atakuwa alikuwa anamsubiri Bashiru tu? Kwani huko alikofanya ziara hakuna binadamu wengine wanaoweza kujeruhiwa na huyo kichaa? Mbwembwe zisizo na kichwa wala miguu.
Kwa onyesho ka hili hata kichaa atajiuliza mara mbili kama atathubutu kumsogelea
 
Wasalaam, hivi ni kweli jeshi la police mmepoteza weledi na kuamua kumtumikia kafiri? Mbona mnavunja katiba ya jamhuriya muungano ya Tanzania? Mmejipofua macho na kuamua kuwa vibaraka wa ccm huku mkilipwa kwa kodi za watanganyika.

Hakika mungu anawaona
 
Attachments

  • 2316672_uvccm.jpg
    2316672_uvccm.jpg
    20.8 KB · Views: 1
Hata nyie chadema mkichukua nchi mtapata Raha zote hizo hivo acheni wivu
 
2316889_FB_IMG_1582491848963.jpg

Pamoja na Ulinzi wa namna hii wa viongozi wa ccm lakini kumbe viongozi hawa wanaweza kudhurika ! wanaweza hata kupigwa vibao , kupigwa fimbo ama hata kupewa sumu kama Ilivyothibitishwa na RPC wa Dar es Salaam Lazaro Mambosasa.

Natoa wito kwa wanadamu kuacha kujivuna na kujimwambafai kwa sababu ya madaraka , mlinzi pekee na wa uhakika ni Mungu pekee , huyu hawezi kukubwaga wala kukutilia sumu .

Maandiko matakatifu yanaeleza kwamba AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU (YEREMIA 17 : 5)
 
Manabii,wachungaji na ma askofu wwmekuwa wengi sana

Kanisa lako linaitwaje?
 
Mbona hao hao wanaosema mlinzi ni Yesu pekee humo ndani unakuta wamesimamisha
mijitu ya milaba minne na mawani meusi kama majini! Usimsemee Mungu mwache atajisemea mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1382873

Pamoja na Ulinzi wa namna hii wa viongozi wa ccm lakini kumbe viongozi hawa wanaweza kudhurika ! wanaweza hata kupigwa vibao , kupigwa fimbo ama hata kupewa sumu kama Ilivyothibitishwa na RPC wa Dar es Salaam Lazaro Mambosasa.

Natoa wito kwa wanadamu kuacha kujivuna na kujimwambafai kwa sababu ya madaraka , mlinzi pekee na wa uhakika ni Mungu pekee , huyu hawezi kukubwaga wala kukutilia sumu .

Maandiko matakatifu yanaeleza kwamba AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU ( YEREMIA 17 : 5 )
Na pia imeandikwa Kama Bwana asipoulinda Mji waulindao wafanya kazi bure. Hakika mlinzi wa uhakika ni Mungu tu
 
Hilo ni gwaride au wanatuma ujumbe kwamba CCM ni chama cha kipolisi?

Halafu kinachofuata?

Kusimikwa kwa udikteta ama?

People don't need these stupid parades or whatever they call it.

Watu wanahitaji ajira, maji safi, makazi bora, usafiri, elimu ya uhakika na uchumi imara.

Zaidi ya yote, watu wanataka Katiba iheshimiwe na viongozi wawajibike na ikibidi wawajibishwe kupitia sanduku HURU la kura. FULL STOP.

Sio huu ujinga wa mabuti!
Bashiru alishajibu hii kauli yako.
 
Back
Top Bottom