Polisi wadaiwa kujeruhi watu wanne mgodi wa Nyamongo

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Polisi wadaiwa kujeruhi watu wanne mgodi wa Nyamongo Send to a friend
Friday, 15 July 2011 20:23
0diggsdigg

Anthony Mayunga, Mara
POLISI wanaolinda mgodi wa Nyamongo unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick North Mara, wanadaiwa kujeruhi watu wanne kwa kuwapiga risasi eneo la mgodi wa Nyabigena, kwa kile kinachodaiwa kukutwa
wakichukua mchanga unaosadikika kuwa na dhahabu.

Tukio hilo lilitokea saa chache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha, kuzuru Nyamongo na kutangaza kuondoa polisi eneo hilo, kutokana na kutuhumiwa kutumia nguvu kubwa na kuingiza taifa kwenye migogoro isiyo ya lazima.

Akizungumza kwa simu jajan, Diwani wa Kata ya Kemambo, Wilson Mangure,alisema tukio hilo lilitokea Julai 14, saa 5.45 usiku eneo la Nyabigena, Kijiji cha Kewanja.

Kemambo alitaja waliopigwa risasi kuwa, ni Mwita Masaite, Mwita Marembora, Chacha Marembora, wote wakazi wa Kijiji cha Kewanja, Kata ya Kemambo na Kikoma Mogeko, mkazi wa Kijiji cha Nyangoto, Kata ya Matongo.

“Baada ya kupigwa waliachwa hapo, ndugu zao walikwenda kuwachukua,naambiwa wawili wako Hospitali ya Tarime, wengine sijui walikopelekwa,” alisema Kemambo.Alisema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifusi kinachomwagwa karibu na makazi ya watu, huwafanya wananchi kudhani kina mawe yenye madini ya dhahabu.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho ambaye hakutaka kutajwa,Alidai chanzo kinatokana na polisi kutaka wapewa fedha ili kuwaruhusu wananchi kuingia, lakini walikataliwa na vijana hao waliingia kwa kutumia ubabe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/ Rorya, Deusdedith Katto, alisema hana taarifa na tukio hilo.
Pia, Msemaji wa Kampuni ya African Barrick Gold Mine, Tewel Tewel,alisema hakuwa na taarifa hizo, huku akiahidi kufuatilia suala hilo.

 
hii nchi sasa! sasa hicho kifusi chao ya nini kwenda kukimwaga karibu na makazi? they have ample space! halafu polisi wanawaona wezi (kwa maana ya mtu achukuaye mali isiyo yake), wamewapiga pengine labda wali-resist kukamatwa, sasa inakuwaje wanawatelekeza! nilidhani utaratibu ni ukifanikiwa kumkamata mwizi unampeleka polisi, kama ameumia unampeleka hospitali chini ya ulinzi na wengine wanasomewa mashtaka hosp!ina maana hawa hawafunguliwi mashtaka,wameshapata hukumu yao?
 
Du kwa kweli, imebabakia masaa wananchi kuchukua sheria mkononi, mambo ya ajabu hayo.
 
Polisi hawana cha kufanya kwenye huo mgodi kazi ni kupiga risasi raia tu?nchi hii haina utu kabisa.vipi kama raia wataamua kwenda kulipa kisasi?
 
Back
Top Bottom