Polisi wakatwa mishahara yao ni kuilipa DOWANS? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wakatwa mishahara yao ni kuilipa DOWANS?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by amba.nkya, Jan 28, 2011.

 1. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  WanaJF,
  Kuna taarifa za uhakika kabisa kuwa polisi wamekatwa 100,000/= kila mmoja kutoka kwenye mishahara yao ya mwezi huu ili serikali iweze kuilipa Dowans mabilioni ya shilingi.
  Ni jambo la kusikitisha sana kwa vile linawanyima haki yao polisi wetu hasa ikizingatiwa mishahara yao ni midogo na mazingira magumu ya kazi zao. Sijui ni kwanini wamekata mishahara ya polisi pekee na sio watumishi wengine wa umma kama JWTZ, mahakama, TRA, n.k, n.k...

  Tujadili............


  Source: Taarifa za ndani ya Polisi
  Magazeti ya leo
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu polisi akikatwa laki ina maana anabakiwa na elfu 40. Can that be possible?
   
 3. Pilato2006

  Pilato2006 Senior Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani, hivi DOWNS hawa wana kichwa kama cha Kamongo, wanajua kabisa wanadanganya, kumbe hata hukumu waliandikia pale MovenPick.Bill 100 hizo wakipewa tutaishije? Hawa jamaa hawana hata Hofu ya Mungu. Rais wetu wamemuweka pabaya kiasi cha kwamba sasa anajificha ficha.

  Inabidi tufanye kama kule Misri na Tunisia
   
 4. D

  Derimto JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wacha wakatwe wameshaonekana ni vibaraka wa kuwapiga watu ovyo na kulinda maslahi ya chama wengi hawana elimu na hivyo ili kujihakikishia uhakika wa kuendelea kula rushwa na kunyanyasa watu watakaa kimya tu mimi naona tunisia inakuja hapa siku siyo nyingi
   
 5. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Poti,
  Hali ndiyo hivyo, hawabakiwi na kitu ikizingatiwa wengine wanakatwa mikopo kwenye taasisi mbalimbali za fedha, wana hali mbaya sana polisi wetu, hawana la kufanya wao hulalamika chinichini tu...
   
 6. nyondoloja

  nyondoloja Senior Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  imeka vizuli hawawenzetu wanajifanya vipofu matatizoyote hawayaonio kwamara2 napendakuwakumbusha watumishi wa uma tendenihaki kujipendekezaupande 1 nakutuzurum hakizetu tuliowengi nirana wamewatumia mumemwagwa musipigekelele waramsibambikizie kesi wanyonge jee? Mkiandamana nani awapige na mabomu au kwasasa mtatuunga mkono wanyonge?
   
 7. The Good

  The Good Senior Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii haiwezi kuwa kweli. Nadhani hii habari ni calculated move kuwagonganisha hawa jamaa na serikali. kwani watumishi wa serikali ni Polisi tu? After all kuna maeneo mengi yanayoweza kuguswa amabyo hayana impact moja kwa moja kwa mtumishi na hizo hela zikapatikana (Kama wataamua kulipa fasta fasta anyway)
   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  lizabeth Ernest na Fidelis Butahe
  [​IMG]SERIKALI imeondoa posho ya upepelezi na nyumba kwa askari polisi bila maelezo katika mishahara ya miezi ya Desemba 2010 na Januari mwaka huu, Mwananchi limebaini.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa, posho hizo zitaendelea kukatwa kwani baadhi ya askari waliokwishapata mshahara wa Januari, wamesema fedha hizo hazipo.

  Baadhi ya askari polisi walilithibitishia Mwananchi kuhusu kukatwa kwa mishahara yao, huku taasisi husika za serikali ambazo ni polisi makao makuu na hazina, wakirushiana mpira kuhusu suala hilo.

  "Ni kweli tumekatwa posho zetu zote na tatizo hilo limeanza mwezi huu," askari mmoja wa mkoani Ruvuma alilieleza gazeti hili.

  Askari mwingine aliyefika kwenye ofisi za gazeti hili jana alisema anasikitishwa na hatua hiyo kwani imeharibu bajeti yote aliyoiweka kwa mwezi Januari.

  "Haya mambo ya ajabu sana, watu wamekatwa posho tena bila maelezo, wanataka askari sasa waanze kuwabambikia raia kesi ili kujiongezea kipato?"alisema.

  Polisi huyo alidai kuwa katika mshahara wake wa mwezi Desemba mwaka jana, alikatwa Sh150,000 jambo ambalo limemfanya akope kwa ajili ya kuwapeleka watoto shule.

  "Kukatwa posho bila maelezo ni ngumu sana na kimsingi hii inatupa shida kubwa kuzoea mazingira mapya, inaonekana hawa watu wanakata pesa zetu ili wawalipe Dowans (kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyozua zogo kutokana na mkataba tata),"alisema.

