Polisi wadaiwa kukataa kufanya uchunguzi wa aliyepotea katika mazingira tata hadi wapewe hela na ndugu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
981
2,659
Askari wa Kituo cha Polisi Misigiri katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida wanadaiwa kukataa kufanya uchunguzi wa tukio la Stella Jingu (38) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha miaka miwili iliyopita wakitaka kwanza wapewe fedha na ndugu wa mwanamke huyo.

Inadaiwa askari hao (majina tunayahifadhi) walitaka wapewe Tsh 45,000 ndipo waweze kufuatilia suala hilo kwenye mtandao lakini ndugu waliposhindwa kutoa fedha hizo kutokana na hali ngumu ya maisha waliyonayo, wakasema na wao hawawezi kufuatilia tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Binilith Mahenge, alielezwa hayo na mtoto wa mwanamke huyo aliyepotea, Roda Philipo wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Kijiji cha Misigiri wilayani Iramba.

Roda alisema mama yake alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Februari 2020 ambapo siku ya tukio, mlango wa nyumba aliyokuwa akiishi ulikutwa upo wazi huku nguo na vitu mbalimbali vilivyokuwamo ndani vikiwa vimetupwa ovyo.

Alisema kuwa baada ya tukio hilo, kaka wa mwanamke aliyepotea aitwaye Nyerere Jingu na shangazi yake Mama Zahara, walikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Misigiri lakini katika hali ya kushangaza askari waliokuwapo zamu, walisema hawawezi kufuatilia suala hilo hadi wapewe pesa.

Roda alisema baada ya kugonga mwamba polisi, walikwenda kutoa taarifa kwa viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Misigiri ambapo Mwenyekiti wa Kijiji, aliitisha mkutano wa kijiji kuwaomba wananchi kama kuna mtu alikuwa anamdai Stella Jingu (aliyepotea) ajitokeze alipwe ili amrudishe alikompeleka.

Hata hivyo, hakuna mtu yeyote aliyejitokeza na hadi sasa wamekuwa wakifuatilia wenyewe kwa ndugu wengine waliopo nje ya wilaya na vijiji jirani bila mafanikio huku Jeshi la Polisi likituhumiwa kutofuatilia tukio hilo.

"Mama yangu alipotea tangu 2020 na hajulikani aliko hadi sasa, tukienda polisi wanasema tutoe fedha ndipo watafuatilia suala hili, lakini hali yetu kiuchumi ni mbaya. Tumeshindwa kupata fedha zinazohitajika, tunakuomba Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa utusaidie, hatujui kama mama yetu yupo hai au alishakufa," alisema.

Kufuatia malalamiko hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mahenge, alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Lucas Mwakatundu, kufuatilia suala hilo na apewe ripoti ndani ya wiki mbili.

"Kama kweli polisi hawakulifanyia kazi tukio hili kwa kutaka kwanza wapewe pesa, itabidi hatua zichukuliwe kwa wahusika, pia muangalie kama walisajili tukio hilo hapo kituoni," aliagiza.

Source: IPP
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,938
17,247
Kinachokera zaidi polisi watateteana na hakuna hatua yoyote itachukuliwa. Utashangaa jibu litakalotolewa na polisi
 
Kunguru wa Manzese

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
12,550
16,860
Duuh huyu kapotea kweli miaka miwili hata kupiga simu nyumbani au kusikia taarifa

Kuna watu watasema yupo kwa lifather analilea
 
maneka

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
603
566
Binafsi sijawahi kuwa na imani na kiumbe kinachojiita au kuitwa Polisi wa Tanzania!

Hawa utawasikia wameua mfanya biashara wa madini, wameshiriki kupora, wamebambikizia kesi, kudai rushwa, wameonekana wakimteka mtu na haijulikani kashikiliwa kituo gani n.k

Naogopa kuuliza kama waliwapata walio mshambulia Tundu Lissu huko Makao Makuu ya Nchi tena kipindi cha bunge.

Kama bado huyo mkulima wa kijijini polisi gani wa Nchi hii atajisumbua bila pesa.

Najaribu tu kuwaza kwa maandishi. Wahaphithina msinichukie.
 
Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
36,592
39,322
Huko ni nyumbani kwa mkuu wa fedha, mambo haya makubwa hivi ya kipotea mtu tokea 2020 hakuyasikia?

Hivi ule mnara wa yule mwamba umeshajengwa?
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
17,285
30,303
Askari wa Kituo cha Polisi Misigiri katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida wanadaiwa kukataa kufanya uchunguzi wa tukio la Stella Jingu (38) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha miaka miwili iliyopita wakitaka kwanza wapewe fedha na ndugu wa mwanamke huyo.

