Elections 2010 Polisi wajazana Mwananyamala

ndugu wanajamvi... nimepita maeneo ya mwananyamala karibu na hospitali.. ile njia unayopita kama unataka kutokea kinondoni biafra NIMEKUTA MAGARI YA JESHI ZAIDI YA 10... Nashindwa kuelewa kwa nini yamejazana maeneo hayo.. tena yapo maeneo ya makazi,

jamani wakuu wa jf mmepatwa na nini! risasi zimerindima wapi? rekebisha heading very fast
 
zilifyatuliwa hewani mida flani hv mchana, watu walihisi kuibiwa kura wakajazana maeneo ya kituo lakini baadae walitawanywa kwa risasi zilizorushwa hewani.
Walidai kuna gari lilikuja na magumashi na pia mgombea wa udiwani wa makumbusho (ccm) alihusishwa na alijaribu kuwaletea wananchi ndefu ndo wakamvimbishia misuli. (eneo lenyewe mwananyamala maeneo karibu na manjunju a.k.a masaki wale atu mi nawaogopa)
Nilipita maeneo hayo kabla ffu hawajafika yaani nilitaani nipae.



.
 
Wadau kwa mujibu wa Channel ten... Risasi na Mabomu ya machozi vimerindima muda huu M'nyamala... Kuna mdau yupo huko atujuze zaidi? SOURCE CHANNEL TEN ya Rostam Aziz.

Ni taarifa za kweli, inasemekana diwani anayemaliza muda wake na ni mgombea wa CCM kwa jina Mutayoba alikuwa analeta watu tokja maeneo mengine kwa ajili ya kumpigia kura wananchi wakashtukia na kuanza kumuwashia moto akatoa bastola haikusaidia mpaka polisi walipoingilia kati na kutupa bomu la machozi.
 
huyo mutayoba atatukoma ngoja tuingie pale magogoni, lazima aende kisutu akajibu kesi
 
Tuachane na fikra potofu JWTZ ni binadamu kama sisi na hawako kwa ajili ya fujo.Tutulie nduguzanguni
 
Back
Top Bottom