polisi wajiandaa na uchaguzi mkuu, je kuna ulazima wowote

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,360
MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA KUKUTANA DODOMA KUJIPANGA NA UCHAGUZI MKUU UJAO
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi hapa nchini,
kesho Jumatatu Desemba, 14, watakutana mjini Dodoma kupanga mikakati mipya itakayofanikisha uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani utakaofanyika baadaye mwakani.

Mkuu wa Sera na Utafiti wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msadizi Mwandamizi Paul Ntobi, amesema leo mjini hapa kuwa mafunzo hayo yatafunguliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame.

Amesema kuwa mafunzo hayo pia yatawashirikisha Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia wa mikoa, Wakuu wa Upelelezi na Wakuu wa Operesheni maalum kutoka kila mkoa hapa nchini.

Kamanda Ntobi amesema mafunzo kama hayo pia yaliwahi kutolewa kwa Wakuu wa Polisi wa walaya na wa Upelelezi wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.

Amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, watahudhuria kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo yatakayofanyika mjini Dodoma.

Tayari washiriki wote wa mafunzo hayo kutoka bara na Visiwani wameshawasili mjini Dodoma kwa ajili ya mafunzo hayo.

Vyama 18 vya Siasa vyenye usajili wa kudumu hapa nchini, vinatarajiwa kushiriki katika kinyang'anyiro hicho huku baadhi ya vyama hivyo vikiwa na wagombea wa viti vya urais na vingine vikiwa na Wagombea wa Viti vya Ubunge na Udiwani pekee.


source: michuzi.blog
Wadau hii inashangaza kidogo, polisi wanakutana kupanga mikakati ya kufaniskisha uchaguzi mkuu, kusimamia usalama wakati wa uchaguzi mkuu ni sehemu ya kawaida kabisa ya kazi za kipolisi je wanahitaji kupanga mikakati, hii mbona inatia shaka.

Pili mafunzo yanafunguliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ambaye ni sehehmu muhimu katika kuandaa, kusimamia na mwishoni kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu, kwa nini wasimwite Prof Lipumba au sema Mbowe ili afungue huo mkutano, Mwenyekiti wa tume ana nini cha ziada cha kuwaambia.

Kwa nini Mwenyekiti asikae na wananchi wapiga kura kuwapa elimu ya Uraia ambayo wananchi wanaikosa na badala yake yuko busy na mapolisi.

Refa na kibendera waliochaguliwa na timu moja wakijifungia pamoja kwenye chumba wakitoka humo na kuchezasha mechi baina ya timu iliyowachagua refa na kibendera hao dhidi ya timu pinzani, kutakuwa na usalama kweli???

Naomba tulijadili hili.
 
Hii ni kweli kwa sababu nimeipata kutoka kwa mmoja wa maaskari kwamba hawa wakuu wamekwenda kupanga mikakati ya uchaguzi na tume ya uchaguzi.
Kwa jinsi nilivyoona miaka iliyopita polisi wakichezea kura zetu, nawambia michezo yao ni mauti kwetu!
Well, hii ningeielewa kama wangeipanga wakiwa na wawakilishi wa vyama ili na vyama vijue wajibu wao katika kushirikiana na walugaluga hawa.
Lakini hiki kitendo wanachojaribu kukifanya tume ya uchaguzi ni hatari kwa maisha yetu na maisha ya watoto wetu.
Kenya walijaribu kufanya hivi na matokeo tuliyaona.
Wananchi wakikasirika mimi nawaambia siku zote utawaua utawamaliza, na mwisho wewe utashindwa hata kutawala.
Msijidanganye nyie polisi tukichafuka hakuna wa kupona. Mkipona nyie na bunduki zenu vipi wazazi na wajomba na mashangazi na wadada na wakaka zenu?
Be carefull plz.
 
Back
Top Bottom