Polisi waja na mpya mtuhumiwa wako wa JINAI kama ni kibaka tu hana HELA unaambiwa ni KESI ya madai nenda mahakani

Mungu Tusamehe Afrika

Senior Member
Jan 18, 2022
139
204
Habari,

Nimejaribu kufuatilia chanzo cha panya road na kukuta sababu moja wapo ni POLISI kuwaachia vijana wengi wanaofikishwa polisi kwa makosa ya utapeli wa mali au fedha au kukosa uaminifu kwa ujumla.

Mfano kijana anapatana kufanya kazi fulani au kuleta kitu fulani anakabidhiwa fedha na kuahidi atatekeleza baadae anakula ile pesa na kazi asifanye unaamua kwenda polisi ambapo wao wanakwambia hiyo ni kesi ya madai nendeni mmalizane au nenda mahakamani ufungue kesi ya madai.

Hapo ndipo shida inaanzia sasa angekuwa ni mtu mwenye hela ndiyo umemshitaki katika mazingira hayo basi angepewa kesi ya kujipatia pesa au mali kwa njia ya udanganyifu ili wapate KUMKAMUA kwenye dhamana na mambo mengineyo ila akiwa kibaka tu hana mbele wala nyuma wanajua hana cha kuwapa hawana shida nae wanameachia.

Kwa hali hii polisi hawana pa kukwepea juu ya kuongezeka kwa PANYAROAD ni wajibu wa serikali kytoa mafunzo juu ya mazingira ya makosa ya madai na makosa ya jinai hasa katika mazira kama haya.
 
Back
Top Bottom