Inadaiwa askari hao (majina tunayahifadhi) walitaka wapewe Tsh 45,000 ndipo waweze kufuatilia suala hilo kwenye mtandao lakini ndugu waliposhindwa kutoa fedha hizo kutokana na hali ngumu ya maisha waliyonayo, wakasema na wao hawawezi kufuatilia tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Binilith Mahenge, alielezwa hayo na mtoto wa mwanamke huyo aliyepotea, Roda Philipo wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Kijiji cha Misigiri wilayani Iramba.

Roda alisema mama yake alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Februari 2020 ambapo siku ya tukio, mlango wa nyumba aliyokuwa akiishi ulikutwa upo wazi huku nguo na vitu mbalimbali vilivyokuwamo ndani vikiwa vimetupwa ovyo.

Alisema kuwa baada ya tukio hilo, kaka wa mwanamke aliyepotea aitwaye Nyerere Jingu na shangazi yake Mama Zahara, walikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Misigiri lakini katika hali ya kushangaza askari waliokuwapo zamu, walisema hawawezi kufuatilia suala hilo hadi wapewe pesa.

Roda alisema baada ya kugonga mwamba polisi, walikwenda kutoa taarifa kwa viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Misigiri ambapo Mwenyekiti wa Kijiji, aliitisha mkutano wa kijiji kuwaomba wananchi kama kuna mtu alikuwa anamdai Stella Jingu (aliyepotea) ajitokeze alipwe ili amrudishe alikompeleka.

Hata hivyo, hakuna mtu yeyote aliyejitokeza na hadi sasa wamekuwa wakifuatilia wenyewe kwa ndugu wengine waliopo nje ya wilaya na vijiji jirani bila mafanikio huku Jeshi la Polisi likituhumiwa kutofuatilia tukio hilo.

"Mama yangu alipotea tangu 2020 na hajulikani aliko hadi sasa, tukienda polisi wanasema tutoe fedha ndipo watafuatilia suala hili, lakini hali yetu kiuchumi ni mbaya. Tumeshindwa kupata fedha zinazohitajika, tunakuomba Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa utusaidie, hatujui kama mama yetu yupo hai au alishakufa," alisema.

Kufuatia malalamiko hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mahenge, alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Lucas Mwakatundu, kufuatilia suala hilo na apewe ripoti ndani ya wiki mbili.

"Kama kweli polisi hawakulifanyia kazi tukio hili kwa kutaka kwanza wapewe pesa, itabidi hatua zichukuliwe kwa wahusika, pia muangalie kama walisajili tukio hilo hapo kituoni," aliagiza.

Source: IPP
Polisi Wana matatizo lakini hii habari naamini imetiwa chumvi. Mtu akipotea ukienda kuripoti unapewa Muda si chini ya saa 24 ndo urudi kufungua Taarifa. Na katika Hali ya kawaida upoteaji wa Bi Stella unaonekana awali ilikuwa ni upotevu wa kawaida. Katika suala hili ndugu wanahusika zaidi kumtafuta ndugu Yao kuliko Polisi maana Hakuna kesi zaidi ya Taarifa ya kawaida ya kupotea kwa Mtu.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
26,973
30,055
Binafsi sijawahi kuwa na imani na kiumbe kinachojiita au kuitwa Polisi wa Tanzania!

Hawa utawasikia wameua mfanya biashara wa madini, wameshiriki kupora, wamebambikizia kesi, kudai rushwa, wameonekana wakimteka mtu na haijulikani kashikiliwa kituo gani n.k

Naogopa kuuliza kama waliwapata walio mshambulia Tundu Lissu huko Makao Makuu ya Nchi tena kipindi cha bunge.

Kama bado huyo mkulima wa kijijini polisi gani wa Nchi hii atajisumbua bila pesa.

Najaribu tu kuwaza kwa maandishi. Wahaphithina msinichukie.
tafuta hela mkuu.

ukikosa hela hata kaka yako usimwamini.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
26,973
30,055
Polisi Wana matatizo lakini hii habari naamini imetiwa chumvi. Mtu akipotea ukienda kuripoti unapewa Muda si chini ya saa 24 ndo urudi kufungua Taarifa. Na katika Hali ya kawaida upoteaji wa Bi Stella unaonekana awali ilikuwa ni upotevu wa kawaida. Katika suala hili ndugu wanahusika zaidi kumtafuta ndugu Yao kuliko Polisi maana Hakuna kesi zaidi ya Taarifa ya kawaida ya kupotea kwa Mtu.
halafu wakaomba 45k😁😁😁

ndio maana hata majina yamefichwa maana hao watu hawapo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom