Polisi wahangaika kushughulikia tuhuma za Msemakweli kuhusu EPA, Manji na DPP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wahangaika kushughulikia tuhuma za Msemakweli kuhusu EPA, Manji na DPP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 8, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Polisi nchini limesema bado linaendelea na uchunguzi wa ushahidi uliotolewa na Mwanaharakati na Mwanasheria maaurufu, Kainerugaba Msemakweli, dhidi ya kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.
  Kampuni hiyo inadaiwa kukwapua Sh. bilioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (Epa), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
  Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso, alisema bado polisi wanaendelea na uchunguzi wao.
  Hata hivyo, alisema asingependa kuzungumzia zaidi kuhusu suala hilo na kuomba wananchi wawe na subira wakati polisi wakifanya uchunguzi. Alisema uchunguzi utakapokamilika, taarifa itawekwa hadharani.
  Habari za kuaminika zilizopatikana jana zinaeleza kuwa uchunguzi unaoendelea, unahusisha kuwahoji baadhi ya watu walionyooshewa kidole katika ushahidi uliowasilishwa na Msemakweli. Kwa mujibu wa habari hizo, watu wanaohojiwa kwa nyakati tofauti wanafikia 27.
  Hivi karibuni Msemakweli alidai amefanya uchunguzi na kupata ushahidi dhidi ya Kagoda, kampuni inayodaiwa kukwapua Sh. bilioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika Epa katika BoT.
  Alidai ushahidi huo aliuwasilisha kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).
  Alisema katika ushahidi wake huo kwa DPP, amewataja wamiliki saba halali wa kampuni hiyo, wakiwamo wafanyabiashara Yusuf Manji na aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
  Alisema pia aliwasilisha kwa DPP baadhi ya vielelezo vinavyoonyesha kwamba, wahusika hao saba waliratibu na kuiba dola za Marekani milioni 30.7 kutoka Epa.
  Alidai amefanikiwa kukusanya na kufahamu ushahidi unaowaunganisha moja kwa moja Rostam, Manji, Gulam Chakaar, Bahram Chakaar, John Kato, Barati Goda na Tabu Omary, kuwa ni wahusika wakuu katika wizi huo.
  Baada ya Msemakweli kutoa madai hayo, alihojiwa na kikosi kazi kinachoundwa na maofisa waandamizi kutoka vyombo vitatu vya dola.
  Vyombo hivyo, ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Jeshi la Polisi na Ofisi ya DPP.
  Akizungumza na NIPASHE jana, Msemakweli alisema hadi sasa amefanikiwa kwa asilimia 90 kuwasilisha ushahidi kwa kikosi kazi hicho.
  Alisema kwa uzito wa ushahidi aliokwisha kuuwasilisha, unafaa kutumika kufungua kesi mahakamani dhidi ya Kagoda.
  Hata hivyo, alisema anachosubiri hivi sasa ni kuwasilisha nyaraka za serikali kwa kikosi kazi hicho, zikiwa ni sehemu ya ushahidi dhidi ya Kagoda kuhusika kwake na wizi huo.
  Alisema tayari amekwisha kuzungumza na DPP, Eliezer Felesh na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Kamishna Robert Manumba, kuomba wamhakikishie kwa maandishi kwamba, iwapo atawasilisha ushahidi wa nyaraka hizo katika kikosi kazi hicho, hatashtakiwa kwa kumiliki nyaraka za serikali.
  “Nimeshaongea na DPP na DCI ili nisije ‘nika-chenjiwa’ baadaye kama nitawasilisha nyaraka hizo kwa kikosi kazi,” alisema Msemakweli.
  Septemba 2, mwaka huu, Msemakweli, alikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa amefanya uchunguzi na kupata ushahidi dhidi ya Kagoda, kampuni inayodaiwa kukwapua Sh. bilioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (Epa) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
  Alisema katika ushahidi wake huo uliouwasilisha kwa DPP, amewataja wamiliki saba halali wa kampuni hiyo, wakiwamo wafanyabiashara Yusufu Manji na aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
  Alisema pia aliwasilisha kwa DPP baadhi ya vielelezo vinavyoonyesha kwamba wahusika hao saba waliratibu na kuiba dola za Marekani milioni 30.7 kutoka Epa.
  Alidai amefanikiwa kukusanya na kufahamu ushahidi unaowaunganisha moja kwa moja Rostam, Manji, Gulam Chakaar, Bahram Chakaar, John Kato, Barati Goda na Tabu Omary, kuwa ni wahusika wakuu katika wizi huo.
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Haya ya ka aa goda yamefunikwa na ya misaada ya Cameron, Cameron amekuwa muwazi kwenu kama mnataka kuendelea kupokea misaada basi muwapishe wawatende kile wanachotendewa wengine.
   
 3. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa vizuri kama akina Rostam na Manji wakaenda Uingereza wakapewa hiyo misaada. Wakaachana na udokozi wa pesa ya makapuku wa Bongo. Haya shime Manji na Rostam nendeni kwa David Cameron kuna misaada chekwa.
   
 4. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2016
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  Tanzania shamba la bibi wachache wananeemeka kupitia serikali na raslimali za nchi....
   
 5. m

  mwembemdogo JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2016
  Joined: Feb 28, 2016
  Messages: 2,293
  Likes Received: 1,225
  Trophy Points: 280
  Hiyo kesi imekwisha funguliwa au bado?
   
 6. mamseri

  mamseri JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2016
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 682
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Yaan mpaka leo hawajamaliza upelelezi? Tunaomba JPM alichukue na hili kama kweli amejitoa mhanga
   
Loading...