  Hata hivyo kukatwa kwa fedha hiyo kumeibua utata hasa baada ya uongozi wa jeshi la polisi kutupiana mpira na Wizara ya Fedha walipotakiwa kutoa maelezo kuhusu suala hilo.

  Wakati polisi ikisema yenyewe haihusiki na malipo ya askari wake, Wizara ya fedha na uchimi ilisesema inaandaa malipo ya wafanyakazi kulingana na maelekezo ya mwajiri husika.

  Msemaji wa polisi, Advera Senso aliliambia gazeti hili jana kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwani malipo ya polisi yanafanywa na Wizara ya Fedha (Hazina).

  “Hilo suala ungewauliza watu wa Wizara ya Fedha kwa sababu sisi sio watu tunaotoa mishahara,”alisema Senso na kuongeza kuwa wao huandaa malipo kisha kuyapeleka hazina kwa ajili ya malipo.

  Naye Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ingiahedi Mduma, alisema kuwa wizara haihusiki na suala la kupanga mishahara ya watu.

  "Tunacholipa wafanyakazi ni maagizo yanayotoka kwa mwajiri," alisema Mduma.

  Kwa mujibu wa Mduma jeshi la polisi haliko chini ya Wizara ya Fedha bali Ofisi ya Rais - Manejimenti ya Utumishi wa Umma, kwa hiyo mishahara inayopangwa kutoka Utumishi, ndiyo inayolipwa na Hazina.

  “Sisi ni kama mawakala tu suala la kulipa mishahara linatokana na mipango iliyotolewa na Utumishi na Jeshi hilo, kwa hiyo hatuwezi kubadilisha chochote tunacholetewa,”alisema.

  Lakini Mduma alidokeza kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya polisi ambao hawajalipwa fedha za pango kuwa tayari wamepewa nyumba za kuishi.

  “Inategemea kama hao polisi hawajalipwa inawezekana tayari wamegawiwa nyumba kwa hiyo kile kiasi walichokuwa wanapewa kwa ajili ya makazi kimefutwa,"alisema na kuongeza:

  "Au fedha za pango walizokuwa wakilipwa walikuwa wakilipwa kwa makosa. Kama ni hivyo basi, itabidi wakatwe kwa muda wote ule waliokuwa wakiingiziwa fedha hizo, hadi deni litakapomalizika.”

  Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo jana, Kamishna wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la polisi, Clodwig Mtweve alisema anahitaji muda kulifuatilia.

  Alisema, "Ndio kwanza umeniambia, sasa ngoja niwasiliane na kitengo cha mishahara nijue tatizo ni nini." Mtweve aliahidi kuwa atatoa maelezo ya suala hilo leo.

  Alipotafutwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Nahodha hakuweza kupatikana na baadaye katika mawasiliano ya simu haikupatikana, lakini msaidizi wake alisema kuwa waziri alikuwa safarini Indonesia kufuatilia shughuli za uanzishwaji mradi wa vitambulisho vya taifa.
  Polisi ni miongoni mwa kada za watumishi wa umma ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikia mishahara midogo, huku malipo hayo yakielezwa kuwa kichocheo cha kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya chombo hicho cha usalama wa raia.

  Ripoti ya utafiti uliofanywa na Tasisi ya Wanaharakati wa Maendeleeo barani Afrika (ForDIA) na kutolewa Januari 18, mwaka huu inaonyesha kuwa Idara ya Polisi ni kinara wa rushwa ikizitangulia idara nyingine za serikali ambazo ni Afya na Mahakama.
  Kwa mujibu Fordia, polisi inaongoza kwa kupokea rushwa, huku sekta za Afya, Mahakama, Elimu, Tanesco na idara za leseni na ushuru zikitajwa pia kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa.

  Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bubelwa Kaiza alisema “polisi ndio vinara wa rushwa kwa sasa”.

  Alisema utafiti huo unaonyesha kuwa polisi wanaongozwa kwa asilimia 81.9 kwa kupokea na kutoa rushwa. “Polisi imeendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kuongoza idara nyingine kwa kuwa na asilimia 85.3 mwaka jana kutoka nafasi ya pili ya asilimia 75.8 waliyokuwa wakiishikilia mwaka 2009,’’alisema Bubelwa.Kwa mujibu wa Fordia utafiti huo ulifanyika katika mikoa 11 ya Tanzania ambayo ni Dar es salaam, Tanga, Kagera, Manyara, Rukwa, Tabora, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Pwani na Mtwara. Utafiti huo pia umejumuisha serikali za mitaa 47 katika wilaya tofauti nchini na kulishirikisha watu mbalimbali wapatao 1,122 ambao waliulizwa maswali, lengo likiwa kujua kinara wa rushwa nchini.

  Kati ya watu hao 1,122 waliohojiwa wanaume walikuwa 646 na wanawake 476. Hata hivyo watu walioweza kutoa majibu walikuwa 367, ambapo wanaume walikuwa 248 na wanawake 119, huku Bubelwa akieleza kuwa watu waliohojiwa ni wanaoishi mijini na vijijini.

