POLISI WAFANIKIWA KUMWOKOA DC MOMBA MBEYA; Watatu wajeruhiwa na risasi, wanne wakamatwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,868
1,225
[h=2]Wednesday, November 28, 2012[/h]
By Pastor Gordon Kalulunga.

*Watatu wajeruhiwa na risasi, wanne wakamatwa...

TAARIFA zilizotufikia hivi punde ni kwamba askari Polisi wanawatawanya wananchi wa Kijiji cha Kamsamba,wilayani Momba mkoani Mbeya kwa ajili ya kumwokoa Mkuu wa wilaya hiyo Abiud Saudea

Hali hiyo ilijitokeza kuazia majira ya saa Nane mchana leo baada ya Mkuu hyo wa wilaya kufika kijijini hapo na kuanza kuhutubia huku viongozi hao wa wilaya wakikusudia kumrejesha madarakani Mwenyekiti wa Kijiji hicho Vitus Sauzen aliyetimuliwa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha.

Hali hiyo iliwakera wananchi na kuanza kuzomea jambo ambalo lilizusha vurugu mbele ya Mkuu huyo wa wilaya, kamanda wa polisi wa wilaya hiyo (OCD) na viongozi wengine.

Kutokana na fujo hizo, askari polisi waliingilia kati na kuwatawanya wnanchi na mabomu ya machozi hali ambayo haikufua dafu na kuamua kutumia risasi za moto ambazo zimejeruhi watu watatu ambao wamekimbizwa Hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani hapa.

Mbali na hao watu wanne wamekamatwa kwa kuhusika na uratibu wa fujo hizo wakiwemo viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kata na kijiji hicho cha Kamsamba.

Waliokamatwa na Polisi ni pamoja na Richard Nyoni, Michael Simfukwe ambao ni viongozi wa Chadema. Wengine ni Jofrey Dismas na Sabati Kigaya. 

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,335
2,000
Wanadhani wananchi bado ni wajinga wajinga eeh! Acha wapopolewe mawe.
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,832
2,000
Heri wangemshikisha adabu ili liwe somo kwa wanaodhani kuwa watanzani wote ni kondoo wehu. Taratibu watu wanaanza kubadilika, kuamka na kuukubali ukweli kuwa bila kujisimamia hakuna atayeleta ukombozi. Big up wanakijiji wa Kamsamba. Heri mngempasua msamba huyo mwizi aliyeletwa na rais kuwaibia.
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,919
2,000
Huko Kamsamba sio ndio anakotoka yule Mwandishi maarufu wa Makala ndugu Pascally Mayega a.k.a Simba Mangu? Hawa wameshaelimika na kujua namna ya kudai haki zao...Wanamsoma kila siku ndugu yao Mayega anavyomlilia Rais wake.
Ukurasa wa 18 wa Kitabu "Mwalimu Mkuu wa watu" una maneno haya " Elimu duni ya uraia kwa wananchi imechangia sana kuiweka hali hii kuwa kama ilivyo.Viongozi wanatumia ujinga na umaskini walionao wananchi kuwaghilibu. Watakuja kujuta pale wananchi watakapoitambua na kuielewa hali hii na kusema sasa basi, liwalo na liwe!" Uko wapi Mkuu Bujibuji? Nahisi kama na wewe unatokea maeneo haya!
 
Last edited by a moderator:

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,919
2,000
Huko Kamsamba sio ndio anakotoka yule Mwandishi maarufu wa Makala ndugu Pascally Mayega a.k.a Simba Mangu? Hawa wameshaelimika na kujua namna ya kudai haki zao...Wanamsoma kila siku ndugu yao Mayega anavyomlilia Rais wake.
Ukurasa wa 18 wa Kitabu "Mwalimu Mkuu wa watu" una maneno haya " Elimu duni ya uraia kwa wananchi imechangia sana kuiweka hali hii kuwa kama ilivyo.Viongozi wanatumia ujinga na umaskini walionao wananchi kuwaghilibu. Watakuja kujuta pale wananchi watakapoitambua na kuielewa hali hii na kusema sasa basi, liwalo na liwe!" Leo zamu ya DC, kesho itakuwa ya Pindamgongo na keshokutwa ya Mr Dhaifu nani anajua?Uko wapi Mkuu Bujibuji? Nahisi kama na wewe unatokea maeneo haya!
 
Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,328
2,000
Huyo DC alizoea kuwapelekesha Wasukuma wa Meatu! Anafikiri na huko wamelala kama Meatu? Wangemtoa ngeu ndo ingekuwa shega!!

Abihud Saideya umebugi step meeen!!! Huko hakusomeki meeeen!
 
PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,056
2,000
huyu DC alihongwa gari na kampuni ya uwindaji huko Meatu na pinda akakiri kuwa watamvua mafaraka, lakini leo kahamishwa , hawa ndi wakupiga mawe tu.
 
acanthocyte

Senior Member
Nov 27, 2012
178
250
Huko Kamsamba sio ndio anakotoka yule Mwandishi maarufu wa Makala ndugu Pascally Mayega a.k.a Simba Mangu? Hawa wameshaelimika na kujua namna ya kudai haki zao...Wanamsoma kila siku ndugu yao Mayega anavyomlilia Rais wake.
Ukurasa wa 18 wa Kitabu "Mwalimu Mkuu wa watu" una maneno haya " Elimu duni ya uraia kwa wananchi imechangia sana kuiweka hali hii kuwa kama ilivyo.Viongozi wanatumia ujinga na umaskini walionao wananchi kuwaghilibu. Watakuja kujuta pale wananchi watakapoitambua na kuielewa hali hii na kusema sasa basi, liwalo na liwe!" Uko wapi Mkuu Bujibuji? Nahisi kama na wewe unatokea maeneo haya!

Mkuu SG8 pamoja na kuwa anatokea huko mwandishi mahiri na mkongwe Pascally Mayega ''mwalimu mkuu wa watu'' lakin pia ndiko anakotokea Mbunge wa mbozi magharibi Ndugu David Silinde wa chadema. Wao elimu ya uraia walishaipata siku nyingi.
 
  • Thanks
Reactions: SG8

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,697
2,000
Huyo DC alikuwa hajui historia ya watu wa mkoa huo! Huwa hawana longo longo kwao nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe! Kandoro mwenyewe hana hamu!
 
nemasisi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,955
2,000
hii ndo safi, vinginevyo hatutaheshimiana, kuna watu huwa wanadhani wanaweza kufanya lolote popote, sasa huyu nadhani atakuwa amepata somo, naamini atawaambia madc wenzake ambao muda mwingi wanautumia kufanya kazi za ukada badala ya kuleta maendeleo kwa wananchi
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,268
2,000
Hawa jamaa waitwa ma DC na vyeo vyao vya "kishika uchumba" huwa wanajiona wapo salama sana na wana nguvu sana.Soon watabadilika na kuwa kafara nchi nzima.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
58,592
2,000
Ni furaha sana kusikia kuwa wasukuma wenzangu wa bonde la Kamsamba wameamka kiasi hicho. Safi sana
Huko Kamsamba sio ndio anakotoka yule Mwandishi maarufu wa Makala ndugu Pascally Mayega a.k.a Simba Mangu? Hawa wameshaelimika na kujua namna ya kudai haki zao...Wanamsoma kila siku ndugu yao Mayega anavyomlilia Rais wake.
Ukurasa wa 18 wa Kitabu "Mwalimu Mkuu wa watu" una maneno haya " Elimu duni ya uraia kwa wananchi imechangia sana kuiweka hali hii kuwa kama ilivyo.Viongozi wanatumia ujinga na umaskini walionao wananchi kuwaghilibu. Watakuja kujuta pale wananchi watakapoitambua na kuielewa hali hii na kusema sasa basi, liwalo na liwe!" Uko wapi Mkuu Bujibuji? Nahisi kama na wewe unatokea maeneo haya!
 
marejesho

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
6,642
2,000
Mpaka 2015 ifike tutaona mengi!!
DC na wenzake walitakiwa kusoma alama za nyakati mapema!!!
 
Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,480
2,000
Hapo ndio nawakubali watu JF, kuchonga ngenga mnaweza hasa mkiwa mbali na maeneo ya tukio na kupongeza wakati wengine wana risasi katika miili yao nyie mko roho kwatu.
Bado watu wanaweza kudai haki bila fujo na ndio tunapaswa kuelekea huko, ikibidi nyie mnaunga mkono muunge mkono mkiwa risasi katika miili yenu sio ya wenzenu
 
iseesa

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
943
0
Huyo DC alizoea kuwapelekesha Wasukuma wa Meatu! Anafikiri na huko wamelala kama Meatu? Wangemtoa ngeu ndo ingekuwa shega!!

Abihud Saideya umebugi step meeen!!! Huko hakusomeki meeeen!

Ingekuwa shega kama angeuawa kama kamanda Barlow ili MAGAMBA wajue kuwa watu wamechoka kunyanyaswa na sasa wanataka mapinduzi
 
Kirode

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
3,567
0
Songa mbele...........
Hapo ndio nawakubali watu JF, kuchonga ngenga mnaweza hasa mkiwa mbali na maeneo ya tukio na kupongeza wakati wengine wana risasi katika miili yao nyie mko roho kwatu.
Bado watu wanaweza kudai haki bila fujo na ndio tunapaswa kuelekea huko, ikibidi nyie mnaunga mkono muunge mkono mkiwa risasi katika miili yenu sio ya wenzenu
 
Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,424
2,000
Mleta uzi huu ni mwongo DC huyu mzee saidea yuko likizo nyumbani kwake samunge kwa babu wiki 2 zilizopita!
 
Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,475
2,000
Wanadhani wananchi bado ni wajinga wajinga eeh! Acha wapopolewe mawe.

mimi nimesikitika kwa kutokumpiga mawe. Wamezoea kuiba ndo mana wanataka wezi wenzao wawepo madarakani ili wasiwakosoe. Sasa mwenyekiti si alichaguliwa na wananchi? Amekiuka kazi tunamtoa, ndo sheria zilivyo, kwa nini ulazimishe?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom