Polisi wajeruhiana kwa risasi wakimgombania mwanamke

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
500
Maafisa wawili wa polisi wamejeruhiana kwa risasi usiku wa siku ya Ijumaa baada ya kutokea ugomvi juu ya mwanamke katika klabu moja eneo la Barabara ya Thika, Nairobi nchini Kenya.

Ugomvi kati ya Konstebo Festus Musyoka na Konstebo Lawrence Muturi ulitokana na mwanamke aliyekuwa ameambatana na PC Musyoka, hali iliyomfanya Musyoka kutoa bastola na kumjeruhi PC Muturi mkononi.

Kama sehemu ya kujihami, PC Muturi alitoa bastola na kufyatua risasi iliyomjeruhi PC Musyoka shingoni, na risasi nyingine iliyompata mwanamke huyo, aliyejulikana kama Felistas Nzisa, tumboni.

Polisi wa Kituo cha Kasarani walitaarifiwa na raia mwema, ndipo walipowasili katika eneo la tukio na kufanikiwa kuwanyang’anya silaha maafisa hao.

Wote watatu wamekimbizwa hospitali ambapo wanaendelea na matibabu.

Chanzo: Citizen
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom