Polisi waendelea kuuana kwa wivu wa mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waendelea kuuana kwa wivu wa mapenzi

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Oct 1, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Wimbi la askari kuuana kwa wivu wa mapenzi limeendelea kushika kasi nchini kufuatia tukio jingine la skari polisi, Mwajabu Ramadhani (22), mkazi wa Babati, mkoani Manyara, kuuawa kwa kupigwa risasi na askari mwenzake kwa sababu ya wivu wa mapenzi.
  Marehemu anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi kifuani na kwenye goti na mtuhumiwa, Willibrod Turuwahi Gwandu (26).

  Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Palmera Sumari, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 29, mwaka huu, majira ya saa 3.00 asubuhi katika kambi ya Magereza, mkoani Manyara.
  Kamanda Sumari alisema kuwa siku hiyo ya tukio, marehemu alikuwa katika gereza hilo akiangalia wafungwa wa kike na ndipo alipotokea mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani na kuanza kumuuliza sababu za kumuacha kimapenzi.

  “Wakati huyu askari akijibu swali aliloulizwa, alishtukia anapigwa risasi kwa kutumia bunduki aina ya SAR, sehemu ya kifuani kulia na kwenye mguu wa kulia chini ya goti,” alieleza Kamanda Sumari.

  Kamanda huyo alisema kuwa baada kumpiga risasi, mtuhumiwa huyo alijipiga risasi katika eneo la kidevu kwa lengo la kutaka kujifyatua ubongo, lakini bahati mbaya haikuwa kama alivyotarajia badala yake kujikuta akiwa amejeruhiwa.
  Kwa mujibu wa Kamanda Sumari, polisi waliokuwepo eneo la tukio walimkimbiza mtuhumiwa huyo katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, ambako amelazwa na kwamba anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
  Kamanda Sumari alisema kuwa baada ya matibabu, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji.
  Tukio hili linatokea ndani ya mwezi mmoja baada ya askari polisi mwingine mkoani Iringa, G13 Mashauri (24), kujiua kwa kujipiga risasi mbili chini ya kidevu kutokana na wivu wa mapenzi.
  Katika tukio la Iringa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema Mashauri alijipiga risasi na kufa papo hapo saa 3:00 usiku katika eneo la makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa lililipo Gangilonga, katika Manispaa ya Iringa.
  Alisimulia kuwa kabla ya G13 Mashauri kujiua, alikuwa kwenye lindo eneo la benki ya CRDB ambako aliingia saa 12:00 jioni ya siku hiyo na kutoka saa 1:30 usiku kuelekea nyumbani kwa askari mwenzake wa kike.
  Ilidaiwa kuwa zamani Mashauri na askari huyo wa kike, WP 7137 Zahara, walikuwa na mahusiano ya kimapenzi, lakini baadaye waliachana kutokana na kutofautiana.
  Baada ya kuachana kila mmoja aliendelea na mambo yake, lakini siku ya tukio hilo inawezekana Mashauri alikuwa akifuatilia nyendo za Zahara.
  Kamanda Mangalla alisema askari huyo akiwa amevaa sare akiwa na silaha, aliondoka kwenye lindo lake na kuelekea eneo la Mafifi, Kihesa nyumbani kwa Zahara na kwamba baada ya kufika alibisha hodi na kufunguliwa mlango.
  “Baada ya kufunguliwa alimkuta Zahara amekaa na kijana mmoja aitwae Sunday Tumaini, mfanyakazi wa Bayport, akawatishia, ndipo Zahara alipiga kelele kuomba msaada,” alisema Mangalla na kuongeza:
  “Askari mwingine aliyekuwa amepanga kwenye nyumba moja na Zahara alitoka na kusaidia.”
  Alisema baada ya kelele hizo, askari huyo aliingilia kati kumsaidia Zahara kwa alimnyang’anya marehemu silaha aliyekuwanayo na baada ya kunyang’anywa, aliondoka eneo hilo na kwenda kwenye lindo jingine katika eneo la Gangilonga kwenye nyumba ya wageni ya polisi ambako aliwakuta askari wengine na kuanza kuzungumza nao.
  Mangalla alisema kuwa baada ya kuzungumza nao, ghafla alimnyang’anya silaha askari mwenzake na kuondoka nayo kwenda kwenye eneo alikojiulia kwa kujipiga risasi mbili chini ya kidevu.


  Wakati huo huo, Lembris Edward (32), mkazi wa Longido Madukani, ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni, kwa tuhuma za mapenzi.

  Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Basilio Matei, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 27, mwaka huu, saa 2:30 usiku katika eneo la Longido Madukani, kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mtuhumiwa, Joshua John (32), ambaye alikuwa mpenzi wake.

  Matei alisema kuwa sababu ya mauaji hayo ni wivu wa mapenzi na kuongeza kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mbona kila siku ni maaskari tu wanaouana kwa wivu wa mapenzi?
  Tena ni wa vyo vya chini wenye mishahara midogo sana na maisha magumu sana.
  Hawa wanakabiliwa na msongo wa mawazo.
  wanahitaji huduma ya ushauri wa kisaikolojia na kuboresha maisha yao.
   
 3. e

  ejogo JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh! Hiyo miaka ya hao askari inaonyesha bado ni wadogo sana. Bado hawakukomaa mpaka waachiwe wacheze na vitu vya moto.
   
Loading...