  Alisema sula la umri lilizingatiwa katika kuwahoji watu ambapo, waliohojiwa wote walizidi miaka 18, hivyo utafiti huo kuhusisha vijana, wazee na watu wenye umri wa kawaida.

  Alifafanua kuwa walipata majibu na maoni mbali mbali kutoka kwa wananchi kuhusu suala la polisi ambapo walielezwa kuwa watu hukamatwa kwa uonevu na hulazimika kutoa 'kitu kidogo' (rushwa), ili waachiwe hata kama hawakuwa na makosa, ambapo pia watu wenye makosa wanapofikishwa polisi huachiwa baada ya muda mfupi kutokana na kutoa kitu kidogo.
  Alisema lengo la utafiti huo ambao ulifanyika kwa nchi nzima ilikuwa ni kuanzisha majadiliano ili kuonyesha uelewa kwa wananchi na kuipa changamoto serikali juu ya mapambano ya rushwa.
   
 9. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  hahahahahaha alinichekesha mtu mmoja alikuwa akihutubia akasema polisi ni kama karai. linafanya kazi nyingi sana na ni la muhimu wakati wa ujenzi. nyumba ikikamilika halitakiwi hata kuonekana.......polisi wanatumwa kutupiga mabomu na kutuua...halafu wanakatwa mishahara kinyambilinsi!
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,592
  Likes Received: 4,697
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndiyo maana wameanza operesheni kamata kamata kwenye mabaa mchana kwa vile wanajua wanaokwenda kunywa wana vijisenti ili wazibe pengo hilo.Lakini siku zote mwiso wa ubaya ni aibu.
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  CCM Mission Accomplished.

  Posho zitarudishwa 2015 kabla ya uchaguzi mkuu
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mimi nataka wasilipwe kabisa, kwani wakati walipokuwa wanawaua watanzania huko Arusha walietegemea kuongezwa mishahara? Polisi wa Tanzania wanapenda sana kutumiwa na wanasiasa mafisadi sasa wanavuna walicho panda. Wasilalamike waandamane sasa kama hawajafukuzwa kazi na Mafisadi. Intelejensia yao haikufanyakazi na kuangalia kuwa wanataka kuktwa mishahara:laugh: Tena Wakome kabisa matatizo yao wasiyulete sisi huku mitaani wawapeleke hao hao Mafisadi wanao watumia kuua au kuwapiga mabomu ya machozi watanzania wenzao:clap2:
   
 13. t

  tarita Senior Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Laana za mauaji inawanyemelea,TUBUNI,NA MWACHE DHAMBI HII,vinginevyo si mishahara tu yatawapata makubwa zaidi.
   
 14. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Toa uongo wako hapa. Kwa mishahara ipi walio nayo hadi wakatwe laki 1 na wabaki na takehome
   
 15. M

  MFILIPINO Senior Member

  #15
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli serikali ya CCM kiboko, they use you when they are in need(ARUSHA CRISIS) and they dump you after getting satisfactions(just like a whole) kama walivyowakata mishahara. next time msikubali kutumika, halafu mnakuja kukopa kwa mangi mliyempiga kwa virungu na kumwaga damu yake! Mtakuwa wajasiri sana, mjue kwamba mnaishi na raia mnaowanyanyasa na mtawakimbilia mkiwa na shida sio serikali ya CCM
   
 16. nyondoloja

  nyondoloja Senior Member

  #16
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  sikuyakufa nyani mitiyote huteleza rana nimbaya ataa yes aliposema wakunisaliti tunaye yudaalikana kumbuka ruswa zuluma nk nichuhizo machoni pa mungu mtakachoking nakukubaliana duniani na mbinguni kimekubaliwa kwasasa kilio cha wanyonge tuliowengi ufujaj wamali za uma wachache ndowanafaidika kiujula waliowengihawanaimanina silikali tena kupoteana unakokuona hawapendi mungu kasikiyakiliochawanyonge ataungewashauli nisikiyorakufa
   
 17. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Amount iliyokatwa na kwamba ni kwa ajili ya Dowans inaweza kuwa si sahihi lakini kwamba wamekatwa hata mie jamaa yangu polisi kanithibitishia.
  Ila hainiumi wacha wakatwe tu maana tukiilaum serikali wantupiga mabomu.

  Bahati mbaya ni kwamba serikali inashamirisha rushwa maana lazima wafidie gap.
   
 18. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni sawa kabisa wakatwe ili wakati watu wako mstari mbele kudai uhuru na maisha ya kweli wajue na wasimamie ukweli maana nawao wanahitaji maisha mazuri.
   
 19. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Tena washukuru kuwa wamekatwa mimi nilikuwa nataka wasipwe kabisa. Wataujuwa UFISADI wa KIKWETE:clap2:.
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  inadawa zimeondolewa posho ya upelelezi na nyumba...soma mwananchii la leo
   
Loading...