Polisi waishiwa mabomu ya machozi maeneo ya Mjimwema (Kigamboni) na kukimbia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waishiwa mabomu ya machozi maeneo ya Mjimwema (Kigamboni) na kukimbia!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Henry Kilewo, Aug 14, 2012.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Leo wa kazi wa mji mwema kigamboni walifunga barabara baada ya kuamriwa kuondoka kwenye eneo la machimbo ya mawe na wananchio hawa kugoma, jambo hilo la kugoma lililazimisha polisi kutumia mabomu kama kawaida yake, ila la kushangaza polisi wameishiwa na mabomu hayo na kukimbia kusikojulikana baada ya wananchi kuwazidi nguvu.

  kwasasa jeshi la jwtz limewasili maeneo hayo na linaondoa matairi yalikuwa yamechomwa barabarani, kuwasili huko kwa jeshi hilo kumewafanya wananchi kutulia ila wapo maeneo hayo hayo ya tukio.

  UPDATE


  KWATAARIFA ZA AWALI ZINASEMA MWANANCHI MMOJA AMEPIGWA RISASI YA MGUU NA MWINGINE AMEPATA AJALI YA KUGONGWA NA PIKIPIKI WAKATI AKIWA KWENYE HEKA HEKA ZA KUJIOKOA. ENDELEENI KUFUATILIA KUPITIA HAPA NITAWAJUZA KILA KITU KINACHOENDELEA NIMEMTUMA KATIBU WA CHAMA WA JIMBO LA KIGAMBONI KWENDA ENEO LA TUKIO ILI CHAMA KIWEZE KUAPATA TAARIFA KAMILI NA SAHIHI ISIYOCHAKACHULIWA.

  Kwasasa RPC wa TEMEKE aamuru gulio la Mjimwema kigamboni kufungwa Gulio hilo hufanyika kila siku ya J4, Vijana zaidi ya 12 wakamatwa. kwasasa bado hali ni tete Police wamerudi eneo la tukio. wananchi wapo pembezoni huku wakisikika wakisema hapa kitaleweka tu, ni lazima serikali itusikilize wananchi tunataka nini. endelea kufuatia tukio hili kupitia hapa.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  hayo machimbo yako nje na ule mradi wao wa mji mpya?
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Naanza kukubaliana na wale waliosema wanajeshi wanatakiwa sasa waende vitani kwasababu wanagharamiwa tu na pesa za walipa kodi, kama hawafanyi kazi yao,sasa ndo wanatumika dhidi ya wananchi?Kazi ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi si ku police,nchi haiko vitani yote bayo ya nini?
   
 4. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Asante kwa taarifa mkuu, nafikiri walikuwa wajifua kwa ajili ya 2015
   
 5. Mzalendo2015

  Mzalendo2015 JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 1,946
  Likes Received: 2,301
  Trophy Points: 280
  Hii inadhihirisha kuwa kwa sasa Watanzania wamechoshwa na hizi harakati za Polisi za kupiga watu mabomu kila kukicha!

  Kwa maana nyingine wako tayari kwa lolote. Acha na hao JW waje na vifaru,risasi na SMG zao watapiga risasi zitaisha na mwisho watakimbia. Huo ndiyo utakuwa mwanzo wa kuikomboa nchi hii iliyo chini ya Mafisadi wa Chama cha Majambazi. Kila kitu kina mwanzo na mwisho wake.

  CCM wanapotamba kuwa watatawala nchi hii milele bila shaka wanajidanganya.
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Yana mwisho, nao waja.
   
 7. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata mwanao kama kila kosa unamtanga mwisho anajenga Usugu! Hii ni dalili kuwa wabongo wameanza kujenga Usugu wa Mabomu ya machozi!
   
 8. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  freedom is coming tomorrow!!
   
 9. B

  Bob G JF Bronze Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jeshi linajidhalilisha na kujiondolea heshima kwa umma
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kweli hawa polisi na wanajeshi waende vitani maana wanahamu.si wawapeleke somaria wakawasaidie wakenya.
   
 11. a

  annalolo JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vp kova hajafika huko awaite waandishi wa habari na kutoa ripoti zake za kizushi
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,545
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wanajeshi badala ya kulinda mipaka yetu mpaka Malawi wanatangaza kuwa ziwa nyasa ni mali yao kwa 100% wao wanakuja kuwatumikia mafisadi.
   
 13. b

  balosi Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walishaambiwa nchi haitatawalika wakang'ag'ania!
   
 14. W

  Wimana JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Nadhani hizo ni salaamu maalumu, wakati wa fidia za kuupisha mji mpya itabidi Serikali ijipange vilivyo.
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru kwa taarifa mkuu.
   
 16. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wamezidi kuwa wengi mjini hata makambini hawapajui siku hizi, full kuleta fujo mjini yu. Hatuombi vita lakini bora itokee waende huko ili wapunguze nghasia kwa wananchi mijini!
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,688
  Likes Received: 12,725
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa
   
 18. M

  Mwakalukwa Member

  #18
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti wametumwa na CHADEMA. Si punde utayasikia hayo!
   
 19. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwani tuna jeshi?.
  Jeshi gani linapigana na wanachi wasio na silaha? Tuna maPolisi wanaotumia sare tofauti tofauti!.
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,625
  Likes Received: 1,380
  Trophy Points: 280
  Chadema hao.. LOL! Kova na Nape watatoa matamko baadae stay tuned
   
Loading...