Polisi wachukua wajibu wa Miundombinu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wachukua wajibu wa Miundombinu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chereko, Aug 21, 2009.

 1. C

  Chereko Member

  #1
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Polisi kwa sasa wameweka uzito mkubwa wa kusimamia foleni na magari barabarani (Nawapongeza kwa jitahada zao) nadhani Bw Mwema kama sikosei idadi ya askari barabarani itakuwa imeongezeka maradufu hivi karibuni - hii inadhihirishwa na kuona sare za polisi wa kawaida zikivaliwa na kofia nyeupe. Endapo wenzetu wa Miundombinu wangefanya kazi zao barabara na kutimiza wajibu wao kwa kuangalia kwa makini mwelekeo wa nchi na mahitaji halisi ya miundombinu hali hii leo isingekuwepo!!! Wizara ya Miundo mbinu itimize wajibu wake tumechoka na hatupendi muwabebeshe Polisi udhaifu wenu - wana kazi zao kulinda usalama wa raia na sio kujipanga barabarani kuhimiza foleni.


  Wananchi tunalipa kodi ambayo sehemu yake ni mishahara ya Polisi, wanapozidi kwa idadi bila sababu pengine pesa hizo zingefanya kazi ingine au tu kuboresha maslahi ya Polisi kuwa na jeshi dogo lenye nguvu na askari wenye ari ya kufanya kazi zao barabara!
  • Wizara haikuona kuwa mfumo wa usafiri wa umma DSM ni mbovu na haufai kiasi kwamba wananchi wanakopa, wanajinyima (au hata wanafanya ufisadi) ili waweze kujipatia kausafiri? Kila mtu anaponunua gari, barabara ziko wapi?
  • Wananchi badala ya kutumia pesa kidogo walizonazo kwa kazi za maendeleo yao wanagharamia magari - mafuta, matengenezo, leseni za barabara oh Uwiiiiiiiii
  • Hivi kwa nini msifikirie kuanzisha mfumo wa kueleweka wa usafiri wa umma, funga daladala weka mwekezaji mmoja awekeze kwenye mabasi makubwa yanayofata ratiba sio kukaa na kungja abiria wajae, mbona DSM Motor Transport (DMT) miaka ile usafiri ulikuwa bomba DSM (kabla UDA kuboronga?) Kwa kweli kwa DMT, uliweza kuwa na uhakika wa kutumia basi kwenda uwanja wa ndege, ukafika kwa wakati ukiwa nadhifu na kuwahi ndege yako, ukashuka mbele tu ya jengo la abiria kule uwanja wa zamani. Ilikuwa makosa makubwa kutaifisha DMT (mambo ya mrengo wa kushoto tuache hayo).
  • Wengi tuna magari lakini kama upo usafiri wa kueleweka wa umma tutayafungia ndani tutumie kwenda sokoni, kanisani na arusini barabara zitapumua. Acheni longo longo za RBT barabara zenyewe ziko wapi?
  • Ile International school iliyopo Upanga (hii ni mojawapo tu) - karibu kila mtoto analetwa na gari asubuhi na kurudishwa jioni shule inapofungwa barabara za Ali Hassan Mwinyi, UN zinapumua, zikifunguliwa tu ngoma inaanza. Kwa nini wasiletwe na mabasi ya shule au hamisheni shule hiyo kwa kweli pale Slender Bridge ni kazi kubwa wakati shule inaendelea!!! Serikali si ina mkono pale? Mzee Lukuvi vipi hapo? Changamkia tenda basi!
  • Malori yanayotoka bandarini ni kero kubwa barabara za Mandela, Sam Nujoma na Morogoro. Ule mtazamo wa awali (Mwanya wa Bandari) haupo tena kwa kuwa sehemu za Mabibo, Tabata n.k. tayari ni makazi ya watu wengi wa Jijini - Je MID hawakuona mabadiliko haya?
  Pengine hayo matatu tu yaani
  1. Usafiri wa Umma wa kueleweka unaotumia saa na ratiba na sio ule wa daladala kupigania na kuongoja abiria wajae
  2. Kusisitiza mabasi ya wanafunzi badala ya magari binafsi kupeleka watoto shuleni
  Na kwa baadae
  1. Kujenga "Mwanya wa bandari" mpya nina maana ya "Port access road", malori yakitoka bandarini yaanze huko kwa huko kwenda bara
  yakifanyika hayo labda ndoto za "daraja za kuruka" hazitakuwa na haja ya mara moja kwani ni gharama kubwa
   
Loading...