Polisi wafunga baadhi ya barabara mjini moshi kuzuia wananchi kusikiliza kikao cha madiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wafunga baadhi ya barabara mjini moshi kuzuia wananchi kusikiliza kikao cha madiwani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mndeme, Apr 20, 2011.

 1. m

  mndeme JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna mdau kanipasha kuwa kwa sasa polisi wa mjini moshi wametanda mji mzima na wamefunga baadhi ya barabara ili kuwazuia wananchi wasihudhurie kwenye ukumbi wa halmashauri kusikiliza kikao cha madiwani kinachoendelea.

  Pia mkurugenzi amekimbia ukumbini akihofia ile hoja ya kuchukua viwanja vya wazi vilivyomilikishwa kwa cc.

  Je polisi ni mali ya chama tawala?

  Sipati majibu ni lini tutakuwa na demokrasia ya ukweli hapa tz.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwa nini wananchi wazuiwe ...? Mantiki yake ni ....?
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mijizi yote hii yaani polisi watasema wamepata habari za ki itelijensia kuwa kuna umwagaji mkubwa na uvunjifu wa amani utatokea ....
   
 4. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sijaelewa mkuu, kwa nini wanazuia wananchi wasihudhurie?
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ufisadi uliofanywa na ccm wakati wanaongoza halmashauri unawapa shida. Waligawana viwanja vya mji kwa wingi wao kwenye baraza sasa cdm ni wengi na wanampango wa kuyafuta maamuzi ya kifisadi waliyofanya. Wanaogopa wananchi wasisikilize huo mjadala. Nawashauri madiwani warekodi hata kwenye simu halafu waje watuhabarishe. Haya yatafika mwisho tu!
   
 6. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mh Jafari Meya mpambanaji usirudi nyuma mafisadi ni wengi pambana kamanda 2po pamoja Kamanda Hawa najua hapo kazi tuu msiwaonee huruma Wafisadi.
   
Loading...